"Wasiojulikana" wamepunguzwa kasi au ndio tuseme siku hizi kimeeleweka?

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,704
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,704 2,000
Miaka kama miwili iliyopita kasi za kikundi cha "Wasiojulikana" ilikuwa ya juu ajabu. Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu nani hasa walikuwa nyuma ya hiki kikundi, na mengi sana yalisemwa.

Kwa wengi ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa kikundi cha "Wasiojulikana" kilikuwa hakina uhusiano na serikali kwa lojiki kwamba wale waliotekwa au kuuwawa walikuwa (victims) na "Wasiojulikana" ni wale tu walioonekana kuikosoa serikali au viongozi wa serikali, na hata Rais Magufuli. Kwa maneno mengine, ilionwa wazi kwamba uwepo wa kikundi cha "Wasiojulikana" ulikuwa kwa manufaa ya serikali iliyopo madarakani.

Na pia watu walihoji uwezo wa kifedha na ujipangaji wa kikosi hiki, ambao ni wazi haukuwa wa kikundi kisicho na mafunzo au kuwa na chanzo kikubwa cha fedha. Kwa mfano, gari aina ya Nissan Patrol mpya inayosemekana kutumika katika tukio mojawapo la "Wasijulikana" linasemakana kuchomwa moto ili kupoteza ushahidi.

Na ajabu ni kwamba mara zote matukio ya "Wasiojulikana" yalipotokea, Polisi walionekana kujiumauma katika kutoa majibu au kufanya upelelezi. Hadi leo hii, hakuna kesi hata moja inayohusu "Wasiojulikana" ambapo wahusika walikamatwa na kuhukumiwa.

Lakini sasa kikundi hiki cha "Wasiojulikana" ni kama kimepunguza kasi yake. Sintadiriki kusema kimefutwa au kukoma kuwapo. Je, ni kwa kuwa watu wameelewa kwamba katika awamu hii ukiikosoa serikali au watawala "utapotezewa" na "Wasiojulikana" ambao ni wazi wanafanya "uhalifu" kwa namna ya kuinufaisha serikali iliyopo madarakani dhidi ya kukosolewa na kutuhumiwa, huku serikali hiyo ikikana kuwafahamu au kuhusika nao. Inawezekana kuna mtu au watu wenye busara waliongea neno la hekima na "Wasiojulikana" wakawekwa gavana, kwa kuwa kuna wakati walifanya vitendo vyao kwa namna ya kuelekea kuwa kama enzi za "State Research Bureau" ya enzi ya Idd Amin wa Uganda, kikosi cha intelijensia kilichoteka na kuua yeyote aliyemkosoa Idd Amin na serikali yake.

Je, kuna siku ukweli kuhusu "Wasiojulikana" utajulikana?
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,704
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,704 2,000
Mungu ni mkubwa kuliko hata wao. Tusubili time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
Nasikia kuna wakati kuna mtu aliiambia serikali hivi, mie niko tayari kutangaza zawadi ya Tshs 300m (milioni mia tatu) kwa mtu atakaetoa taarifa kuhusu "Wasiojulikana" ili tujue ukweli. Alisema lazima "Wasiojulikana" wana rafiki, ndugu zao au hata wake zao, ambao wanajua mengi kuwahusu na watashawishika na zawadi. Basi tutangaze hii zawadi ili mtu atupe habari zao kwa siri.

Sijui kama hilo donge nono bado lipo, lakini nahisi huyo mtu aliambiwa waache polisi wafanye kazi yao usiwaingilie labda kama unataka uisaidie polisi!
 
technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Messages
8,690
Points
2,000

technically

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2016
8,690 2,000
Kundi la Bashite limepewa msukosuko mkubwa ndani hawana nguvu ya kufanya fake-operation kama walivyofanya kipindi cha nyuma.

Diwani Athumani anajaribu kusafisha

Ila kipimo ni kwenye uchaguzi ujao kama watu hawatapotea basi nitaamini kawapoteza.
 
Qwy

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2018
Messages
1,770
Points
2,000

Qwy

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2018
1,770 2,000
Miaka kama miwili iliyopita kasi za kikundi cha "Wasiojulikana" ilikuwa ya juu ajabu. Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu nani hasa walikuwa nyuma ya hiki kikundi, na mengi sana yalisemwa.

Kwa wengi ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa kikundi cha "Wasiojulikana" kilikuwa hakina uhusiano na serikali kwa lojiki kwamba wale waliotekwa au kuuwawa walikuwa (victims) na "Wasiojulikana" ni wale tu walioonekana kuikosoa serikali au viongozi wa serikali, na hata Rais Magufuli. Kwa maneno mengine, ilionwa wazi kwamba uwepo wa kikundi cha "Wasiojulikana" ulikuwa kwa manufaa ya serikali iliyopo madarakani.

Na ajabu ni kwamba mara zote matukio ya "Wasiojulikana" yalipotokea, Polisi walionekana kujiumauma katika kutoa majibu au kufanya upelelezi. Hadi leo hii, hakuna kesi hata moja inayohusu "Wasiojulikana" ambapo wahusika walikamatwa na kuhukumiwa.

Lakini sasa kikundi hiki cha "Wasiojulikana" ni kama kimepunguza kasi yake. Sintadiriki kusema kimefutwa au kukoma kuwapo. Je, ni kwa kuwa watu wameelewa kwamba katika awamu hii ukiikosoa serikali au watawala "utapotezewa" na "Wasiojulikana" ambao ni wazi wanafanya "uhalifu" kwa namna ya kuinufaisha serikali iliyopo madarakani dhidi ya kukosolewa na kutuhumiwa, huku serikali hiyo ikikana kuwafahamu au kuhusika nao. Inawezekana kuna mtu au watu wenye busara waliongea neno la hekima na "Wasiojulikana" wakawekwa gavana, kwa kuwa kuna wakati walifanya vitendo vyao kwa namna ya kuelekea kuwa kama enzi za "State Research Bureau" ya enzi ya Idd Amin wa Uganda, kikosi cha intelijensia kilichoteka na kuua yeyote aliyemkosoa Idd Amin na serikali yake.

Je, kuna siku ukweli kuhusu "Wasiojulikana" utajulikana?
Nadhani wamebadilisha styles lakini pia woga umekuwa ni mkubwa, siamini kama ukatili wao umepungua kwani tungefanyiwa japo 'danganya toto' ya kukamata angalau wawili au watatu.

Imagine 'mpuuzi' anakwambia uchunguzi wa tukio la kumshambulia Lissu haliwezekani kwa kuwa hajaja kutoa maelezo, hiyo inamaana mtu yoyote akishambuliwa kwa risasi na akafariki katika shambulio hilo haitawezekana kufanya uchunguzi kwani anayetakiwa 'kuisaidia polisi' amefariki.

Imagine kupotea kwa Ben Saanane polisi wanachukulia kama si tukio linalohitaji ufafanuzi wakati aliyepotea alikuwa ni mwanasiasa na tukio lina public interest.

Imagine tukio la Mdude CHADEMA pamoja na maelezo yote aliyoyatoa polisi wanachukulia kama vile hakuna kilichotokea.

'Wasiojulikana' hawajapunguza kasi bali wananchi wamakuwa waoga kusema ukweli ambao hauendani na matakwa ya serikali, hata mitandaoni wale wanaosifia(wengine kinafiki) ndiyo wanaojiachia kwa uhuru jinsi watakavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,704
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,704 2,000
Imagine tukio la Mdude CHADEMA pamoja na maelezo yote aliyoyatoa polisi wanachukulia kama vile hakuna kilichotokea.

'Wasiojulikana' hawajapunguza kasi bali wananchi wamakuwa waoga kusema ukweli ambao hauendani na matakwa ya serikali, hata mitandaoni wale wanaosifia(wengine kinafiki) ndiyo wanaojiachia kwa uhuru jinsi watakavyo.
Kwa hili la Wasiojulikana, inabidi uwe na akili za mwendawazimu kudhani kwamba serikali ilikuwa inasema ukweli juu yake. Na amini nawaambieni, kuwapo kwa Wasiojulikana na amri zilizotolewa kwao ni jambo ambalo linaweza kuwafikisha viongozi mahakama za kimataifa. Kwa sababu hiyo, upinzani hauwwezi kuachiwa uchukue madaraka 2020 kwa hali yoyote ile, kwa kuwa Upinzani wakichukua nchi jambo la kwanza kufanya itakuwa ni kupata undani wa Wasiojulikana - nani alikianzisha, nani alikisimamia, nani alitoa amri, waliotekwa wako, waliouwawa walizikwa wapi. Fikiria nani atakuwa tayari kuruhusu mazingira ya majibu kwa maswali hayo? Atakuwa tayari kufanya lolote ili mazingira ya ukweli yasipatikane.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,704
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,704 2,000
Kundi la Bashite limepewa msukosuko mkubwa ndani hawana nguvu ya kufanya fake-operation kama walivyofanya kipindi cha nyuma.

Diwani Athumani anajaribu kusafisha

Ila kipimo ni kwenye uchaguzi ujao kama watu hawatapotea basi nitaamini kawapoteza.
Diwani Athumani ana nguvu zaidi ya yule alietoa wazo la kuwapo kwa Wasiojulikana" na kuwapa fedha za operations?
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,704
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,704 2,000
Kuna waliopata majanga ya Mungu Yaani Almighty God alichowafanyia ni ushindi kwa waliodhulmiwa.
Nadhani Watanzania tumefikia hapo. Tutafanywa lolote na viongozi wetu na kutulia tuli. Nyerere alikosea kusema kwamba Watanzania hawatavumilia kuona viongozi wachache wakiwanyima haki zao. Hakujua kuwa Watanzania sio Watunisia.
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
16,476
Points
2,000

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
16,476 2,000
Miaka kama miwili iliyopita kasi za kikundi cha "Wasiojulikana" ilikuwa ya juu ajabu. Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu nani hasa walikuwa nyuma ya hiki kikundi, na mengi sana yalisemwa.

Kwa wengi ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa kikundi cha "Wasiojulikana" kilikuwa hakina uhusiano na serikali kwa lojiki kwamba wale waliotekwa au kuuwawa walikuwa (victims) na "Wasiojulikana" ni wale tu walioonekana kuikosoa serikali au viongozi wa serikali, na hata Rais Magufuli. Kwa maneno mengine, ilionwa wazi kwamba uwepo wa kikundi cha "Wasiojulikana" ulikuwa kwa manufaa ya serikali iliyopo madarakani.

Na pia watu walihoji uwezo wa kifedha na ujipangaji wa kikosi hiki, ambao ni wazi haukuwa wa kikundi kisicho na mafunzo au kuwa na chanzo kikubwa cha fedha. Kwa mfano, gari aina ya Nissan Patrol mpya inayosemekana kutumika katika tukio mojawapo la "Wasijulikana" linasemakana kuchomwa moto ili kupoteza ushahidi.

Na ajabu ni kwamba mara zote matukio ya "Wasiojulikana" yalipotokea, Polisi walionekana kujiumauma katika kutoa majibu au kufanya upelelezi. Hadi leo hii, hakuna kesi hata moja inayohusu "Wasiojulikana" ambapo wahusika walikamatwa na kuhukumiwa.

Lakini sasa kikundi hiki cha "Wasiojulikana" ni kama kimepunguza kasi yake. Sintadiriki kusema kimefutwa au kukoma kuwapo. Je, ni kwa kuwa watu wameelewa kwamba katika awamu hii ukiikosoa serikali au watawala "utapotezewa" na "Wasiojulikana" ambao ni wazi wanafanya "uhalifu" kwa namna ya kuinufaisha serikali iliyopo madarakani dhidi ya kukosolewa na kutuhumiwa, huku serikali hiyo ikikana kuwafahamu au kuhusika nao. Inawezekana kuna mtu au watu wenye busara waliongea neno la hekima na "Wasiojulikana" wakawekwa gavana, kwa kuwa kuna wakati walifanya vitendo vyao kwa namna ya kuelekea kuwa kama enzi za "State Research Bureau" ya enzi ya Idd Amin wa Uganda, kikosi cha intelijensia kilichoteka na kuua yeyote aliyemkosoa Idd Amin na serikali yake.

Je, kuna siku ukweli kuhusu "Wasiojulikana" utajulikana?
Kiongozi wao siku hizi anajifanya kuhubiri Injili pia kishakua tajiri kwaku tafuna misaada
Lizaboni
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,704
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,704 2,000
Kiongozi wao siku hizi anajifanya kuhubiri Injili pia kishakua tajiri kwaku tafuna misaada
Lizaboni
Mwache afaidi utajiri. Mtu unapewa fedha za operation ambazo hazina ukaguzi wala risiti, upewe nini zaidi ya hapo! Alikuwa anazigawa kama njugu. Ofisi yake ikawa tofauti na watu kama yeye, hata magari anayotumia - fedha kwa ajili ya kuua na kuteka watu. Labda dhamiri inamsuta ndio maana anahubiri na kulia hovyo. Damu ya mwanadamu ni nzito sana kuimwaga, hasa kwa tofauti za kisiasa tu.
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Messages
8,360
Points
2,000

Kinyungu

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2008
8,360 2,000
Kundi la Bashite limepewa msukosuko mkubwa ndani hawana nguvu ya kufanya fake-operation kama walivyofanya kipindi cha nyuma.

Diwani Athumani anajaribu kusafisha

Ila kipimo ni kwenye uchaguzi ujao kama watu hawatapotea basi nitaamini kawapoteza.
Bado unaamini kutakuwa na uchaguzi?
 
Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
7,514
Points
2,000

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
7,514 2,000
Kiongozi mkuu wa kikundi hiki ni abashite. Bado yupo. Na umaarufu wake mkubwa ulikuwa ni nafasi yake kwenye kikundi hiki cha mauaji, utesaji na utekaji. Wengi walimhofia kutokana na nafasi yake kwenye kikundi hiki. Maadam huyo bwana bado yupo, kikundi hiki bado kipo lakini yawezekana kuna wenye akili wamempiga gavana.

Ijulikane kuwa kikundi hicho cha Wasiojulikana ni kikundi cha kishetani, kwa hiyo hata kijijenge vipi, hakitakuja kiwe cha kudumu. Uovu hutamalaki kwa kipindi fulani tu, kisha uovu ule ni lazima uonje ukomo, iwe ni kwa umauti au kwa kukataliwa au kukomeshwa.
 
Forum statistics

Threads 1,391,376
Members 528,393
Posts 34,079,470
Top