Amani iwe kwenu Great thinkers
Kwa kweli wote tumeona ushujaa uliooneshwa na Mbunge wa Chadema Arusha mjini katika kudai uchaguzi huru wa meya na naibu wake. Katika harakati hizo ilipelekea yeye kupigwa kionevu na polisi hadi kulazwa hospitali. Still hakukata tamaa, na akaanda maandamano makubwa ya kudai haki hiyo ambapo polisi walimkamata pamoja na viongozi wengine wa CDM huku wakimwaga damu za watu wasiokua na hatia. Hili limetikisa nchi na tunaamini lazima uchaguzi urudiwe. Hivyo basi kwa kutambua mchango wa GODBLESS LEMA, tunaomba yeyete mweye kujua background yake atujuze hapa jamvini.
Mimi nadhani ukiona huna cha kuchangia si lazima uandike wakati mwingine unaweza kuipotezea tu thread kama uhuisani nayo, mdau ameomba cv ya mtu kwa kua yeye anahitaji kumfahamu, lakini baadhi ya wachangiaji wameanza kwa kutoa majibu ya dharau, yasiyohusiana lakini pia wapo waliotoa jibu la moja kwa moja kulingana na maswali. Tuheshimu mada/mawazo/kutoelewa/kuelewa kwa jambo ambalo mtu anahitaju ufafanuzi. Ni hayo tu
exactly,,,tena ni mchaga kama mbowe
Kwa kuwa anajua matatizo ya vijana wengi mkoani humo na yeye binafsi ameshawahi kuwa katika kadhia hiyo, hapana shaka atatumia muda wake wa ubunge kutatua matatizo hayo. Badala ya kupoteza muda kwa shughuli ambazo hazina tija kwa wapiga kura wake!
Michelle kwa kusafisha majina ya "wanyumbani" kwa kweli nakukubali....Huyu jamaa angekuwa wa kwengine sidhani kama kungelika hapa na CV yake ya ubabaishaji Bin ujanjaujanja....
Pia Godbless Ni mpambanaji na Visionary wa maendeleo. Always haamini katika kushindwa bali siku zote anaamini kuna best alternative. Hii ilimpelekea kuamua kuunda ArDF yaani arusha Development foundation ambayo tayari mwaka huu inalipia watoto 1000 kutoka familia fukara ada shule ya sekondari hasa kwa walnaoanza form one. 2011.
Ana mpango wa kupeleka wanafunzi wa maskini 25 kusoma vyuo mbalimbali vikuu vya nje na tayari amekwisha establish contact na vyuo hivyo.
Ana mpango wa kutumia slabs au vimatofali kujenga barabara za mji badala ya lami.Hii itapunguza 50mil. TZS kwa kila KM 1 ya barabara itakayojengwa. Yuko determined na anayo support kubwa nyuma yake ambayo si tu ya mnaowaona mikutanoni bali hata millionaires wa Arusha ambao ni wafanya biashara na wasomi wakubwa. Nguvu yake ya kujiamini inatokana na support ya walioko nyuma yake na ukweli anaweza
Godbless Lema ni mtoto wa mjini, tapeli turned into politics. Kama ukiweza fanya background check yake pale mahakamani utaona mara ngapi alivyoburuzwa kortini kwa tuhuma kibao za utapeli. Ila demokrasia imechukua mkondo wake na kapewa ubunge na wana Arusha.
umeimalizia vizuri sana post yako.wananchi wamechoka na 'wasomi' waliotegemewa kuleta mabadiliko wamechemsha hivyo wenyenchi wametumia haki yao kumuweka mtu atakayetekeleza wanachokikata.
Amesoma kama sikosei advanced Diploma ya HR pale IAA
Ni mume wa Neema Tarimo
Ana watoto wawili
Ni mchaga wa Machame
Ni mfanyabiashara
Amejiunga CHADEMA akitokea TLP,aligombea ubunge kupitia TLP 2005
Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Lutheran
...............................................................................

Mi ninavyojua godbleas lema,ni mmachame,wa nronga,ni baba wa watoto 2,kuhusu elimu mi sijui kapataje diploma,mana najua ajafika form 4.aliyesoma nae au anayejua shule aliyesoma atujulishe.
Amesoma kama sikosei advanced Diploma ya HR pale IAA
Ni mume wa Neema Tarimo
Ana watoto wawili
Ni mchaga wa Machame
Ni mfanyabiashara
Amejiunga CHADEMA akitokea TLP,aligombea ubunge kupitia TLP 2005
Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Lutheran
...............................................................................
...............................................................................
...............................................................................
kwa kweli mm simjui mbunge huyu wa arusha, ila kwa matukio ninayoyaona kupitia tv na redio anaonekana ni mtu jasiri sana, mungu amsaidie asonge mbele,tunahitaji watu majasiri kama lema kwa wakati huu ili tuweze kutoka katika minyororo ya utawala thalimu wa CCM.