Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Habari wanaJF,
Nimeona ni vyema nikawapitisha kwenye wasifu mfupi wa ndugu Emmerson Mnangagwa ambaye anatajwa sana hivi sasa katika mgogoro wa kisiasa unaondelea katika nchi ya Zimbabwe.
Alizaliwa mnamo tarehe 15 September, 1942.
Alisoma elimu yake ya O-Level na A-Level akiwa ni Mfungwa. Mwaka 1972 alimaliza kusoma Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha London na Postgraduate ya Sheria pia.
Mwaka 1962 alijiunga rasmi na chama cha Zimbabwe African Peoples Union (ZAPU) Kisha akaondoka kuja Tanzania kwaajili ya kambi ya mafunzo ya Kijeshi.
Mwaka 1963 Chama cha ZAPU kikamtuma tena kuja Dar es Salaam kisha nchini Misri kwaajili ya mafunzo ya Kijeshi.
Mwaka 1964 alimaliza mafunzo ya Kijeshi na kuunda kundi la 'Crocodile Group' ambalo lilikuwa kwaajili ya kusafirisha silaha kuingia Zimbabwe na kusajili wafuasi ambao wengi wao walisafiri kuja Tanzania kwaajili ya mafunzo.
Mwaka 1965 bwana Mnangagwa alikamatwa na kushikiliwa ambapo aliteswa na kuhukumiwa kwa makosa ya uhaini akafungwa miaka 10 ambapo alikuwa pamoja na Wanaharakati wengine akiwemo Rais Robert Mugabe.
Mwaka 1977 alichaguliwa kuwa msaidizi rasmi wa Rais wa ZANU na kuwa kiongozi wa Divisheni ya Kijeshi ndani ya Chama.
Baada ya ukombozi wa Zimbabwe alihudumu katika nafasi mbalimbali katika Baraza la Mawaziri la Zimbabwe ikiwa ni pamoja na Waziri wa Wizara ya Ulinzi, Sheria, na Masuala ya Bunge.
Ni mmoja kati ya Wanasiasa Matajiri nchini Zimbabwe.
Umoja wa Mataifa umewahi kumtuhumu kwa kujihusisha na biashara ya Almasi kinyume cha Sheria. Umoja wa Mataifa ukashauri awekewe vikwazo vya kusafiri na vya kiuchumi.
Mwezi Disemba mwaka 2014 Rais Robert Mugabe alimteua kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais baada ya kutengua uteuzi wa Joice Mujuru. Mujuru amekuwa hasimu wa muda mrefu wa bwana Mnangagwa katika vita ya kupigania madaraka.
Mnamo tarehe 06 Novemba mwaka 2017 Rais Robert Mugabe alitengua nafasi yake ya umakamu wa Rais na kuanza mchakato wa kumuweka Mke wake Bi. Grace Mugabe.
Ni hayo tu kwa ufupi.