Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kujiimarisha na kujiongezea nguvu baada ya kuwashawishi wasomi 300 kanda ya mashariki kujiunga na chama hicho na kupokelewa kwa hadhi kubwa katika event iliyofanyika bagamoyo jana ambapo mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM wilaya ya bagamoyo Ndugu Ridhwan Jakaya Kikwete alikuwa ni mgeni rasmi katika tukio hilo lililoratibiwa na katibu wa wilaya (mkoa maalum wa vyuo vikuu) ndugu Ally Salum Hapi.
wasomi hao kutoka vyuo mbalimbali kanda ya mashariki mkoa wa pwani na dar es salaam wamechukua uamuz huo baada ya kukiri kuwa chama cha siasa kilicho na misingi ya haki na uadilifu ni CCM pekee.
baada ya tukio hilo wasomi hao wameahidi kuwa wajumbe wa Chama katika vyuo vyao kuwafikishia ujumbe wanafunzi wenzao ambao bado hawajafanya uamuz huo makini. Wamesema wanafunzi wengi kwa kutopata ujumbe na taarifa sahihi kuhusu CCM wamejikuta wakifanya makosa kwa kujiunga na vyama vingine vya siasa ambavyo havina mwelekeo wa kimaendeleo wala misingi ya uadilifu.