Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Kwa hoja hii akili zako zinakuaminisha kuwa msimamo wako haujulukani
Na hili ndilo tatizo linalo wasumbua nyinyu Mataga! Yaani mnadhani kila anayeichukia ccm au mwenyekiti wenu kutokana na utawala wa hovyo, basi ni lazima awe Chadema! Poleni sana.
 
Ukimaliza drs la 7 na miaka 12 unakuwa umeanza la kwanza na miaka 3? We kweli kiazi. Halafu eti na wewe unajua kuandika na kuhesabu!
we bibi mwenye nyege iyo3 nimekosea kuandika!napo miaka5 uwez kuanza darasa la kwanza
 
Bado we ni kiazi kweli. Ukimaliza la saba na miaka 12 unakuwa umeanza la kwanza na miaka 5? Kwa hesabu za wapi? Halafu na wewe umeenda while?
 
Ukimaliza drs la 7 na miaka 12 unakuwa umeanza la kwanza na miaka 3? We kweli kiazi. Halafu eti na wewe unajua kuandika na kuhesabu!
hajui huyo hesabu anayemaliza la saba akiwa na miaja 12 la kwanza huanza akiwa na miaka 6
 
Age ni Numbers tu pia ana achievement kubwa ambayo wewe hutakaa umfikie
Wewe umefiri vizuri sana.Huyo amefanikiwa kwa haraka sana.Na pia inaonyesha huyu jamaa amekulia mazingira magumu utotoni na pia bright sana.
 
Kati ya wanawake wenye uono wa mbali ni pamoja na mke wa mh.Bashiru. Mwanamke huyo aliolewa na mheshimiwa ambaye alikuwa hana kazi kwa kipindi hicho wakati mwanamke akiwa ni mwalimu shule ya msingi Kanazi. Nafikiri mwanamke ana mchango mkubwa sana kwa mheshimiwa.
 
Sababu ya kuchelewa kuanza shule inawezekana mazingira ya Kijijini kwao,labda alikuwa anatakiwa kuchunga ng'ombe kwanza.

Kuna msaidizi mmoja wa Nyerere alienda Bwiru kuanza kidato cha kwanza akiwa nyumbani kwao kaacha mke.
Zamani ilikuwa kawaida.
Huyu msheshimiwa kusema ukweli ni mtu wa bahati sana. Hakuzaliwa familia ya kishua. Ujombani kwao na mke wake wameplay part kubwa sana kwenye mafanikio yake. Pia alipomaliza form six alifundisha kwa kujitolea shule ya sekondari Kashozi huku akiuza mihogo kwa wanafunzi na ndo alipo bahatika kumuoa mke wake ambae alikuwa mwalimu shule ya msingi Kanazi.
 
Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.
Alikwenda standard one akiwa na miaka 12!!!
 
Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.
"Waliniambia nimemteua kuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati yeye ni CUF, na mimi nikasema, huyohuyo wa CUF ndiye namtaka" alisikika akisema
 
Wasifu wa Dakta Bashiru kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

=====

Huyu ndiye Dk Bashiru Ally​

Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala ni uteuzi wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa balozi na katibu mkuu kiongozi.

Ni uteuzi ambao haukutarajiwa uliokwenda sambamba na msomi huyo kuteuliwa kuwa balozi, wengi wanajadili uzoefu wake wakiamini anaweza kuitumikia vyema nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dk Bashiru ulitangazwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na mapema leo Rais John Magufuli amemuapisha kwa mujibu wa katiba ya nchi na kuanza kutumikia upya wadhifa wake huo mpya.

Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.

Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari ya Kilosa mkoani Morogoro alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1990 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo iliyopo Bukoba alikosoma kidato cha tano na sita na kumaliza mwaka 1993.

Mwaka 1997/98 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya kwanza sayansi ya siasa na kumaliza mwaka 2000 ambapo aliunganisha na kusoma shahada ya uzamili aliyomaliza mwaka 2002.

Mwaka 2003 aliajiriwa na taasisi ya Haki Elimu lakini mwaka huohuo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe ambako alifundisha kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kama mhadhiri msaidizi.

Akiwa chuoni hapo aliendelea na kusoma akichukua shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Amewahi kuwa makamu mwenyekiti na kaimu mwenyekiti wa Chama cha kitaaluma cha UDSM (Udasa), makamu Mwenyekiti wa chama cha wanataaluma nchini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei, 2018 Dk Bashiru akiwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa UDSM vilevile alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.

Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.

Chanzo: Mwananchi
Walichua shahada ya uzamili au alisoma?
 
Tujazie time gaps. 1993 alienda JKT kuanzia June hadi December. Alikuwa wapi kuanzia January 1994 hadi alipojiunga UDSM 1997?
 
Jane,
Hata mimi nimeshangaa sana, pia form one aliingia akiwa na umri wa miaka 19! Hii ni kwa mujibu wa "CV- Wasifu" .

Undergraduate umri miaka 30 hivyo ameanza kazi rasmi akiwa na umri miaka 35 ! Kama wasifu usemavyo kama siyo akiwa na umri wa miaka 40 ktk uhalisia. Na hapa ameanzia ngazi ya chini ktk utumishi wa umma chuoni UDSM.
Kuanza shule katika umri wa miaka 12 lilikuwa jambo la kawaida kwa watu wa generation yetu hasa tuliokulia vijijini. Mimi nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 11, na darasani kwetu aliyekuwa mdogo sana alikuwa na miaka 10 na mkubwa sana alikuwa na miaka 14.
Hilo sisi wengine hatushangai, tumeyaishi hayo maisha.
 
Back
Top Bottom