Wassira amjibu Lazaro Nyalandu!

Wassira amjibu Lazaro Nyalandu!

alikuwa anamaanisha yule mchezaji mpira wa zamani wa simba na taifa stars hahahahaha jf

Ungechangia mada husika ingekuwa vema zaidi,! Swala la kukosea majina ni swala dogo sana na pia lilisharekebishwa Mkuu!

Embu jikite kwenye "Hoja" iliyoko jukwaani ili tukujue ni Gteat Thinker wachana na Mboyoyo!
 
Lazima kuna mtu amehaki akaunti yako,..... Wewe wa kumsema mwanaCCM mwenzio...??? Wengine mmekunywa maji ya benera ya chama, yaani hata mwanachama akosee vipi, huwa mnamtetea....

Hahah!
Huwajuhi MACCM wewe, Ukiona Hivyo ujue kuna Vita Vya URAISI hapo, So angaliwi mtu usoni.
 
Sikuona ajabu kwa kauli kama ile kutoka kwa nyalandu mana sio mtu makini, amefika hapo kwa kujipendekeza pendekeza sio kwa umakini wa kiutendaji. Ntashangaa sana kama rais atamrudisha katika baraza la mawaziri
Ona ulivyo mjinga na zuzu, ni lini baraza la mawaziri lilivunjwa mpaka utake Nyalandu asirudi? Jinga kabisa kabisa wewe.
 
Kaka umenena, majangili wanapeta kwa mwendo wa kasi, Jana tu Tembo mmoja akiwa na mtoto wake wamepigwa risasi nne nne, na kufa hapohapo. Ni katika eneo fulani la hifadhi ya Selous. Nyalandu yupo sahihi kwani ripoti ya lembeli ililenga kuteka hisia za wengi na kushinda, lakini yeye anajaribu kuzitoa hisia hizo na kuwarejesha watu kwenye uhalisia kwan hakuna opereshen ya kijesh isiyokuwa na madhara hata kidogo. Uhalisia Ni Kwamba Tembo Wanauwawa Tena Kasi Inaongezeka Kurudi Ile Ya Tembo 30 Kuuwawa Kwa Siku.
 
Kila operesheni huwa na madhala yake hususani Kama haikuratibiwa Vizuri kisayansi na miiko ya kazi kuzingatiwa kwani hata Operesheni Kimbunga nayo ilikumba waliokuwemo na wasio kuwemo lakini baada ya wanasiasa kuziingilia hizi Operesheni Sasa Majangiri na Wahamiaji wote wameludi Kama zamani na sasa Majangiri ni Kama hawana wa kuwazuia Tembo wanateketea kwa kasi ya Ajabu Majangiri wao wapo kazini wakati Wasira na Nyalando na akina Limbeli wanaendeleza Malumbano kule mbugani Tembo wanateketea : Ushauri wa Bure Tunaiomba Serikari ifanye Operesheni ingine lakini ifanyike Kisayansi zaidi yenye kuzingatia Haki za Binadamu kabla ya Operesheni watumwe wapelelezi wa Siri kwenye vijiji vyote vilivyo jirani na Hifadhi za wanyama ikibidi wachukuliwe wanavijiji waminifu watumike Kama informer wa kuleta Habari za kiintelijensia ili Operesheni ikifanyika iweze kuwatokomeza Majangiri kirahisi kinyume na hapo Malumbano hayatakwisha huku Tembo wanateketea kwa kasi

Mkuu ushauri wako ni mzuri sana na ndivyo inatakiwa iwe. Kabla operation kamata kamata haijaingia uchunguzi wa kina unatakiwa uwe umefanyika ili kutokuwaingiza wasiohusika. Ila kwa sababu inasemekana kuwa ujangili unafanywa na watu wenye pesa wakishirikiana na wakubwa serikalini na ndani ya maliasili yenyewe, lazima waplan vibaya ili wananchi walalame na zoezi lisitishwe.
 
Kila operesheni huwa na madhala yake hususani Kama haikuratibiwa Vizuri kisayansi na miiko ya kazi kuzingatiwa kwani hata Operesheni Kimbunga nayo ilikumba waliokuwemo na wasio kuwemo lakini baada ya wanasiasa kuziingilia hizi Operesheni Sasa Majangiri na Wahamiaji wote wameludi Kama zamani na sasa Majangiri ni Kama hawana wa kuwazuia Tembo wanateketea kwa kasi ya Ajabu Majangiri wao wapo kazini wakati Wasira na Nyalando na akina Limbeli wanaendeleza Malumbano kule mbugani Tembo wanateketea : Ushauri wa Bure Tunaiomba Serikari ifanye Operesheni ingine lakini ifanyike Kisayansi zaidi yenye kuzingatia Haki za Binadamu kabla ya Operesheni watumwe wapelelezi wa Siri kwenye vijiji vyote vilivyo jirani na Hifadhi za wanyama ikibidi wachukuliwe wanavijiji waminifu watumike Kama informer wa kuleta Habari za kiintelijensia ili Operesheni ikifanyika iweze kuwatokomeza Majangiri kirahisi kinyume na hapo Malumbano hayatakwisha huku Tembo wanateketea kwa kasi

wanatuchezea akili maana majangili wanafahamika kwa majina wengine wako nao humohumo bungeni but they are untouchable chini ya utawala wa ccm.
 
Waziri ktk ofisi ya Rais mahusiano na uratibu na mbunge wa Bunda mh Stephen Masatu Wassira, amesema kuwa hakuna kiongozi yeyote mwenye akili timamu atakaepinga kuwa Opereshen Tokomeza haikuwa na madhara kwa Wananchi!

Kauli hii inakuja baada ya siku chache zilizopita Naibu waziri wa Mali asili na Utalii, mh Lazaro Nyalando kutoa kauli akidai kuwa ripoti ya kamati ya bunge iliyokua chini ya mbunge wa Kahama mh James Lembeli ilipotosha ukweli dhidi ya Opereshen Tokomeza!

Source: Radio Free Afrika tuzungumze Magazeti
Jamani nimekuwa nikisiliza kwa makini kauli za Mawaziri wetu, kwanza nilimfuatilia huyu Lazaro Nyalandu juu ya riporiti ya mh Lembeli kuwa ilipotoshwa na sasa Mh Stevin Wasira juu ya riport hiyo, hawa mawaziri wanatoka katika baraza moja au wanafanya kazi katika baraza moja la mawaziri?. Lakini nimejiuliza, kauli zao wanazitoa kama kauli ya waziri au mtu mwingine yeyote?.
 
Mawaziri wizara wote wendawazimu ni magaidi tu!
 
Kishajua rais amempiga chini ameamua kufanya fujo Fulani lakn maamuzi ya rais yatabaki kuwa vilevile
 
Hii wizara ya utalii inahitaji mtu makini na mzima kiumri na mwenye maamuzi magumu nasikia majangili wameuwa faru tena jamani tunakwenda wapi na Tanapa mnafanya nini kwani hao faru si wanalindwa kwa kupokezana?ingetakiwa sasa hivi tusikie askari aliyekuwa lindoni anahojiwa na mkuu wa faru pia,la sivyo faru na tembo kweli wataisha,na ningeshauri hao majangili waliouwa faru nao wauliwe.
 
nyalandu ana kampuni ya masuala ya utalii,sasa sijui kama inagusa UWINDAJI TEMBO KITALII
 
Sometimes we need to balance the story. Hii ishu inaweza kuwa na usahii pande zote mbili hasa tukizingatia ni kweli kuwa watu waliteswa na hii operation. On the other hand tutakubaliana kuwa Tembo wanateketezwa kwa kasi ya kutisha ukilinganisha na kuzaliana kwao. Huwezi jua pengine hawa Majangili wakubwa wanaowapa fedha vijana wakaue tembo wameifake hii ishu. But ukweli utakuja julikana.
 
------ hana tabu na vile ndio kabatizwa jina la Vasco Dagama hana mpango endelevu juu ya sector hii..... Bado tuna mwaka 1 na miezi 9 ya kuendelea kulia na huyu ------.
 
Hakuna mshindi,tembo wanauwawa na watu wasio na hatia waliteswa,labda mshindi ni vyombo vya habari vitapata habari za kuandika.
 
Waziri ktk ofisi ya Rais mahusiano na uratibu na mbunge wa Bunda mh Stephen Masatu Wassira, amesema kuwa hakuna kiongozi yeyote mwenye akili timamu atakaepinga kuwa Opereshen Tokomeza haikuwa na madhara kwa Wananchi!

Kauli hii inakuja baada ya siku chache zilizopita Naibu waziri wa Mali asili na Utalii, mh Lazaro Nyalando kutoa kauli akidai kuwa ripoti ya kamati ya bunge iliyokua chini ya mbunge wa Kahama mh James Lembeli ilipotosha ukweli dhidi ya Opereshen Tokomeza!

Source: Radio Free Afrika tuzungumze Magazeti

nnawasiwasi nyalandu yupo ile kambi nyingine
 
Back
Top Bottom