Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Wasifu wa Dakta Bashiru kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

=====

Huyu ndiye Dk Bashiru Ally​

Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala ni uteuzi wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa balozi na katibu mkuu kiongozi.

Ni uteuzi ambao haukutarajiwa uliokwenda sambamba na msomi huyo kuteuliwa kuwa balozi, wengi wanajadili uzoefu wake wakiamini anaweza kuitumikia vyema nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dk Bashiru ulitangazwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na mapema leo Rais John Magufuli amemuapisha kwa mujibu wa katiba ya nchi na kuanza kutumikia upya wadhifa wake huo mpya.

Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.

Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari ya Kilosa mkoani Morogoro alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1990 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo iliyopo Bukoba alikosoma kidato cha tano na sita na kumaliza mwaka 1993.

Mwaka 1997/98 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya kwanza sayansi ya siasa na kumaliza mwaka 2000 ambapo aliunganisha na kusoma shahada ya uzamili aliyomaliza mwaka 2002.

Mwaka 2003 aliajiriwa na taasisi ya Haki Elimu lakini mwaka huohuo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe ambako alifundisha kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kama mhadhiri msaidizi.

Akiwa chuoni hapo aliendelea na kusoma akichukua shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Amewahi kuwa makamu mwenyekiti na kaimu mwenyekiti wa Chama cha kitaaluma cha UDSM (Udasa), makamu Mwenyekiti wa chama cha wanataaluma nchini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei, 2018 Dk Bashiru akiwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa UDSM vilevile alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.

Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.

Chanzo: Mwananchi

Cv ya mwizi wa kura fullstop.
 
Kwanini alichelewa sana kuanza darasa la kwanza? Miaka 12! At this age mimi ndiyo nilikuwa namaliza darasa la 7.

Mfuatilie vizuri utakuta hata hajazaliwa huo mwaka, huo mwaka wa kuzaliwa ni wa kufoji. Nilisikia RIP Ngitiye eti ana miaka 51. Nilipopitia hiyo cv yake ndio nikajua ni umri wa kufoji. Maccm mengi huwa yanapenda sana kufoji.
 
CV yake ndogo mnoo ndiyo maana hata weledi kwake sifuri, exposure pia iko chini sana na hajawai shika nafasi nyeti tofauti na hiyo ya ukatibu mkuu CCM, hapa sasa utumishi wa umma umeingia shimoni rasmi maana yeye na JPM yaleyale...
Exposure ataipata humo humo.
 
Mfuatilie vizuri utakuta hata hajazaliwa huo mwaka, huo mwaka wa kuzaliwa ni wa kufoji. Nilisikia RIP Ngitiye eti ana miaka 51. Nilipopitia hiyo cv yake ndio nikajua ni umri wa kufoji. Maccm mengi huwa yanapenda sana kufoji.
Sasa wanafoji umri ili iweje???.
 
CV yake ndogo mnoo ndiyo maana hata weledi kwake sifuri, exposure pia iko chini sana na hajawai shika nafasi nyeti tofauti na hiyo ya ukatibu mkuu CCM, hapa sasa utumishi wa umma umeingia shimoni rasmi maana yeye na JPM yaleyale...
Aah kumbe,mkuu unaonaje ukituwekea CV zako hatari tukalinganisha na huyu uliye pania kumzodoa?
 
Kwanini alichelewa sana kuanza darasa la kwanza? Miaka 12! At this age mimi ndiyo nilikuwa namaliza darasa la 7.
Miaka ya kabla 1980 shule zilikuwa chache na ziko mbali toka maeneo ya vijijini; enzi hizo ilikuwa kawaida sana mwanafunzi kutembea umbali mrefu sana kwenda shule tena wakipita machakani, kula mara moja kwa siku tena jioni unaporudi shule. Mazingira hayo yalifanya watoto waende shule wakiwa wakubwa ili kuhimili shuruba za shule.
 
Kwa hiyo ameteuliwa pia kuwa Balozi wa nini? /Nchi gani? Mnazidi kupeana tu ulaji huku wahitimu lukuki wakiwa wanahangaika tu mtaani.

Hivi KMK Ni lazima awe Balozi?Sijui huyu Mapadlocks huwa anawaxaga nini! Yaani jitu moja veo lukuki...Haya mafisi ya Lumumba Ni shidaaa!!!!
 
Ina maana hana familia na umri wote huo miaka Zaidi ya 50?!
Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.
 
Ina maana hadi sasa jamaa hana watoto mkuu??
Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.
 
Wasifu wa Dakta Bashiru kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

=====

Huyu ndiye Dk Bashiru Ally​

Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala ni uteuzi wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa balozi na katibu mkuu kiongozi.

Ni uteuzi ambao haukutarajiwa uliokwenda sambamba na msomi huyo kuteuliwa kuwa balozi, wengi wanajadili uzoefu wake wakiamini anaweza kuitumikia vyema nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dk Bashiru ulitangazwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na mapema leo Rais John Magufuli amemuapisha kwa mujibu wa katiba ya nchi na kuanza kutumikia upya wadhifa wake huo mpya.

Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.

Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari ya Kilosa mkoani Morogoro alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1990 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo iliyopo Bukoba alikosoma kidato cha tano na sita na kumaliza mwaka 1993.

Mwaka 1997/98 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya kwanza sayansi ya siasa na kumaliza mwaka 2000 ambapo aliunganisha na kusoma shahada ya uzamili aliyomaliza mwaka 2002.

Mwaka 2003 aliajiriwa na taasisi ya Haki Elimu lakini mwaka huohuo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe ambako alifundisha kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kama mhadhiri msaidizi.

Akiwa chuoni hapo aliendelea na kusoma akichukua shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Amewahi kuwa makamu mwenyekiti na kaimu mwenyekiti wa Chama cha kitaaluma cha UDSM (Udasa), makamu Mwenyekiti wa chama cha wanataaluma nchini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei, 2018 Dk Bashiru akiwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa UDSM vilevile alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.

Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.

Chanzo: Mwananchi
Historia feki kabisa..
Mbona umaskip kua alikua mwalimu wa shule ya msingi?
Mbona umeskip kua ukoo wake wametokea huko kwenye vita...AWRNDA
 
Back
Top Bottom