"Wasiojulikana" wamepunguzwa kasi au ndio tuseme siku hizi kimeeleweka?

Wasiojulikana wanaojulikana....Pasco Mayalla.
 
He is guilty in his heart, he will be unhappy the whole of his life.
 
Word
 

Nakuunga mkono kwa maelezo haya, hii ndio maana chaguzi zinanajisiwa na hata zisipofanyika hao wafanya maovu hawajali ili miradi wanaendelea kukaa madarakani, maana usalama wao upo tu kama wataendelea kuwepo madarakani. Hivyo hilo kundi la watu wasiojulikana halijafa kabisa bali lengo lako la kuwatia wananchi woga limefanikiwa kwa kiwango fulani. Ikitokea tu wananchi wanaanza kuhoji kwa uwazi mambo ya serikali, hilo kundi litarudi tena kazini, na wahanga watakuwa vinara wa kuhoji.
 
Na DAB naye siku hizi yupo kimyaa... sijui ni coincidence au ndo hao hao..!!
 
Nadhani Watanzania tumefikia hapo. Tutafanywa lolote na viongozi wetu na kutulia tuli. Nyerere alikosea kusema kwamba Watanzania hawatavumilia kuona viongozi wachache wakiwanyima haki zao. Hakujua kuwa Watanzania sio Watunisia.

Mkuu tufanywe hivyo mara mbili? Kama uchaguzi mkubwa wa serikali za mitaa umetoa viongozi wasio na uhalali wa umma na inaonekana ni sawa, hapo unategemea nini?
 
Wanajulikana ila wanaowajua hawakuguswa ndiomaana ikawa kweli hawajulikani.

Kumbuka:-
1. Juma Ighondu baada ya kufanya mipango iliyofeli ya kumuua Dr Ulimboka, ametoweka mpaka leo hayupo Tanzania.
2. Aliye mnyoshea siraha Waziri Nape Yuko Wete Pemba, watu wamemuona huko Sasa anaishi maisha ya kujifichaficha
3. Waliompiga risasi Tundu Lisu, msimamizi wao anagombano na baadhi ya wakuu wa wilaya mkoani kwake hapakaliki

Kifupi nchi hii ni yetu tunawajua wote ila hawajatoa betri sehemu yenye mizizi

Ahsante Sana Chief

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ekweli na ushahidi uko wazi. Ni usalama wa taifa nje ya usalama wa taifa chini ya kiongozi mwenye baraka za magogoni asiye kuwa na akili kwa maamuzi na maslahi ya mgonjwa wa akili.
 
Mkuu Synthesizer , kumbe tulikuwa tunaionea serikali yetu bure, kwa kuihisi ni serikali inahusika na wasiojulikana hawa, kumbe...
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…