Wasomi wahoji uzalendo wa Lissu

Wasomi wahoji uzalendo wa Lissu

BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana.

Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji.
Kwa hiyo huyo Bana na huyo Ndumbaro wanaona ni sawa watanzania kulipa mabikioni sababu tu ya MTU mmoja kujiamulia kuvunja sheria,wasomi gani njaaa hawa,nani hapo mzalendo wanafiki.
 
Wasomi gani hao? Its better for the group of sheep to be lead by one lion lather than the group of lion to be lead by sheep.

Sioni wasomi wakinena uhalisia bali naona wasomi wanafiki wakijipendekeza ili wapate pa kula.

Zaidi ya yote wasomi hao ni fisiem sasa kwa nini wasiseme hivyo?

Lissi is a typical african patriot nashangaa kusikia mabwenyenye eti wamemkosoa kwani hao wasomi hawakuwepo kipindi madudu haya yanafanyika?

Walikua wapi hata kushauli? Kweli elimu ya tanzania haiko relevant katika maendeleo ya nchi hii maana wanaitwa wasomi ni watu wa kujipendekeza waoga wanafiki na wachumia tumbo.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao si wasomi kwa maana halisi ya wasomi. Hao ni wajasilia masomo!
Bana anafahamika,ni kipaza sauti cha Lumumba.Semboja hana jipya.Kila analoongea ni "uharo" tupu.Wanategeshea uteuzi kama mkumbo. HOJA ya kupinga inapotoshwa.Kununuliwa ndege kwa mtindo wa kukiuka taratibu ndiyo kiini cha upinzani. Wasomi hao hawaoni au wanafumbia macho?

Watueleze mtindo huu wa maamuzi yanayokinzana n.a. sheria na taratibu ni sahihi au la? Wanaopiga kelele kupinga utamaduni huu kosa liko wapi?

Kama kuwa msomi ni kuunga mkono n.a. kutetea ukiukwaji dhahiri wa taratibu,sheria n.a. kanuni zilizowekwa kwa nia njema ya "ku-check and balance" mihimili ya dola,basi kuna tatizo kubwa kwa waitwao wasomi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi Tz kuna wasomi!?.naomba nijuzen jaman!,kwan sioni tofaut ya hawa ma prof sijui na ma doctor na wakulima kule kijijin.tena afadhal na wakukima wanajua ata vipindi vya kiangaz,masika na vuli!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usomi unapowekwa kapuni na kuendekeza siasa. Yaani kutumia tweet katika mawasiliano enzi hizi yeye anaona sio njia sahihi, eti watu watajua, watu gani anaowaongelea kama sio ambao hela yao ya kodi iko rehani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanatafta nyadhifa kwa uleeeeee uteuzi kwa mh.rais ktk nyanja za kisiasa.
 
Back
Top Bottom