Wassira acha Hasira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira acha Hasira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Jul 7, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  [​IMG][TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wasira alishambulia Mwananchi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 07 July 2011 11:16 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg


  Leon Bahati, Dodoma

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wassira, amelishambulia gazeti hili akisema linaandika habari za uchochezi.

  Wassira alisema kwamba hivi karibuni gazeti hili lilitoa picha yake akiwa amelala bungeni,akijitetea kwamba alikuwa mgonjwa na alitumia dawa ambayo inasababisha usingizi.

  Hata hivyo, Wassira alikiri kuwa alikuwa amesinzia wakati Bunge likiwa linaendelea, lakini akakiita kitendo cha gazeti la Mwananchi kutoa picha wakati akionekana amelala kuwa ni “uchochezi”.

  "Juzi nilikuwa nimekaa pale alipokaa Mheshimiwa Samuel Sitta, lakini nilikuja hapa naumwa nikapitia Zahanati ile pale (zahanati ya Bunge), wakanipa dawa ya mafua, ile dawa ya mafua inaweza kukufanya ukawa drowse (ukalala), kesho nikakuta gazeti eti limenipiga picha kwamba nimesinzia.

  “Sasa ninawaambia wanipige picha niko live sasa. Wanafiki wakubwa hawa wanachochea wanataka kuleta mgogoro usiokuwa na msingi," alisema Wassira.

  Wassira aliyaeleza hayo juzi jioni wakati akifanya majumuisho ya bajeti ya matumizi ya Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu ambapo Bunge lilimuidhinishia Sh7.4bilioni kwa mwaka 2011/12.

  Kwa tafsiri ya Wassira, Mwananchi lilitoa picha hiyo kwa lengo la kuchochea huku akitaja baadhi ya habari ambazo ziliwahi kutolewa na gazeti hili ambazo kwa mtazamo wake anasema ni za kiuchochezi.

  Wassira alikwenda mbali zaidi akanukuu vichwa vya habari ambavyo alidai ni za uchochezi akisema: “ Kuna gazeti hapa linaitwa Mwananchi limeandika Chadema yaibwaga CCM kuhusu posho’ kulikuwa na mpira wa posho humu bungeni?,” .

  “…. mimi nilileta hapa hoja ya tume, ndani ya hoja mle ndani ya kitabu tumesema tutatazama upya posho mbalimbali kwa ajili ya kupunguza matumizi. Waziri wa Fedha amesema, sasa hoja ilikuwa iko wapi ambayo Chadema iliibwaga CCM? Uchochezi mtupu”.

  Wassira alikuwa akizungumzia pendekezo la kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na watumishi wengine wa umma ambalo liliibuliwa na wabunge wa Chadema, kiasi cha wabunge hao kuitwa “wanafiki”.

  Hata hivyo, baadaye Mbunge wa Bumbuli, January Makamba aliwagutua wabunge wenzake wa CCM ambao walikuwa wakipinga hoja hiyo kwa kuwaambia kwamba suala la kufutwa kwa posho lilikuwa sehemu ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni na Serikali.

  Kadhalika, Wassira alisema: "Juzi alikuwepo Mheshimiwa Edward Lowassa, akatoa maoni yake kama Mbunge tu wa Monduli, gazeti hili la Mwananchi linasema; “Vita ya Lowassa, Serikali ya JK sasa wazi’ Vita gani? Ipi? Hawa ni wachochezi na gazeti hili lina asili ya nje."

  " Na labda lingependa mambo ya nje yawe kama ya hapa, tunamwambia umechelewa hapa hayawezekani," alisema Wassira.

  Kauli ya Makinda
  Akizungumzia malalamiko ya Wassira, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema yako mengi ambayo vyombo vya habari vinakosea katika kuripoti.

  “Tunajitahidi kuwahimiza wajenge umoja wa Waandishi wa Habari za Bunge kwa sababu kwa kweli wanapotosha vitu vingi sana, zaidi ya hapo wanasema mimi naongoza Bunge, lakini mbumbu, sasa si unaona mambo yenyewe hayo, halafu ninapayuka payuka, sasa kazi yenyewe hii jamani,"alisema Makinda.

  Hata hivyo, Makinda aliweka bayana kwamba wabunge hushindana kwa hoja ndani ya Bunge, lakini akaeleza kufurahishwa kwake na wabunge hao kuanza kukomaa kwa kutokuwea maadui nje ya Bunge.
  "Juzi tulicheza dansi na Tundu Lissu, wakasema mnaona hawa, niko kwenye gazeti mojawapo, sasa mtu wangu mmoja alikuwa anawasikiliza akaniambia aliwasikia wanasema ‘unawaona hawa waongo kabisa hawa, kila siku anamwambia kaa chini, kaa chini, sasa unawaona wanachokifanya hapa,"alisema.

  Aliwaeleza wabunge kwamba wao hawana uadui wala ugomvi ila wanataka watu wawakilishe watu kwa sauti yao na nguvu zao zote, lakini wakitoka nje wanashikana mikono.

  "Mheshimiwa Freeman Mbowe, huyu ameshiriki kwenye msiba wa mama yangu, amefika mwenyewe physically (yeye mwenyewe) na wenzake wengi kule ndani kijijini, unajua pale kijijini wanasemaje?" alisema na kuongeza:

  "Hawa wanasema wapinzani, wapinzani kitu gani? Mbona amefika kwenye msiba? Hivi kweli kwenye msiba hatuwezi kwenda? Mimi nitakwenda kwenye msiba wa mtu yeyote, sasa wananchi watuelewe tuko hapa tumeshinda, tumechaguliwa tunakuja kuwakilisha, tutashindana kwa hoja hapa, nje tutakaa pamoja, tutakula pamoja na tutatembea pamoja."

  Mwananchi bungeni
  Wasira alilishambulia gazeti hili ikiwa ni karibu wiki mbili zimepita Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kamati ya Hesabu za Serikali, Augustine Mrema kulisifu Mwananchi kuwa ni gazeti linaloandika habari zake kwa umakini.

  Vilevile, mashambulizi ya Wassira yamekuja wakati wabunge kadhaa wamekuwa wakinukuu taarifa za gazeti hili ili kujenga hoja kuhusiana na kero mbalimbali zinazowapata wananchi.

  Mojawapo ni Msemaji Mkuu wa kambi ya Upinzani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma, Susan Lyimo aliliambia Bunge kuwa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), umekuwa ukijihusisha na vitendo vya kitapeli.

  Susan akionyesha kuwa taarifa hizo ni kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la Julai 2010 pamoja na mtandao wa YouTube, alifafanua kuwa wanachama hao walikuwa wameambiwa watoe Sh18,000 kama kiingilio na amana ya Sh250,000 kwa ahadi ya kukopeshwa Sh1 milioni ndani ya kipindi cha wiki moja

  Source: Mwananchi

  Hii habari inasikitisha,inakera na inaudhi.

  Kwako Mhe. Wassira Watanzania wanakuheshimu sana lakini pia wanakuvumilia sana kwa upuuzi na tabia zako unazozionyesha ukiwa kama Waziri. Mimi nakupa ushauri wa bure kabisa kuwa ACHA HASIRA we kibabu.

  Hivi gazeti kuchukua picha ya Mbunge tena Waziri anayelala Bungeni ni UCHOCHEZI kweeri muraa?????Labda kama maana halisi ya neno UCHOCHEZI itakuwa imepoteza maana yake. Yaani unataka uende mjengoni ukalale na kukoroma tu huku kila siku ukivuta hela zetu za walipa kodi 150,000/= bila aibu!

  Kama ulikuwa unaumwa kwanini uliingia ndani ya Ukumbi wa Bunge? Kwanini ueze dawa ambazo unajua zitaku-drowse???Kwanini hukuomba E.D.(Excuse for Duty) kwa siku hiyo? Hii inaonyesha jinsi vibabu vya CCM mlivyo na uchu na pesa! Uliona kuwa ukipewa ED hutaingia mjengoni na hivo ile posho ya 80,000+70.000/ =150,000/=ungeikosa!

  Je,ulitaka ufie mjengoni au uzimikie humo kwa sababu ya 150,000/=.?

  Mjomba yako Nyerere aling'atuka mapema kwasababu ya adha kama hizi. Wewe umeanza kuwa kiongozi ndani ya Serikali tangu enzi za huyo mjomba yako Nyerere miaka ya 1970s mpaka leo unang'ang'ania kuwa Mbunge uende Bungeni. Shame on you.

  Nakushauri uombe kujiuzulu Ubunge ili ukapata muda mzuri wa kupumzika na kulala nyumbani kwako na siyo Bungeni. Muda uliolitumikia Taifa unatosha sana. Lakini kama unang'ang'ania basi unapopigwa picha ukiwa umelala Bungeni uache hasira na kulaumu vyombo vya habari kuwa eti vinaleta uchochezi.

  Nawasilisha.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ma CCM ndiyo yalivyo haki na kweli zote kwao ni uchochezi .Huwajui kwani ? Mwache abwabwaje atakamatika tena kalala shortly .
   
 3. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hana lolote huyo alilala asiwalaghai watz kama watoto.
   
 4. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna haja gani kuudhuria Bungeni wakati unajua hauko katika hali ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za Bunge. Unaumwa pumzika wabunge waliomo Bugeni kwa ajili ya posho kama Wassira wanaonekana.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Cardinal rules kwa mwanasiasa yeyote:
  1. Dont fight media unless you are trully a saint!
  2. Dont fight media unless you are trully a saint!
  3. Dont fight media unless you are trully a saint!

  JUST DONT.
   
 6. kongomboli

  kongomboli Senior Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wassira hajui kusoma,mi ninalo hilo gazeti,picha inamuonesha amesinzia bt wamemuheshimu sana kuandika 'anatafakari' sasa hasira za nini wakati bos wao jk ashasema ktambo kuwa mawaziri wake hawalali bungeni bali wanatafakari!!
  JAMANI KIDGUMU CHAMA CHETU
   
 7. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Walizoea kufanya bunge kijiwe cha kupotezea muda, ila sasa media zinawaumbua!
   
 8. b

  bulunga JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi akilala tena bungeni atasema nini, usitukane mamba kabla ya kuvuka mto, nina uhakika atapigwa picha nyingine undenda ukimporomoka; halafu atasema alikuwa na Malaria
   
 9. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 80
  [​IMG]
   
 10. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  long live mwananchii!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kwa nini asingeenda kulala hotelini kwake?!!! uongo tu........
   
 12. m

  mtimbaru Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mh wassira aache kulishambulia gazeti la mwananchi, ni kweli alilala na kama alimeza dawa alipaswa kupumzika nasio kuingia bungeni.NAOMBA AACHE KUTISHA MAGAZETI. WASSIRA ALIOMBE RADHI GAZETI LA MWANANCHI
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  ''Nilikunywa PIRITON....nikaona nikienda kulala hotelini nitakosa posho'' alisema Wassira
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Shame on Government. Viongozi wote wa nchi mko hivyo. Wazungu wanaleta ndege zinabeba madini na kuondoka, nyie mnakalia ofisi and you don't deliver!!! Mpaka tufanye fujo make hamtoki madarakani tumesha wasoma kama gadafi vile!
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Posho amwchie nani.
   
 16. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alikuwa amevimbiwa posho
   
 17. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha! Yaani udhaifu wake anataka kuufanya ni ugomvi wa serikali na gazeti,nani mchochezi hapo? Yeye ndo anataka kugombanisha gazeti na serikali.ila duu,ile picha inachekesha sana,kila atakapoiona popote atamind sana! Loool!
   
 18. m

  mwl JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 180
  Magazeti ya leo yanamuumbua zaidi Wassira kwa kuonyesha kweli serikali ya JK inamkomalia EL, hata UHURU imeona hilo, sasa Wassira alikemee na hili.
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama ukipigwa picha umekaa vibaya ni uchochezi mwisho neno uchochezi litapoteza maana yake halisi.
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nashangaa wanaaa kujibizana na Wassira. Ni mtu mzuri sana akiwa nyumbani kwake au anapoongea na ndugu na marafiki, lakini akishatoka nje tu, ni monster asiyekuwa na akili yoyote ile.
   
Loading...