Wasomi wetu wengi ni mambumbumbu!

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Tanzania tumebarikiwa kuwa na wasomi si haba,lakini kwa ujumla hali yao ina sikitisha.Si wasomi hasa,ila ni watu ambao kwa kiingereza naweza kuwaita opportunists.Watu walio jiingiza kwenye usomi kwa nia ya kutafuta maisha,au kwa lugha ya mitaani kuganga njaa.Ni wasomi uchwara wasio kuwa na nia ya kweli ya kusaidia wenzao ambao hawakubahatika kupata nafasi kama yao.Wamekuwa rahisi kutumiwa na maadui wa Tanzania kwa sababu ya tamaa iliyokithiri.Kwa ujumla wamewatelekeza walala hoi wa Tanzania,huku wao wakila kuku kwa mrija kwa hela chafu za wanaoitwa kwa makosa wafadhili,na zile walizo wapora wale wale ambao walipashwa kuwasaidia.Aibu sana.

Wasomi hawa uchwara wamefumbwa macho wasijue kabisa kinachoendelea.Asilan wao kujisomea ili waweze kujua mawimbi haya makubwa yanayoikumba Tanzania yanatokana na nini imekuwa ni kero kwao.Wamezama kabisa katika tamaa na starehe zisizo na mwisho.Ukweli ulio fichika wameshindwa kabisa kuujua.Wameridhika kabisa na lugha za matapeli wa Ulaya kwamba kila wanacholeta matapeli hawa ni chema na hakina tatizo lolote.Hawana uwezo kabisa wa kujua upande wa pili wa shilingi.Wamelimbukia katika elimu feki waliyopewa madarasani wasiweze kuihoji kabisa, wasijue kwamba mengi waliyofundishwa yalikuwa indocrination ili waweze kuingizwa mkenge na kutawalika vizuri na kiurahisi.Nawapa pole sana!

Baya zaidi ni kwamba pamoja na kwamba wao wenyewe ni mbumbu wasiojua upande wa pili wa shilingi,wanashirikiana na kutumiwa na watesi wetu kuficha ukweli wa kile kinachoendelea,hata pale wanapo kijua.Inasikitisha kwamba watanzania wengi walalahoi,wamekwama kabisa na kutumbukia katika dimbwi la umaskini,kwa vile wale walio pashwa kuwasaidia wamewaangusha.

Tuzinduke basi wasomi na kutoka katika upumbavu huu uliotuzinga, ili tulitoe taifa letu letu katika dimbwi hili la umaskini uliokithiri.
 
Sio wote wako kama unavyodai, kwa mfano The late Prof S. Chachage. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
 
Wengi wamekulia kwenye system ambazo hazikuwa zinawapa nafasi kutoa kwa uhuru mawazo yao. Waliojaribu kufanya hivyo walionekana kama ni wapinzani. Hata hivyo, mambo yamebadilika. New generation ya wasomi inabidi kuonyesha kwa vitendo nini tunatakiwa kufanya.
 
Aisee! uko ryt mzee... Tukiendelea hivyi nchi tutawapa wababaishaji.....
 
Back
Top Bottom