expirience man
JF-Expert Member
- Nov 16, 2013
- 212
- 94
Ni mara yangu ya kwanza kuingia jukwaa la elimu lakini nimekuwa msomaji wa masuala mbalimbali ya elimu kama yanavyowasilishwa jukwaani. Wanabodi mimi nimehamasika kwa kipindi kuwa msomaji wa vitabu mbalimbali kama vili vya akina mother theresa, Ben Carson, Napoleon Hilo, Robert Kiosaki, Robin Sharma na wengineo, ambavyo nimepata maarifa na ufahamu wa mambo mbalimbali yakiwemo saikolojia, falsafa, biashara, uchumi na mambo kadha wa kadha. Pia katika kupia jukwaa hili nimewahi kupata vitabu vilivyowahi kupostiwa katika uzi mmoja uliopostiwa na mmoja wa wanabodi uliokwenda kwa jina " kitabu kilichowahi kubadili maisha yako", watu wakataja na kupost vitabu mbalimbali. Kwa hivyo leo mimi nawaomba wanabodi tupeane hamasa tupieni tena vitabu mbalimbai tukuze ufahamu wetu . Mie nilikua navyo vyote tajwa hapo juu lakini nilipotelewa na kifaa nilichohifadhia nyaraka hizo. Hivyo kwa heshi kubwq nawaombeni wakubwa na wadogo kila atakae pita hapa atipie chochote anachokijua. Samahani kwa uandishi wangu kama utawakwaza.