Wassira Asema Marekebisho Ya Muswada Wa Katiba Unaorejeshwa Bungeni Ni Juhudi Zao

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,651
2,627
Huyu mzee alikuwa akihojiwa ma TBC.Ameulizwa swali kuwa kwa nini wanarejesha muswada huo wakati ulipitishwa hivi karibuni.Wahasira akafura akasema serikali ndo imeona mapungufu na mtu yeyote asijisifu kuwa kamshauri rais,na akakanusha mh rais kubembeleza wabunge wa ccm wasisusie leo wakti muswada huo ukirejeshwa
 
Ujuha hauna dawa, akili za magamba zinawatosha wao tu. Anadhani huu ni mwaka 1980 ambapo walikuwa wanahodhi habari, wanachokitaka kisikike na kiaaminiwe ndicho hicho kilichowekwa hadharani. Leo hii anategemea kuna mwenye akili zake atausikiliza ujuha wake?
 
Hajamaliza evolution, achana nae, kwani bado nawashangaa watu wa Bunda kana kwamba hakuna mutu mwingine wa kuwawakilisha, mbuzi huyu, achana nae
 
Wakati anahojiwa sura yake ilikuwa inamshitaki kwamba anasema uongo! Hata maswali aliyoulizwa hakuyajibu bali amekwepa kwa kujifanya anatoa background informan, mpaka muda unaisha hata swali hajajibu!
 
A.D umeua tehe tehe tehe 'zinjanthropuz'.wasira njaa zinamsumbua,afu mbona hii wizara ya uhusiano na uratibu wanapewaga 'ajuza' tu? Nakumbuka mzee kinng'e mwiru.yaonyesha hakuna kazi pale
 
Huyu mzee alikuwa akihojiwa ma TBC.Ameulizwa swali kuwa kwa nini wanarejesha muswada huo wakati ulipitishwa hivi karibuni.Wahasira akafura akasema serikali ndo imeona mapungufu na mtu yeyote asijisifu kuwa kamshauri rais,na akakanusha mh rais kubembeleza wabunge wa ccm wasisusie leo wakti muswada huo ukirejeshwa
Mkuu, una uhakika wakati anaulizwa hilo swali na mwandishi hakuwa amelala?.........haaminiki huyu!!

wasira%2Bchapa%2Busingizi.jpg
 
Mna muda wa kuchezea ninyi mnaopata wakati wa kumuangalia wassira akiongea kwenye tv.
Hawezi kuongea jambo lolote lenye maana hata siku moja. Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kuongea mbele ya camera kwamba marekebisho ya sheria ya katiba mpya yanafanyika bila shinikizo na ushauri wa chadema, nccr mageuzi na asasi za kiraia?
 
Hahahahahahahahahaha,wasira anaota kwelikweli eti jitihada za serikali ndio zimeleta mabadiliko haya mmmh,hata mtoto mdogo anaelewa.
 
Wadau leo asubuhi Waziri Wassira alikuwa anahojiwa TBC1 kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya mchakato wa Katiba unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni. Cha kusikitisha na kutia aibu ni kwamba Wassira badala ya kuongea kama Waziri wa Serikali ameongea kama mwanapropaganda wa CCM tena mwenye uelewa wa chini kabisa pungufu ya ule wa Tambwe Hiza. 1. Kwanza ameongea uongo kuwa marekebisho yanayokusudiwa sio maoni ya CDM ni maoni ya rais na CCM na kwa hiyo hakuna lolote linalotokana na maoni ya CDM. Wakati anaongea haya alikuwa anaangalia chini kwa aibu! Shame on him!!!2. Amekataa kuwa hakuna wabunge wa CCM wasiopenda muswada huo kuletwa tena bungeni wala hawana tatizo lolote na mwenyekiti wao wa chama yaani JK kwa kukutana na CDM na kusababisha muswada huo kurudishwa tena bungeni! Huu ni uongo pia kwa sababu wote tunajua walivyomuwekea bifu!3. Anajaribu kujenga hoja kuwa marekebisho hayo ni madogo na ni ya serikali na sio kwa kushinikizwa na kwamba waandishi wa habari wanaeneza uzushi!4. Alikuwa anakwepa maswali ya msingi na kuzungumzia mambo yake mwenyewe akilenga kuwaponda CDM hadi mtangazaji akawa anaduwaa kwani alitegemea anaongea na waziri wa serikali kumbe anaongea na kada wa chama!Kwa maoni yangu waziri kuwa mbabaishaji kiasi hiki ni dalili za kushindwa! Uelewa wake pia ni mdogo sana kama anashindwa kuelewa kuwa ni wakati gani anazungumzia mambo ya chama na wakati gani anazungumza mambo ya serikali!
 
Hivi kumbe bado kuna watu huwa wanamsikiliza huyu "political dinosaur"?
 
Back
Top Bottom