Ndiyo maana nilikuambia kuwa CCM walishammaliza Dr Slaa kwani sifa pekee aliyokuwa anajulikana nayo ni UFISADI.
Waliruhusu makusudi Ufisadi usemwe wazi na mzigo wote akabebeshwa Lowassa wakati siyo kweli.
Ukiniambia Escrow Lowassa alilamba ngapi? Ntailipia kadi yangu ya CCM. Ukiniambia fedha zilizopotea Wizara ya Magufuli Lowassa alikula ngapi? Tatizo lenu ni kutufanya hatuna akili kwa kutulisha upuuzi wenu kuwa Fisadi ni Lowassa peke yake. Nchi ni giza, miaka 10 ya Kikwete bado anaiacha nchi giza. Lawama apewe Lowassa aliyeondoka miaka 8 iliyopita.
Slaa alishapoteza umaarufu wake kwa namna moja au nyingine. Asingeliweza kushindana na CCM hata kidogo. Na ili kuonyesha hilo, serikali za Mitaa, Chadema walifanya vibaya sana. Hata wewe umelijua hilo na umeliandika hapa kwenye BOLD. Sasa ili kutibu hilo tatizo, LOWASSA kaja na kibao kimegeuka. Mnahemewa Kisogoni kwa mara ya kwanza.
Hata kwa Mbinde, safari hii lazima Lowassa awachukue.
https://www.youtube.com/watch?v=mnAlHuGWOFg
CCM ni baba wa UFISADI, kama kweli Magufuli ni mzalendo na Muadilifu kama mnavyompamba kwenye Mabango barabarani atwambie kwanini alikuwa dalali wa uuzaji wa nyumba za serikali, kwanini amenunua Meli chakavu kwa mabilioni ya pesa? kama taasisi iliyo chini yake Tanroads inanuka kwa rushwa je yeye kaponea wapi? Kwanini alikamata meli na kugawa Samaki ilihali alijua kwa kufanya hivyo anavunja sheria za kimataifa...ona sasa tunatakiwa kulipa billions kama fidia....je kwa mifano hiyo michache Unamtofautishaje Magufuli na UFISADI?