Wasome Wanawake tu: Siri za unyago wa Kimakonde! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasome Wanawake tu: Siri za unyago wa Kimakonde!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Zinduna, May 28, 2012.

 1. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwa kawaida wasichana hupata mafunzo ya unyago ndani ya nyumba siyo porini. unyago wa wasichana ni mgumu kuuelezea tofauti na ule wa wavulana maana mambo mengi hufanyika na wanawake kwa siri kubwa. Wamakonde wanaamini kuwa kueleza ovyo ovyo mintarafu mafundisho ya unyago kwa wasichana mtu huweza kuandamwa na balaa hivyo basi ni mwiko mkubwa kusema sema hadharani. Kamwe siyo rahisi kumithilisha mafundisho yale wapatayo wavulana na wasichana.

  Kwa jumla wasichana wanaohusika yawapasa kuvumilia taabu na magumu mengi pindi wawapo katika unyago. Ni marufuku kwa msichana kulia au kulalamika kwa sauti hata kama angeandamwa na maumivu makali namna gani. Hutawishwa kwa muda fulani pengine kwa muda fulani pengine kwa kipindi kirefu hadi ajaliwapo kupata mchumba.Maisha yote toka utoto hadi umri wa kuvunja ungo kwa msichana wa kimakonde hufuata madhehebu ya unyago yajulikanayo kama chiputu.

  Wamakonde wanaamini kuwa kwa msichana bila kupitia mafunzo ya unyago kwa jinsi ya mila na desturi yao matunda ya ndoa hayangefikia au yasingekuwa mema kwa sababu msichana yeyote asiyepitia unyago huhesabiwa kama mwanamke haramu. Mara nyingi hasa siku hizi wasichana hupata mimba kabla kabisa ya kupatiwa elimu ya unyago. Wanao angukiwa na mkasa kama huo hawapatiwi tena mafunzo ya unyago ambayo ni msingi kabisa wa maisha
  yao. Hupachikwa jina anahaku popote aendako. Wazazi hushikwa na majuto sana iwapo binti yao ameingia katika mkumbo huu wa akina anahaku.

  Anahaku huwa hawana raha maana huwakosa marafiki au huadhiriwa.
  Mafunzo ya unyago huanza mapema sana hasa kwa watoto walio watundu na watukutu. Wasichana wengine huwa wamekwisha kulumuka mwongo yaani kuvunja ungo kabla ya kuingia kwenye unyago. Hao hutofautishwa na wenzi wao kwa kuwavisha vidani viitwavyo inano (kundolela inano) kwa kupasua katikati mbegu ya mti uitwao mkangaula.

  Kamwe unyago haupangwi hivi ili ufanyike wakati msichana apatapo hedhi mara ya kwanza ili kama imetokea bahati hiyo basi Bi mkubwa yaani Likolo hutengeneza imale. Likolo hujipaka imale maungoni mwake na mwa walombo wengine ili kujikinga wasije wakapata upofu wa macho katika kushirikiana nao.
  Kama ilivyo elezwa hapo nyuma kwamba matendo ya madabwa yafanyikayo hayasemwi ovyo. Wasichana wa dini za kikristo hawapatiwi tena mafunzo ya unyago kwa ukamilifu bali hupewa mabugo ambayo ni mafunzo mafupi nayo hudumu kwa muda wa siku saba hivi. Hufundishwa juu ya miiko wajibu na matarajio ya mama wa Kimakonde katika jamii.

  Wasichana wote kabla ya kuingia unyagoni hujulikana kama anahaku wengi wanamahaku na baada ya kufundwa hujulikana kama mwali wengi wanawali. Akina mama hujikusanya pamoja na kufanya shauri la kuwapeleka binti zao kwenye chiputu. Wakisha afikiana humchagua Likolo kuwa ndiye mkuu wa taaluma za unyago. Ujira huo hutofautiana baina ya kijiji na kijiji kutegemea uhusiano na uelewa uliopo kati yao. Nyumba ya kutolea mafunzo hayo inande yanole huchaguliwa.Jioni ya siku iliyochaguliwa kuwa ndiyo ya kuanzia mafunzo ya unyago kila msichana atakaye hudhuria mafunzo hushikwa kukamula na wakala fulani ambao wameidhinishwa na wazazi.

  Wakala wa kuwakamata wasichana wanaweza kuwa ni wifi nnamuwe wake au mwanamke yeyote yule ambaye anajuana na yule msichana vya kutosha. Mwanamke ambaye ni wakala asiye shemeji yake huitwa ankamwe-nole.
  Baada ya kumshika msichana hupelekwa kwa mama yake. Mama binti mwenyewe pamoja na nnombo huenda pamoja hadi kule inande yanole. Wakaribiapo inande yanole huimba nyimbo za kumwandaa yule binti anaye sindikizwa kwenye chiputu. Wanapo wasili hapo wasichana huamkiana kwa kugonganishwa vichwa vyao ikiwa ndio ishara ya kuhimiza uhusiano mzuri kati yao kwa muda wote watakapo kuwa pamoja.

  Nitaendelea kuwadondoshea siri zaidi kesho, Inshaallah!

  MUENDELEZO....   
 2. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ole wake mwanaume atakayechangia uzi huu, akipata balaa la kuota majipu sehemu zake za faragha asije akanilaumu~~~~~ LOL
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wiki ijayo mie sitokuwepo.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wacha vitisho wewe Zinduna, hayo ni malove-malove tu. Labda wanaume wa Kimakonde ndio watakaotishwa na mkwala wako.
   
 5. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ngoja naku-PM muendelezo kabla hujakuwepo!
   
 6. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ibrah, wewe subiri joto ya jiwe tu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hao wenzio huwa hawachangii hadi madume yatie magulu.......Ushauri wa bure, ita wanaume hapa uone kama hawajaingia kingi.
   
 9. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Zinduna nipo shost, si unajua tena mambo ya mkate yamenichukulia muda hasa ukizingatia ni J3, Nimeona ya kimakonde nikitulia ntakuletea ya kimanyema na kitusi ili kukazia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  @mjasiria Ina maana hata Kina AshaDii na RussianRoulette wame - boycot?
  Siwataki kabisa ME kwenye huu uzi, wataharibu miiko ya wahenga wa unyago.
   
 11. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
 12. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Hao wote uliowaorodhesha ni ANAHAKU. Lizzy peke yake ndio kifaa.

  Na kuhusu mkwara wako hapa umenoa, majipu tayari ninayo, tena makubwa ya haja. Ukitaka naweza kukuruhusu uone yanavyoning'inia chini ya filimbi shaka hayana
   
 13. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Ooh, huyu keshafika, mtoto sikupendi wewe sijui kwa nini. Umeolewa?
   
 14. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  mie nikikuona roho inafanya lipu lipu lipu, kinachofuata ni kukuota usiku mzima.

  me love u Mwana Mtoka Pabaya. naomba niowe wewe, pleeeeease. hata mkiniowa wote na @Ribosome.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
 16. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya Zinduna umepitia au unataka tu kuolewa Rufiji?
   
 17. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Zinduna hujatenda haki, sema basi ni nini wanafundisha,

  sie ambao hatajaenda unyago tufaidike na wasituite anahaku.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  nikipitia hayo ndio utaniowa? mie ni quick lena.
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha Zinduna Jtatu tunakuwa busy ..
  Ngoja nisome nitauchangia huu uzi mida ya usiku akili imekaa powah..
  Ila kuna mambo itabidi unitumie PM kwa maswali zaidi
   
Loading...