Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Wanaouliza Bashru kuanza shule akiwa Na umri wa miaka 12 jibu Ni kwamba, zamani kuanza la kwanza lazima mkono wako ushike sikio upande wa pili. Kama alikuwa mfupi hata miaka 14 inawezekana kuwahi kuanza kusoma sio kuwahi kupata kazi
 
Mbona mwamba anatakribani miaka 20 akiwa mwenyekiti wenu wa chama, kwani huko kwenyechama chenu wote mnaajira??
Mimi si mwanachama wa chama chochote kile cha kisiasa. Mimi ni Mtanzania tu Mzalendo, Mpenda mabadiliko, na ADUI Namba 1 wa CCM
 
Kwahiyo? Futa utopolo huu. Au ni shemeji yako! Anamshikisha dadiyo?!?
We inakuuma nini badala utafute pesa huku ukisubiri swahiba wako akipata urais ndyo nawewe utapata uteuzi
 
Mimi si mwanachama wa chama chochote kile cha kisiasa. Mimi ni Mtanzania tu Mzalendo, Mpenda mabadiliko, na ADUI Namba 1 wa CCM
Kwahiyo leo umemukana mwamba na yule jamaa yenu aliyegaragazwa kwenye sanduku la kupigia kula, kisha akatengeneza kiki ya kwenda ugaibuni kukwepa aibu ya kugaragazwa??
 
Kwahiyo leo umemukana mwamba na yule jamaa yenu aliyegaragazwa kwenye sanduku la kupigia kula, kisha akatengeneza kiki ya kwenda ugaibuni kukwepa aibu ya kugaragazwa??
Kumuunga mkono Tundu Lissu anapo inyoosha ccm na mwenyekiti wake, kuunga mkono mabadiliko yoyote yale ya kuiondoa ccm madarakani hakunifanyi mimi kuwa mwanachama wa chama chochote kile cha siasa.

Yaani hata atokee kichaa kama Adolf Hitler, akiahidi tu kuiondoa ccm madarakani! Hakika nitamuunga mkono. Ccm ni ukoo wa panya. Ikiendelea kuitawala nchi yetu, umaskini wa kipato utaendelea kuwaumiza wananchi wengi, nikiwemo mimi! Na hilo halikubaliki.
 
Miaka ile ili mtoto aweze kuingia darasa la Kwanza sharti mkono uguse sikio kupitia juu ya kichwa,ukiwa mfupi ndo Bas tena waweza Anza at 15,Miaka yenu hii hata miaka 3 mnaanza shule ndo maana kichwani ni shida tupu
nani alikuja na idea ya kindezi hivo kushika sikio ndio uanze shule?
 
Siku hizi Watanzania tulio wengi hatuwataki Viongozi wenye experience ya kimatifa, maana wengi wao wanaishia kua vibaraka wa Mabeberu na kuuza Rasilimali zetu kwa bei Chee kupitia Mikataba yao mibovu!!
Viongozi wa hvo walimsaidia mno Jakaya ndio maana enzi zake hela nje nje, ajira aliajiri na uwekezaji ulikuwa mkubwa, huwezi linganisha watu wenye international exposure na mtu wa kijijini kwenye maamuzi aisee. Exposure na experience ni kitu muhimu kwenye kazi
 
Viongozi wa hvo walimsaidia mno Jakaya ndio maana enzi zake hela nje nje, ajira aliajiri na uwekezaji ulikuwa mkubwa, huwezi linganisha watu wenye international exposure na mtu wa kijijini kwenye maamuzi aisee. Exposure na experience ni kitu muhimu kwenye kazi

Sawia kabisa. Mimi namuangalia sana Uhuru Kenyatta,exposure imemsaidia sana kuiendesha ile nchi. Japo ana mapungufu,ila uchumi wa ile nchi umechangiwa sana na maisha aliyoishi kabla ya kuwa president
 
Jamaa zangu washapiga mahesabu fulani tayari....kila kitu kinachotokea hakitokei kwa bahati mbaya...
 
Sawia kabisa. Mimi namuangalia sana Uhuru Kenyatta,exposure imemsaidia sana kuiendesha ile nchi. Japo ana mapungufu,ila uchumi wa ile nchi umechangiwa sana na maisha aliyoishi kabla ya kuwa president
Sasa sisi karne ya 21 viongozi wanatumia Sera za ujamaa zilizofeli enzi za Nyerere, kila kitu serikali inafanya na kuua Sector binafsi inayoajiri maelfu ya watanzania. Sasa kila ujenzi serikali na kila kitu kime centralized
 
Wasifu wa Dakta Bashiru kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

=====


Huyu ndiye Dk Bashiru Ally​


Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala ni uteuzi wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa balozi na katibu mkuu kiongozi.

Ni uteuzi ambao haukutarajiwa uliokwenda sambamba na msomi huyo kuteuliwa kuwa balozi, wengi wanajadili uzoefu wake wakiamini anaweza kuitumikia vyema nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dk Bashiru ulitangazwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na mapema leo Rais John Magufuli amemuapisha kwa mujibu wa katiba ya nchi na kuanza kutumikia upya wadhifa wake huo mpya.

Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.

Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari ya Kilosa mkoani Morogoro alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1990 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo iliyopo Bukoba alikosoma kidato cha tano na sita na kumaliza mwaka 1993.

Mwaka 1997/98 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya kwanza sayansi ya siasa na kumaliza mwaka 2000 ambapo aliunganisha na kusoma shahada ya uzamili aliyomaliza mwaka 2002.

Mwaka 2003 aliajiriwa na taasisi ya Haki Elimu lakini mwaka huohuo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe ambako alifundisha kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kama mhadhiri msaidizi.

Akiwa chuoni hapo aliendelea na kusoma akichukua shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Amewahi kuwa makamu mwenyekiti na kaimu mwenyekiti wa Chama cha kitaaluma cha UDSM (Udasa), makamu Mwenyekiti wa chama cha wanataaluma nchini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei, 2018 Dk Bashiru akiwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa UDSM vilevile alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.

Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.

Chanzo: Mwananchi
Huyu anatoka katika familia ya wakimbizi toka nchi jirani kama jiwe
 
Back
Top Bottom