Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
Hao NIDA wanadhani kuna mwananchi asiyetaka kuwa na kitambulisho? La hasha. Tatizo ni NIDA kukosa ubunifu wa kufanya kazi kwa ufanisi.
Tumejiandikisha, tena kwa tabu kubwa sana ya kushinda vituoni, na bado vitambulisho hatupewi. Mie nilijiandikisha awamu ya kwanza na kupigwa picha. Miaka imepita lakini bado sina hicho kitambulisho cha taifa. Ila nina passport.
Huu "ugumu" uko kila sehemu ya serikali Tanzania. Nilikwenda TRA nikashindwa kulipa kodi ya jengo kwani "taarifa walizokusanya mwaka jana bado ziko kwenye makaratasi kama unavyoyaona, bado hazijaingizwa kwenye kompyuta" . Baadaye utawasikia wakigomba kwamba hatutaki kulipa kodi za majengo.
Mheshimiwa Rais, hiyo civil service yako ni mbovu kila mahali. Ifanyike kitu kinaitwa "spill and fill" kila idara. Yaani wanaachishwa wote idara kwa idara, nafasi zinatangazwa na kujazwa upya. Walioachishwa wanashindanishwa na waombaji wapya.