Mkuu, hapa anazungumzia taa, na amini itakua ya kawaida inayotumia single phase. Voltage hapa tuna zungumzia 230v. Sioni possibility ya ku form capacitor au inductor kwa hiyo voltage kidogo. Ingekua 11 kv,33kv ingekua sawa.kwa kesi ya hii hakutakua na umeme utaotumika. No load.for current to flow there must be a load. Na kwa kesi hiyo load ni taa.hakuna taa hakuna umeme
Kwa bahati mbaya umeme utakwenda hata kama bulb haipo; najua watu wengi hawataamini jibu hili ila ndivyo ilivyo. Umeme tunaotumia majumbani na viwandani duniani kote ni wa aina ya AC, ambayo kwa Tanzania inakuwa na frequency yenye mizunguko hamsini kwa sekunde; umeme huu hupita mahali popte iwapo utaweka mradi tu uwe na nyaye mbili kwa karibu zinazokamilisha mzunguko hata kama hazikuuungana, yaani bulb haipo. Nyaya hizo hufanya kitu kiachoitwa capacitance ambayo hukamilisha circuit ya AC. Uzuri ni kuwa umeme huo huenda kwa kasi ndogo ambayo haitaweza kuathiri sana bili yako ya mwezi, ila ukiuacha kwa muda mrefu sana kama mwaka mzima utakuta bili nayo imepanda kwa kiasi fulani.