Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Sidhani kama kuna Raisi wa TZ ambaye amewahusisha wasomi nchi hii kwenye ngazi za Uongozi kama Raisi wa V Magufuli, hivyo yale manung'uniko niliyokuwa nayasikia siku nyingi sana kuhusu kutokuthaminiwa kwa wasomi na Seriklai yetu sasa nafikiri yamepatiwa ufumbuzi kwani kuanzia Mawaziri mpaka Makatibu Wakuu sehemu kubwa ni wasomi tena waliotolewa fresh kabisa kwenye taaluma zao na kukabidhiwa Wizara zinazohusu taaluma zao, sasa wamepewa ukumbi wa kutuonyesha ni nini wanaweza kazi kwao, Wamarekani wana msemo kwamba ,,be careful with what you asked, for because you might just get it" hakuna visingizio tena!
Last edited: