Wasimamizi wa namna hii sijawahi kuwaelewa wanachokifanya

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kuna tabia huwa siielewi kutoka kwa watu tunaoamini ni wataalam!

Afisa wa polisi anaposimamisha basi na kuhoji abiria mbele ya dereva kwamba "Wanaonaje mwenendo wa dereva"

Sijui huwa unatarajia jibu gani jingine zaidi sifa njema kwa dereva!

Hata kama lengo ni zuri lakini ukikosea namna ya kulifikisha navyoamini huleta majibu ya uongo
abiria gani atathubutu kumsema vibaya dereva akiwepo hapo wakati ndiye anmtegemea asafiri naye hadi mwisho wa safari? Kwanini wasinge kuwa wanawaamuru madereva washuke chini ili wawahoji abiria kwa uhuru?

HILO SIYO KWA MAAFANDE TU...
Hata mashuleni wasimamizi wa mitihani ya kitaifa wanapotekeleza majukumu ya usimamizi
Huwa kuna wakaguzi (afisa elimu) wanapita kila shule kukagua mwenendo wa mitihani!

Mbele ya msimamizi Watoto huulizwa na AFISA ELIMU Kwamba mnaonaje MSIMAMIZI WENU anavyowasimamia vibaya au vizuri? amewapatia mtihani ukiwa sawa? n.k
Maswali kama hayo watoto unapowauliza mbele ya msimamizi unategemea watajibu nini tofauti?

Afisa elimu anahoji watoto mbele ya mwalimu wao kwamba! WALIMU WENU HUWA WANAACHANGISHA mia 200 za mitihani kila wiki?
maswali ya sampuli hiyo kama mkaguzi mwenye weledi unapowahoji watoto mbele ya mwalimu wao huwa wanategemea nini?

madodoso ya kutafta taarifa inaonekana bado ni changamoto kubwa sana!

Mambo tunayokutana nayo wananchi huku chini yanafika huko juu yakiwa na taswira tofauti kabisa kutokana na ukosefu wa weledi wawasimamizi

Mfano! Kuna mitihani ya darasa la nne inaendelea nchini; Baadhi ya shule wamechangisha kila mtoto elfu 6 had elf 10 ya chakula kwa kila mtoto!

lakini watoto wamepatiwa robo kikombe cha chai ya rangi,na viandazi viwili asubuhi, mchana watoto wamekula kifinyango kimoja cha nyama na ubwabwa mbaaya! eti wapishi ni watoto wenzao wa darasa la sita kwa kushirikiana na jimama ntilie! serious?

Majanga ya kiafya yakitokea serikali inakuwaga haina taarifa kwasababu haina weled wa kupata taarifa! maafisa hawana weledi kwenye kazi zao wanafanya bora liende tu!
Leo nimezunguka baadhi ya shule Ugindoni primary, mjimwema, raha leo zilizopo kigamboni Nimegundua madudu hayo!

Tena kama pale shule ya msingi Ugindoni watoto wanachangishwa michango mingi sana na wanaambiwa akija mkaguzi watoto wasiseme kama wanachangishwa!

WATAALAM TUMIENI MBINU KUPATA TAARIFA
 
Acha majungu kuchangishwa 6000, ambayo mwanao anakula ndo inakuwa nongwa, mbona ukikamatwa na trafiki hulii unavolia hivo, ulitaka hao walim wakale wapi?
 
Acha majungu kuchangishwa 6000, ambayo mwanao anakula ndo inakuwa nongwa, mbona ukikamatwa na trafiki hulii unavolia hivo, ulitaka hao walim wakale wapi?
ndiyo watoto wapewe kiandazi kimoja na wali mbovu kweli?
Pesa chukua lakini wape watoto kilicho bora ....
wali mbovu maharage manne na michuzi mwaah! watoto wamehesabu yaani ubwabwa mbovu maharage yakuhesabu hayafiki hata matano! mchango elfu 6 kweli?
 
poleni sana ndiyo nchi yetu ndugu
 
ndiyo watoto wapewe kiandazi kimoja na wali mbovu kweli?
Pesa chukua lakini wape watoto kilicho bora ....
wali mbovu maharage manne na michuzi mwaah! watoto wamehesabu yaani ubwabwa mbovu maharage yakuhesabu hayafiki hata matano! mchango elfu 6 kweli?
Tunaomba picha ya wali mbovu na maharage manne
 
Yaan upigaji kilaa konaa Tz hii

Ss hapo wangefanya hyo 6000 mtt ale hapo buku tatu na wao waalimu wale buku tatu.

Chai 300,andazi 3x200=600
Wali 2000
 
Yaan upigaji kilaa konaa Tz hii

Ss hapo wangefanya hyo 6000 mtt ale hapo buku tatu na wao waalimu wale buku tatu.

Chai 300,andazi 3x200=600
Wali 2000
kilo moja ya mchele watu wazima hila wanne ...hivyo kwa watoto ni 8 ...inamaana kuwahudumia vyema watoto wameona tabu ndo wakawapa wali mbovu na kinyama kimoja kama mshikaki na maharage manne kweli? nchi yetu ina watu wa hovyo sana!
 
Acha majungu kuchangishwa 6000, ambayo mwanao anakula ndo inakuwa nongwa, mbona ukikamatwa na trafiki hulii unavolia hivo, ulitaka hao walim wakale wapi?
Hahaaaaa, kuna wazazi wana nongwa kweli. Yaani mtu kuchangia elfu 2 anataka mwanaye ale piza na soda shuleni.

Binafsi sijaona kosa hilo la kuulizwa eti mnaonaje mwendo wa Dereva. Kama anaendesha hovyo, nasema mbele yake kwa huyo trafiki.
 
wewe ukiulizwa uinange JF mbele ya mkurugenzi wa JF utaweza?

pia inaonekana huna nidham ya fedha kabisa!

ukienda hotelini ukalipia sangala mkubwa kwenye menu then ukaletewa kiperege kiduchu hivi cha uvundo hutaacha kuuliza?
 
Unatetea wezi?Hiyo elfu sita huwa inaokotwa jalalani?Behave yourself!
kwanza wanakatisha tamaa viongozi wakubwa wenye ndoto za kuweka sera ya chakula mashuleni!

walitakiwa wajitathimin kupitia vijihuduma kama hivi!
kama wamechakachua vyakula vya watoto wa darasa moja watawezaje kwa shule nzima?

kwanza kumtapeli hadi mtoto mdogo akagundua ni dhambi!
Ukishindwa kumlaghai mtoto mdogo kwa huduma nzuri wewe akili huna
 
Hii post ilikuwa maalum kwaajili ya hao walimu ila polisi na afyawameandikwa kisindikizaji tu
ujue kuna mazoea wataalam wetu huwa wanayafanya ambayo kimsingi hayana faida kabisa !

MKAGUZI ELIMU/ Afisa elimu unazunguka kukagua kasoro za walimu! then Unahoji watoto mbele ya mwalimu huyohuyo unaetaka kujua taarifa zake mbovu! Ajabu kwelikweli
 
Kabla huyo traffic hajapanda ngazi kuingia kwenye basi kuuliza hayo maswali pale chini konda anakuwa kashampatia elf2 yake so humo anaingia kama ushahidi tu aonekane ametimiza wajibu.

Ila cha ajabu kila j2 au ijumaa unawakuta wapo kwenye nyumba za ibada wana sali na kuswali.
 
Back
Top Bottom