Wasomi wahoji uzalendo wa Lissu

Wasomi wahoji uzalendo wa Lissu

Mbona mm ni msomi sija hoji? Na nina imani na T. Lissu.

Mtu kasoma Curriculum Dvt , Psychology in Education za akina K. Mkumbo nae umuite msomi ktk mambo ya Kisheria au ki uchumi? Utakuwa chizi sana!!!

JPM KAMATA WEZI
 
BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana.

Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji.
Swali, Uzalendo ni nini?
Nataka kujua maana ya uzalendo ili niendelee kutoka kwa wadau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtu msomi ambaye shule imekaa vizur kichwan hawez kuongea shit namna hii, uyo Bana hana usomi wowote ni upuuzi mtupu alioongea! sisi ni watanzania ivyo tuna haki ya kujua mustakbal wa nchi yetu kwaiyo uyo Bana alitaka sisi watanzania tusijue kama tunadaiwa? waache upuuzi wao uko na ndio hao hao wanaoitwa ma profesa ndio wametufikisha hapa! maprofesa vilaza kama hao ndio walio sain mikataba mibovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani

UVCCM
MSUKUMA
MILINGA
MAJI MAREFU

Silinde ndio unawaita wasomi?

Wewe ni zero brain,Hujielewi,Bado yule fa fa fa!
 
Vile vichwa vya treni pale Bandarini vimepata mwenyewebama ishakuwa "sadakalawe"
 
Hili neno uzalendo ndio limekua sehemu ya kujifichia watawala wanapofanya makosa. MTU alie katisha mkataba bila ya kuangalia madhara ambayo yamesababisha hasara hii na kukaa kimya. anaitwa mzalendo na yule alie wambia watanzania kua kuna mtu katusababishia hasara anaitwa sio mzalendo. Kama wasomi wenye ndio wako hivyo bora ya Mimi wa dalasa la tano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wana matatizo ya akili na ndiyo maana hawana uchungu na haya mauzauza yote yanayofanya na ccm kiasi kwamba kuna watu hadi leo bado wana mapenzi na ccm.

Na wengine ndiyo wameshindwa kutofautisha kati ya Tanzania na ccm,na ndiyo maana wao haya mauzauza ya serikali kwao hawaoni kama ni athari kwa nchi(Tanzania) bali wao kila yanapoelezwa haya mambo hufurahia kwa kuona wamekomolewa ccm.

Na ndiyo maana mtu anaomba Tanzania inyimwe misaada ila bado watanzania huona ni sawa tu kwa kuamini ccm ndiyo itakomoka.

Ajabu miaka yote uchafu wa serikali unaelezwa hadi wachafuzi wengine hukosa fursa ccm na kuamia kwenda upinzani (kutimiza ndoto zao binafsi) lakini bado ccm ipo madarakani.

Watanzania wanachukizwa na ccm kuliko hata na mabaya yanayofanywa na ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bac Mzee Magu, ndo anapenda kuitumia hii misomi, ndo kaijaza kwenye mazungumzo na Acacia. Wazungu wanaweka watu wao wa kawaida na wanashinda.
 
BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana.

Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji.
Huwezi kuacha kuandika kitu kama hiki lwakua ndio kinakuingizia mkate wako wa siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wajinga, wapumbavu,malofa ndio wanaweza kumsikiliza Bana. Na kama wasomi wenyew ndo hao haki ya Mungu nchi itakuw kipofu milele na milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MaPropesa wanavizia teuzi i za MunguMtu hasa Bana ambaye Hii ni awamu tatu anajipendekeza bila mafanikio
 
Mi sizani km hao maprofesa kama wameongea kweli hayo.Na kama wamenena hayo wachunguzwe vyeti vyao
Waelewe kwamba mwenendo uko hivi Lissu amekuwa toka mwanzo hatua za kijinga jinga zimazochukuliwa na serikali si sahihi lkn watu na viongozi wao hawafikilii wamamuona punguani sasa wameanza kufanya mambo kimya kimya wakati nyuma walijifanya wawazi wanafanya mambo hadhalani na mbwembwe sasa kwanini yanapoanza kuripuka hawasemi. Lissu lazima awaonyeshe ye alikuwa sahihi kuwa approach ya serikali haikuwa sahihi inatupeleka gizani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania tuna asilimia kubwa yawasomi DAHAIFU na WAOGA wasiofikiri vema. Wanaojiita wazalendo huku uzalendo ukiwa hauonekani kabisa.

Kwa sasa tuna wasomi uchwara wanaohoji tamko Tundu Lissu kuwa so ya kizalendo. Wasomi hao uchwara wanafikiri uzalendo unapimwa kwa kusema uongo na kuficha ukweli.

Tundu Lissu kasema ukweli, lakini wasomi uchwara mithili ya akina Dr Bana wanataka Tundu Lissu aseme uwongo na kufunika ukweli.

Kwa wasomi hao uchwara kwao kusema uwongo ni uzalendo na kusema ukweli ni ubaya na kutokuwa mzalendo.

Wasomi wa aina hii ni wa kuogopwa kama ukoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom