Wasira: Hakuna nchi isiyokuwa na manung'uniko

Wasira: Hakuna nchi isiyokuwa na manung'uniko

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Hakuna nchi ambayo haina mtu anayenung’unika- hakuna, hata ungelifanyaje kutakuwa na mtu pale ana matatizo yake na atanung’unika kwa wakati wake na mahali alipo. Ukisema watu wananung’unika nchini nitakuuliza wangapi wananung’unika maana tupo wengi.

Wakati nafanya kazi kwenye serikali ya awamu ya nne tulikuwa na Rais Jakaya Kikwete, tukimwambia mbona watu wananung’unika anatuambia nchi haipoi kama ugali wa jana, nchi lazima iwe inaongea. Na kwakweli kama kuna kitu kinaitwa uhai, ni pamoja na nchi kuongea. Kama nchi haiongei Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atajuaje kama kuna tatizo, na tatizo lipo wapi? Sio kwamba matatizo hayapo!.

Hakuna nchi ambayo haina tatizo na siwezi kukuambia kuwa Tanzania hakuna tatizo na nikikuambia kuwa hakuna tatizo, unaweza kunisaidia kunipeleka hospitali kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili.

Matatizo yapo na watu watanung’unika hapa na pale. Wewe umeniuliza hali ya siasa, hali ilivyo nchini, kwa tathimini vangu hali ni nzuri lakini haindoi maelezo kuwa matatizo yapo.”- Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara kwenye Dakika45 za ITV leo Julai 21, 2025.
 
Back
Top Bottom