Wasomi wa mambo ya umeme naombeni mnisaidie

Baba Wille

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
548
548
WASOMI WA MAMBO YA UMEME NAOMBENI MNISAIDIE:

Ninataka kuweka umeme wa solar nyumbani kijijini, fundi wangu amenishauri kuwa niweke Solar pannel mbili za watt 100 kila moja jumla ziwe watt 200 na betri za watt 100@. Lengo langu ni kutumia kwa ajili ya taa km 10, redio, tv, king'amuzi na friji. Je panel na betri hizo zitatosha?

Nb: umeme utakuwa converted into AC.

NAWASILISHA!
 
Hizi ni general tips.
Vipo vitu vitatu vya kuangalia/kukokotoa

1. Kiasi gani cha nishati betri zako zinaweza kuhifadhi
2. Kiasi gani cha nishati vifaa vyako vya umeme vitatumia nishati hiyo kwa muda gani.
3. Kiasi gani cha nishati solar panel zako zinaweza zalisha umeme kwa muda husika.

Tukianza na namba 1, ni muhimu kujua uwezo wa betri kuhifadhi nishati kisha unaweza kuchagua solar panel itakayofaa kujaza betri zako kulingana na utumizi wako.

1. Kiasi gani cha nishati betri yako inaweza kuhifadhi?
Ujazo wa nishati (capacity) wa/ya betri hupimwa kwa AH (Amp hours) mfano 19AH utahitaji ku convert kipimo cha AH kwenda Watt (W) kwa njia rahisi tu ya kuzidisha na rated voltage ya battery, (mf 12V).

Hesabu rahisi
Y(battery capacity in AH) X (battery voltage)V = Q (Power available in Watt hours)

Mfano;
Kwa battery ya 25AH, 12V
Figure in watt hours =25AH X 12V=300WH

Hiyo figure in WH ina maana hii
Betri lako linaweza deliver 300W ndani ya saa 1
!! 150W ndani ya saa 2
!! 20W ndani ya saa 15
!! 5W ndani ya saa 60

kwa hiyo kama una kifaa chenye rating husika utafanya mgawanyisho kujua ni masaa mangapi unaweza tumia betri likiwa full.
Ntaendelea.................................

******Muendelezo*******
Mtoa mada hizi hesabu ni rahisi sana ni swala la kuzidisha na kugawanya tu hakuna usichoweza kukokotoa hapo, labda hizo terms kama AH, WH ndio zimekuchanganya, nikutoe tu wasiwasi, hizo ndizo hutumika kutambulisha uwezo wa battery unapoenda dukani kununua, ni kama unavyoenda dukani na kuomba uletewe mafuta litre 10.

Sehemu hujaelewa uliza na tutaeleweshana taratibu.
Pia hapa nimejaribu kuelezea upande wa DC tu, kwenda AC ntaweka kipande chake, lengo ni kupata mwanga kotekote, ukijua kukokotoa awali na mwisho utaweza pia.

Niendelee kwenye battery, baada ya kujua namna ya kukokotoa ni rahisi kujua battery ngapi zitatosha kuendesha vifaa vyako vyote kulingana na muda wa matumizi.

Pia battery zipo aina kadhaa ni vizuri kuchagua zenye ubora, zisizosumbufu.

Mfano
1. Lead acid battery's zitakupa 50% ya kiwango chake kilichoidhinishwa mfano imeandikwa itakupa 20AH tegemea kupata 10AH.(Rated power)

2. Li-ion battery's zitakupa 80% ya kiwango kilichoidhinishwa (Rated power). kwa hiyo kama imeandikwa 20AH hapa tunategemea kupata 16AH.

Hizo tajwa hapo juu ni efficiency za battery ama kwa lugha ya kiswahili ufanisi, sababu za kutofautiana ni teknolojia, materials na manufcturing processes na bei pia huwa tofauti.
NB:Yenye efficiency kubwa ndio nzuri.

Kitu kingine cha kufahamu, betri za gari hazifai kwa matumizi ya solar power systems, kwasababu uundwaji wake umelenga kutoa power nyingi haraka, na haiwezi kuvumilia discharge & Recharge ukilinganisha na betri maalum za solar systems.

2. Kiasi gani cha nishati vifaa vyako vya umeme vitatumia nishati hiyo kwa muda husika.

Utumiaji wa umeme katika vifaa hupimwa kwa Wattage (W) na taarifa za kifaa husika hubandikwa kwa kila kifaa, bila shaka umeshakutana na vitu kama 20W, 50W kwenye vifaa mbalimbali iwe bulb, TV, deki, fridge, nk.

Kukokotoa kiwango cha nishati utakachotumia kwa muda fulani ni rahisi, utachukua kiwango cha rated power (watt) utazidisha na muda utakaotumia.
Mfano,
Unayo TV ya 40W unataka kutizama kwa muda wa saa 3, hesabu yake itakuwa;
40W X 3H = 120WH

Rudia zoezi hapo juu kukokotoa vifaa vyote ulivyonavyo na muda gani kila kifaa kitatumika kwa siku.

Mfano;
Taa 5W X 5 hours per day =25WH
TV 40W X 4 hours per day =160WH
Radio 8W X 4hours per day =32WH
................
Endelea kwa vifaa vyote kisha mwisho jumlisha WH zote kwa case yetu hapa tuna 25+160+32=217WH

Baada kupata hizo jumla basi utakua umejua kwa siku matumizi yako ni 217WH kwa vifaa vyote ulivyofanyaia ukokotozi.

Muhimu: kwa taa ni vizuri kutumia LED's kwa sababu zinatumia kiwango kidogo cha nishati na efficiency kubwa. tunaposema efficiency kubwa kunamaana ya kwamba unatumia kiwango kidogo na umeme kupata mwanga mkubwa kwa muda wa kutosha.

Kitu kingine muhimu, ungetumia vifaa vyote vya DC ungepata efficiency kubwa tofauti na kufanya conversion kutoka DC kwenda AC kwa sababu kuna upotevu wa nishati katika process ya DC to AC.

Sehemu ya mwisho ni chaguo la panel kwa ajili ya system yako, uzalishaji wa nishati kwa solar panels pia hupimwa kwa Watts (W) kwa hiyo kupata kiwango cha uzalishwaji wa umeme jua, utachukua rating za solar panel unayotaka kununua/uliyonunua kisha utazidisha na masaa ambayo panel yako itamulikwa na jua kwa siku.

Kiuhalisia sio njia sahihi sana kupata kiwango halisi, kwasababu ya hali ya hewa jua, kutoweka, au kipindi cha mvua na sababu kadha wa kadha zinazopunguza umulikwaji wa panel.

Hesabu
panel ya 50W ikiwa exposed kwenye jua 6hrs
50W X 6H=300WH
300WH zitakwenda kuchaji betri zako.

Kitu cha kufahamu, si zote 300WH zitakwenda kwenye battery, kuna losses kwenye conductor (wire), regulator, na battery lenyewe. kutambua kiwango cha losses mpaka ufanye vipimo vya kutosha, ila mfumo ukifungwa vizuri kwa vifaa vizuri, losses hupungua.

Losses kama hujazielewa ni kwamba tunatarajia panel izalishe 300WH kwenda kuchajisha betri letu lakini, kiwango kinachopokelewa kwenye betri labda ni 210WH kwa hiyo hapo kuna upotevu wa 90WH.

Madhara ya upotevu wa 90WH ni kama haya, kama kwa 300WH betri lingehitajika kuchajiwa kwa masaa 5, kukiwa na upungufu litachijiwa kwa muda mrefu zaidi tofauti na hesabu ulizopiga kwenye makaratasi, mfano litachajiwa full kwa saa 8 badala ya saa 5 kutokana na losses.

Losses haziwezi ondolewa completeley ila tu zaweza kupunguzwa na ziwe ndogo.

Kwenye vitengo vya umeme mkubwa na mdogo kila siku wanapambana kupunguza losses kuanzia kwenye High transmission lines mpaka kwenye simu yako.

Hope this helps.
 
Kiasi gani cha nishati betri yako inaweza kuhifadhi?

Vizuri, umemuelezea katika layman language. Hope itamsaidia, sina cha kujazia katika hili.
 
WASOMI WA MAMBO YA UMEME NAOMBENI MNISAIDIE:

Ninataka kuweka umeme wa solar nyumbani kijijini, fundi wangu amenishauri kuwa niweke Solar pannel mbili za watt 100 kila moja jumla ziwe watt 200 na betri za watt 100@. Lengo langu ni kutumia kwa ajili ya taa km 10, redio, tv, king'amuzi na friji. Je panel na betri hizo zitatosha?

Nb: umeme utakuwa converted into AC.

NAWASILISHA!
kwakifupi utatumia umeme wa betri kazi ya solar ni kucharge hizo betri wakati wa mchana kwakutumia mwanga wa jua
 
WASOMI WA MAMBO YA UMEME NAOMBENI MNISAIDIE:

Ninataka kuweka umeme wa solar nyumbani kijijini, fundi wangu amenishauri kuwa niweke Solar pannel mbili za watt 100 kila moja jumla ziwe watt 200 na betri za watt 100@. Lengo langu ni kutumia kwa ajili ya taa km 10, redio, tv, king'amuzi na friji. Je panel na betri hizo zitatosha?

Nb: umeme utakuwa converted into AC.

NAWASILISHA!

fundi wako yupo sahihi kwa kiasi fulani ila hapo utahitaji kuongeza battery kwa sababu usiku battery inabeba mzigo wote kwa sababu hakuna mwanga wa jua.

unataka kutumia taa 10. Kwa kawaida unapotumia solar hautumii taa za umeme wa kawaida, hapo fundi wako amemaanisha taa za solar ambazo ni za 12 DC LED na zinatumia WATTS kidogo. hivyo kila taa moja inaweza kuwa na 5Watts.

KUHUSU REDIO (kama utatumia redio kubwa isiyo ya solar)
>>Hapa ndio kutakuwa na Inverter DC to AC ili upate umeme Kama wa Tanesco 220v AC

KUHUSU TV, Zipo TV za solar zinatumia 12V DC
>>Kama utatumia TV za kawaida ndio utalazimika kutumia Umeme wa inverter 220V AC

KUHUSU KING'AMUZI
>>Vipo Ving'amuzi vya 12V DC kama vile ZUKU , ukitumia ving'amuzi vingine ndipo utalazimika kutumia umeme wa inverter 220V AC

KUHUSU FRIDGE (JOKOFU)
>>Zipo za solar (ila bei zipo juu kwa friji dogo). Kama utatumia friji la kawaida , ndio utalazimika kutumia umeme wa sola. Friji ndio itakugharimu sana hapo kwa sababu linatakiwa kuwa ON 24hrs, na kawaida ya Friji kila linapowaka linachukua umeme karibu mara 2 ya umeme wake wa kawaida.

Mwambie fundi wako afanye marekebisho hapo kwenye battery ili uweze kuwasha friji usiku na huku ukitmia TV na vitu vingine.
 
Hizi ni general tips.
Vipo vitu vitatu vya kuangalia/kukokotoa

1. Kiasi gani cha nishati betri zako zinaweza kuhifadhi
2. Kiasi gani cha nishati vifaa vyako vya umeme vitatumia nishati hiyo kwa muda gani.
3. Kiasi gani cha nishati solar panel zako zinaweza zalisha umeme kwa muda husika.

Tukianza na namba 1, ni muhimu kujua uwezo wa betri kuhifadhi nishati kisha unaweza kuchagua solar panel itakayofaa kujaza betri zako kulingana na utumizi wako.

Kiasi gani cha nishati betri yako inaweza kuhifadhi?
Ujazo wa nishati (capacity) wa/ya betri hupimwa kwa AH (Amp hours) mfano 19AH utahitaji ku convert kipimo cha AH kwenda Watt (W) kwa njia rahisi tu ya kuzidisha na rated voltage ya battery, (mf 12V).

Hesabu rahisi
Y(battery capacity in AH) X (battery voltage)V = Q (Power available in Watt hours)

Mfano;
Kwa battery ya 25AH, 12V
Figure in watt hours =25AH X 12V=300WH

Hiyo figure in WH ina maana hii
Betri lako linaweza deliver 300W ndani ya saa 1
!! 150W ndani ya saa 2
!! 20W ndani ya saa 15
!! 5W ndani ya saa 60

kwa hiyo kama una kifaa chenye rating husika utafanya mgawanyisho kujua ni masaa mangapi unaweza tumia betri likiwa full.
Ntaendelea.................................
Mkuu nashukuru kwa maelezo ila yamekaa kitaalamu mno nami physics niliishia Form 4 mwaka 2004.. please jaribu kutumia lugha ya kilayman nielewe.. asante
 
Mkuu nashukuru sana. Umenifungua kitu, hasahasa nimefurahis ushauri wa kuongeza betri, lakini je unashauri niongeze betri ya ukubwa gani? Je solar sina haja ya kuongeza?
 
Wille, jambo la kwanza kabisa nunua daftari na kalamu halafu taratibu NA KWA UMAKINI anza kufuatia maelezo ya AH120. huyu anaongea juu ya kitu anachokifahamu na anatumia lugha rahisi.

Utapata msaada zaidi ukifanya yafuatayo.
##. utawasha taa 10 za watt 5 kwa muda wa masaa mangapi kwa siku?

##. Radio itakuwa na watt ngapi? Na utasikiliza kwa saa ngapi kwa siku? (Unaweza kukadiria)

##. Fridge ya watt ngapi?

##. Tv hivyohivyo, ila tu usinunue tv ya chogo (CRT) nunua flati na jaribu kupata yenye option ya umeme wa Dc. Zipo nyingi.

##. Angalia pia kama eneo unaloishi kiasi cha jua linalopatikana kwa siku. Mfano masaa nane au kumi?

Majibu ya hapo juu yatasaidia, kukukadiria ununue kioo cha sola cha ukubwa gani na battery ya ukubwa gani pia.
 
Mkuu nashukuru kwa maelezo ila yamekaa kitaalamu mno nami physics niliishia Form 4 mwaka 2004.. please jaribu kutumia lugha ya kilayman nielewe.. asante
Nimeendeleza pitia tena kwenye shida tutaelekezana.
 
Mi mkazi was dar ila ni mwenyeji wa mkoani
Nimefurah sana kusikia kuna TV za DC pamoja na redio kwa mkoani fridge not a big deal,

Ila naomba kuuliza swali LA general Mimi piavsio mjuzi , nikitaka sola ya kuwasha taa sita ,redio, TV, charge sm, wastani wa bei yake in kiasi gani
 
Wille, jambo la kwanza kabisa nunua daftari na kalamu halafu taratibu NA KWA UMAKINI anza kufuatia maelezo ya AH120. huyu anaongea juu ya kitu anachokifahamu na anatumia lugha rahisi.

Utapata msaada zaidi ukifanya yafuatayo.
##. utawasha taa 10 za watt 5 kwa muda wa masaa mangapi kwa siku?

##. Radio itakuwa na watt ngapi? Na utasikiliza kwa saa ngapi kwa siku? (Unaweza kukadiria)

##. Fridge ya watt ngapi?

##. Tv hivyohivyo, ila tu usinunue tv ya chogo (CRT) nunua flati na jaribu kupata yenye option ya umeme wa Dc. Zipo nyingi.

##. Angalia pia kama eneo unaloishi kiasi cha jua linalopatikana kwa siku. Mfano masaa nane au kumi?

Majibu ya hapo juu yatasaidia, kukukadiria ununue kioo cha sola cha ukubwa gani na battery ya ukubwa gani pia.
Sawa mkuu, asante kapunika
 
Hizi ni general tips.
Vipo vitu vitatu vya kuangalia/kukokotoa

1. Kiasi gani cha nishati betri zako zinaweza kuhifadhi
2. Kiasi gani cha nishati vifaa vyako vya umeme vitatumia nishati hiyo kwa muda gani.
3. Kiasi gani cha nishati solar panel zako zinaweza zalisha umeme kwa muda husika.

Tukianza na namba 1, ni muhimu kujua uwezo wa betri kuhifadhi nishati kisha unaweza kuchagua solar panel itakayofaa kujaza betri zako kulingana na utumizi wako.

1. Kiasi gani cha nishati betri yako inaweza kuhifadhi?
Ujazo wa nishati (capacity) wa/ya betri hupimwa kwa AH (Amp hours) mfano 19AH utahitaji ku convert kipimo cha AH kwenda Watt (W) kwa njia rahisi tu ya kuzidisha na rated voltage ya battery, (mf 12V).

Hesabu rahisi
Y(battery capacity in AH) X (battery voltage)V = Q (Power available in Watt hours)

Mfano;
Kwa battery ya 25AH, 12V
Figure in watt hours =25AH X 12V=300WH

Hiyo figure in WH ina maana hii
Betri lako linaweza deliver 300W ndani ya saa 1
!! 150W ndani ya saa 2
!! 20W ndani ya saa 15
!! 5W ndani ya saa 60

kwa hiyo kama una kifaa chenye rating husika utafanya mgawanyisho kujua ni masaa mangapi unaweza tumia betri likiwa full.
Ntaendelea.................................

******Muendelezo*******
Mtoa mada hizi hesabu ni rahisi sana ni swala la kuzidisha na kugawanya tu hakuna usichoweza kukokotoa hapo, labda hizo terms kama AH, WH ndio zimekuchanganya, nikutoe tu wasiwasi, hizo ndizo hutumika kutambulisha uwezo wa battery unapoenda dukani kununua, ni kama unavyoenda dukani na kuomba uletewe mafuta litre 10.

Sehemu hujaelewa uliza na tutaeleweshana taratibu.
Pia hapa nimejaribu kuelezea upande wa DC tu, kwenda AC ntaweka kipande chake, lengo ni kupata mwanga kotekote, ukijua kukokotoa awali na mwisho utaweza pia.

Niendelee kwenye battery, baada ya kujua namna ya kukokotoa ni rahisi kujua battery ngapi zitatosha kuendesha vifaa vyako vyote kulingana na muda wa matumizi.

Pia battery zipo aina kadhaa ni vizuri kuchagua zenye ubora, zisizosumbufu.

Mfano
1. Lead acid battery's zitakupa 50% ya kiwango chake kilichoidhinishwa mfano imeandikwa itakupa 20AH tegemea kupata 10AH.(Rated power)

2. Li-ion battery's zitakupa 80% ya kiwango kilichoidhinishwa (Rated power). kwa hiyo kama imeandikwa 20AH hapa tunategemea kupata 16AH.

Hizo tajwa hapo juu ni efficiency za battery ama kwa lugha ya kiswahili ufanisi, sababu za kutofautiana ni teknolojia, materials na manufcturing processes na bei pia huwa tofauti.
NB:Yenye efficiency kubwa ndio nzuri.

Kitu kingine cha kufahamu, betri za gari hazifai kwa matumizi ya solar power systems, kwasababu uundwaji wake umelenga kutoa power nyingi haraka, na haiwezi kuvumilia discharge & Recharge ukilinganisha na betri maalum za solar systems.

2. Kiasi gani cha nishati vifaa vyako vya umeme vitatumia nishati hiyo kwa muda husika.

Utumiaji wa umeme katika vifaa hupimwa kwa Wattage (W) na taarifa za kifaa husika hubandikwa kwa kila kifaa, bila shaka umeshakutana na vitu kama 20W, 50W kwenye vifaa mbalimbali iwe bulb, TV, deki, fridge, nk.

Kukokotoa kiwango cha nishati utakachotumia kwa muda fulani ni rahisi, utachukua kiwango cha rated power (watt) utazidisha na muda utakaotumia.
Mfano,
Unayo TV ya 40W unataka kutizama kwa muda wa saa 3, hesabu yake itakuwa;
40W X 3H = 120WH

Rudia zoezi hapo juu kukokotoa vifaa vyote ulivyonavyo na muda gani kila kifaa kitatumika kwa siku.

Mfano;
Taa 5W X 5 hours per day =25WH
TV 40W X 4 hours per day =160WH
Radio 8W X 4hours per day =32WH
................
Endelea kwa vifaa vyote kisha mwisho jumlisha WH zote kwa case yetu hapa tuna 25+160+32=217WH

Baada kupata hizo jumla basi utakua umejua kwa siku matumizi yako ni 217WH kwa vifaa vyote ulivyofanyaia ukokotozi.

Muhimu: kwa taa ni vizuri kutumia LED's kwa sababu zinatumia kiwango kidogo cha nishati na efficiency kubwa. tunaposema efficiency kubwa kunamaana ya kwamba unatumia kiwango kidogo na umeme kupata mwanga mkubwa kwa muda wa kutosha.

Kitu kingine muhimu, ungetumia vifaa vyote vya DC ungepata efficiency kubwa tofauti na kufanya conversion kutoka DC kwenda AC kwa sababu kuna upotevu wa nishati katika process ya DC to AC.

3. Kiasi gani cha nishati solar panel zako zinaweza zalisha umeme kwa muda husika.
Sehemu ya mwisho ni chaguo la panel kwa ajili ya system yako, uzalishaji wa nishati kwa solar panels pia hupimwa kwa Watts (W) kwa hiyo kupata kiwango cha uzalishwaji wa umeme jua, utachukua rating za solar panel unayotaka kununua/uliyonunua kisha utazidisha na masaa ambayo panel yako itamulikwa na jua kwa siku.

Kiuhalisia sio njia sahihi sana kupata kiwango halisi, kwasababu ya hali ya hewa jua, kutoweka, au kipindi cha mvua na sababu kadha wa kadha zinazopunguza umulikwaji wa panel.

Hesabu
panel ya 50W ikiwa exposed kwenye jua 6hrs
50W X 6H=300WH
300WH zitakwenda kuchaji betri zako.

Kitu cha kufahamu, si zote 300WH zitakwenda kwenye battery, kuna losses kwenye conductor (wire), regulator, na battery lenyewe. kutambua kiwango cha losses mpaka ufanye vipimo vya kutosha, ila mfumo ukifungwa vizuri kwa vifaa vizuri, losses hupungua.

Losses kama hujazielewa ni kwamba tunatarajia panel izalishe 300WH kwenda kuchajisha betri letu lakini, kiwango kinachopokelewa kwenye betri labda ni 210WH kwa hiyo hapo kuna upotevu wa 90WH.

Madhara ya upotevu wa 90WH ni kama haya, kama kwa 300WH betri lingehitajika kuchajiwa kwa masaa 5, kukiwa na upungufu litachijiwa kwa muda mrefu zaidi tofauti na hesabu ulizopiga kwenye makaratasi, mfano litachajiwa full kwa saa 8 badala ya saa 5 kutokana na losses.

Losses haziwezi ondolewa completeley ila tu zaweza kupunguzwa na ziwe ndogo.

Kwenye vitengo vya umeme mkubwa na mdogo kila siku wanapambana kupunguza losses kuanzia kwenye High transmission lines mpaka kwenye simu yako.

Hope this helps.
Kaka upo vizuri. Kesho nitakokotoa kimoja baada ya kingine. Thank you alot. Km hutojali nitapenda npate namba yako ya simu pia. Actually mi nakaa mjini sasa nmejengea kijijini nyumba ya kufikia nkaona nisiende kichwa kichwa coz mafundi wenyewe hawa sio wataalamu sana ktk ukokotozi, wanakadilia zaidi kiuzoefu. Thanks once again comrade!
 
Mwalimu mzuri
 
Back
Top Bottom