Wasimamizi Yanga Day Ovyo Kabisa

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
890
1,566
Tayari tumewazoea, ila hatukujua kama hamjabadilika.

Hakuna tamasha la Siku ya mwananchi liliwahi tamatika bila vituko, malalamiko au majonzzi katika miaka ya hivi karibuni. Mwanzo tuliamini bado ni wachanga katika matukio makubwa kama haya. Ila umefanya matukio kama haya zaidi ya mara tano kwanini hakuna mabadiliko?

Leo sasa, ukitoa tamasha kuendeshwa kiswahili swahili(very unprofessional) kuna mambo mengi ni ngumu kuelewa.

1. Suala la ratiba, hii ni kichekesho watu wameanza kuingia saa tatu, unakuja kuwatoa saa tano dakika 20 usiku? Siku ya jumapili na kesho ni shule na makazini?

2. Hivi Haji Manara na kundi lake ni kitu gani walikua wanafanya pale? Mazoea au Jeuri, wamevunja protocal nyingi plus unnecessary drama hadi kero.

3. Show kuwa chini ya kiwango, hivi Harmonize amefanyaa show bure? Sijaona zaidi ya washa tochiii.. Marioo nao ni wale wale poor, very poor.

4. Yuko wapi Ali Kwamwe? Heshimuni sana jitihada za huyu kijana.

Na mengine mengi.

Kipi kimekufurahisha au kukukera siku ya leo?
 
Inaonekana hawakuwa na ratiba ikabidi vice president wa nchi ashuke aseme neno maana wanajiendeshea matukio kienyeji,angezubaa kidogo wangemruka waendelee na azizi na mobeto huyu teacher wangu wa chuo alijiongeza haraka ,pili :-hakuna flow manager waongeaji wengi ni holela holela kwa sababu tukio ni lao ,inafika wakati unamuita hata mchezaji ambaye hayuko tayari na unawatisha watu hauondoki mpaka afike🤣🤣🤣
 
Show imefunika vibaya mno, watu hawakumbuki kabisa kama jana tu ilikuwa Simba day! Kila kitu kilikuwa super mwake mwake babake!! Yanga inatisha kwenye show za kibabe, dunia nzima imeona na kushangaa jinsi Yanga inavyoshinda kila kitu hadi matamasha na mafataki!!

Vitu vilivyowauma sana makolo ambavyo hawana ni wananchi kuvaa uzi mpya uwanja mzima jana zilikuwa kauka nikuvae jezi za zamani mashabiki wa Simba hawana hela ya jezi, makombe matatu makali, mashabiki kujaza viwanja viwili ni maajabu, nongwa za Manara kutambulisha dada zake wa ikwiriri, mrembo Mobeto kuvalishwa jezi na Ki Aziz , kiongozi mkubwa sana kupewa kadi, gari kali la Kitenge, show bab kubwa ya Marioo na Harmonize na ile show kabambe ya half time, mpira kama Real Madrid msako mkali mwanzo mwisho timu ina muunganiko, goli la dhahabu la Mudathir, chenga hatari za Pacome na penati ya karne ya Ki Aziz kipa kaenda sokoni na mengineyo.

Makolo muwe mnaanza tamasha lenu kila siku sisi uto tunamalizia na kuwapoteza!!
 
1. Suala la ratiba, hii ni kichekesho watu wameanza kuingia saa tatu, unakuja kuwatoa saa tano dakika 20 usiku? Siku ya jumapili na kesho ni shule na makazini?
Sasa hapa kosa la Yanga liko wapi?
Ile n kazi yao kwahy na nyie mashabiki mfanye kazi yenu, kama unaona kesho unaenda shule n kwann ukae mpaka usiku?
Ww unawalipa kupitia kiingilio je wao wanakulipa pale?
JPM alikuwa sahihi sana kusema simba na Yanga wanawapumbaza wananchi.
 
Ahmed Ally ni mtu mmoja ila kapangilia Sana siku yake. Kwanza kitendo Cha kutumia ngoma ya kienyeji ni superb Sana tofauti na Hawa waliokuwa wanatuambia mikono juu, kushoto kulia, say yo yo, washa tochi wakati mwanga ni mkali. Mzungu wa buza na Yale ma I iiiiiiiiiii habadiliki. Wamezidiwa mpaka na ashim ibwe kule rwanda Jana? Mimi huwa sijui wale chawa mwenye timu kitenge na zembwela huwaleta wa nini?
 
Tayari tumewazoea, ila hatukujua kama hamjabadilika.

Hakuna tamasha la Siku ya mwananchi liliwahi tamatika bila vituko, malalamiko au majonzzi katika miaka ya hivi karibuni. Mwanzo tuliamini bado ni wachanga katika matukio makubwa kama haya. Ila umefanya matukio kama haya zaidi ya mara tano kwanini hakuna mabadiliko?

Leo sasa, ukitoa tamasha kuendeshwa kiswahili swahili(very unprofessional) kuna mambo mengi ni ngumu kuelewa.

1. Suala la ratiba, hii ni kichekesho watu wameanza kuingia saa tatu, unakuja kuwatoa saa tano dakika 20 usiku? Siku ya jumapili na kesho ni shule na makazini?

2. Hivi Haji Manara na kundi lake ni kitu gani walikua wanafanya pale? Mazoea au Jeuri, wamevunja protocal nyingi plus unnecessary drama hadi kero.

3. Show kuwa chini ya kiwango, hivi Harmonize amefanyaa show bure? Sijaona zaidi ya washa tochiii.. Marioo nao ni wale wale poor, very poor.

4. Yuko wapi Ali Kwamwe? Heshimuni sana jitihada za huyu kijana.

Na mengine mengi.

Kipi kimekufurahisha au kukukera siku ya leo?
Mimi ni Yanga ila Manara analeta mambo ya kipumbavu wakati anajua tukio hili Kuna watu wametulia kufuatilia anatuletea mambo ya uhuni uhuni.Mfano Habari ya Aziz Ki na Mabeto haya ni mambo ya wasanii huko yeye analeta kwenye mpira
 
Hizi show zinajadiliwa kishabiki sana aisee.
Ya mwananchi imefana sana, ilikua na burudani kedekede, wasanii wa kuzidi, shangwe kama lote.
Djs wa kimataifa..

Simba walichofeli mpaka vibe kushuka ni kuingia ubia na crown fm, djs wachanga wa crown fm ndo wakahost tamasha na wasanii wao kina Mwijaku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom