Tanzania kunaWahandisi wahandisi wachache sana. Hawazidi elfu 8. Kama tuki-assume Watanzania wapo mil 46 utaona kuwa katika kila watanzania 5875 kuna Mhandisi mmoja! Ukitilia maanani kuwa kwa sasa kuna miradi mingi ya kihandisi ni dhahiri utaona hilo pengo na ndio chanzo cha hao wahandisi unaowaona kutoka nje! Nchi kama Japani uwiano ni mhandisi mmoja kwa Wajapani kama 200. Na tofauti ya maendeleo yetu pia inaanzia hapo.
Sijaridhishwa na hiyo sababu. Hiyo namba ya wahandisi inatosha kabisa kuleta maendeleo yanayoweza kuonekana nchini. Mbona Madaktari nao ni wachache lakini bado tunaona kazi zao (kupasua kichwa badala ya miguu) na hata Wanasheria nao ni wachache, na tunaona kazi fulani zikifanyika (kesi ya mgombea binafsi, zombe, kesi za EPA, na mikataba ya kimataifa, n.k). Sasa sisi wahandisi wetu wanaishia wapi? TANESCO (electrical engineers ) na TTCL (telecom/electronics engineers)?
Ukienda nchi za watu unaangalia barabara, flyovers, overpass, subways, viwanja vya ndege, Majumba ya kuishi na ya starehe, madaraja, vyote vinakuwa bab-kubwa na ukiona unaridhika kabisa kuwa Wahandisi wao wanafanya kazi. Sasa hapa kwetu mhandisi anajenga culverts kwenye barabara za vumbi, tena kwenye barabara ya kutoka mkomazi kwenda Ndungu?! Halafu zinabomoka muda si mrefu.
Surely there is something wrong.
Kwanini sisi tusiweze? Wahandisi walisoma ulaya wapo, waliofaulu vizuri pale UDSM na kusajiliwa na ERB wapo. Nondo zinatoka nchini, Cement inatoka nchini, mchanga, mawe n.k vyote vinatoka hapa hapa nchini, kwanini hatuna barabara na madaraja mazuri? Hata kale ka-kivuko ka manzese walijenga Wajapani... Hapa tunahitaji kuchunguza zaidi kwa kweli, tatizo liko wapi? Na sio bongo tu, naona hata kenya, kumbe yale ma-flyovers wanajenga wahandisi wa kichina? Au ndio kusema tuna shule ila hatuna tekelinalokujia? Sasa mbona inafahamika kuwa vyuo vyetu vinafundisha sayansi na tekelinalokujia?