Wasomali 90 na Wakenya 2 watimuliwa Marekani

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,400
Approximately 90 citizens of Somalia and Kenya have been displaced both from the United States a few hours after reports emerge that President Donald Trump will be faced by people living in the country illegally.

They have all arrived at the international airport in Nairobi Jomo Kenyatta.
Kenya's government spokesman Eric Kiraithe told the BBC that the citizens of Somalia will be flown directly to Mogadishu.

Trump prevent immigrants entering the United States
Mr. Trump said on Wednesday it will be an important day for US security.

He is expected to set strict conditions for the citizens of seven countries in the Middle East and Africa with the largest number of Muslims who seek visas to the United States.

-------------
Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Wote wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.

Trump kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani
Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.

Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.
058afd5e51784729eb155c1d6a71f6fa.jpg
 
_93644968_gettyimages-578546876.jpg

Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Wote wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.

Chanzo: BBC Swahili
 
"Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu," ameambia BBC.

Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani)".

Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.

Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.

Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi. Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

_93798285_trumpwall.jpg

Anatarajiwa kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.

Na hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

_93534566_3966cc6d-1ccb-4a00-b054-f82876db3c0b.jpg

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.

Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.

Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Hivi wewe utapata faida gani au ndio roho mbaya za kiswahili tu.
Wahamiaji wapo kila nchi ya ulimwengu kwani hata wao si walikuja afrika kutawala na kuchukua rasilimali pia.

Ndukiiiii
Wacha watimuliwe tu!!
 
Mzee ndo ameshaanza hivo
Saivi kwa muislam ama ngozi nyeusi kwenda marekani itakua ishu kweli kweli
Na nilisikia atauondoa ugaidi na magaidi on the face of the earth ..anaongea huku anakunja mdomo
 
Back
Top Bottom