Wasifu/ CV ya Maalim Seif Sharif Hamad, Historia yake kwa Ufupi

Retizinga

Member
Aug 7, 2016
89
70
151007165933_wasifu_wa_maalimu_seif_sharif_hamad_624x485_bbc_nocredit.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF , Maalim

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF , Maalim Seif Sharif Hamad
Kwa ufupi

Maalim alihudhuria masomo ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya mwaka 1962 -1963.

Historia yake

Maalim Seif Sharif Hamad ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar na pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF. Maalim Seif alizaliwa Oktoba 22, 1943 huko Nyali, Mtambwe katika Wilaya ya Wete iliyoko kisiwani Pemba.

Maalim alihudhuria masomo ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya mwaka 1962 -1963.

Pamoja na kufaulu vizuri sana masomo ya kidato cha sita, Maalim Seif hakwenda chuo kikuu kwa sababu serikali ilimtaka afanye kazi serikalini ili kuziba nafasi za kazi zilizokuwa wazi kutokana na kuondoka kwa wingi kwa Waingereza kurudi nchini kwao. Maalim aliajiriwa kama mwalimu kwa miaka tisa, yaani 1964 – 1972 na alifundisha Sekondari Fidel Castro iliyoko Pemba na Chuo cha Ualimu cha Lumumba kilichoko Unguja.

Mwaka 1972 aliruhusiwa kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusomea shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa, Usimamizi wa Umma na Uhusiano wa Kimataifa, alihitimu shahada hii mwaka 1975 akiwa mmoja wa wanafunzi waliofaulu vizuri sana kiasi kwamba chuo kilipenda abakie kufundisha, jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Maalim Seif alianza kujifunza na hata kuingia katika masuala ya uongozi mkubwa wa serikali mwaka 1975, alipoteuliwa kuwa Msaidizi Binafsi wa Rais wa Zanzibar wakati huo (Aboud Jumbe) ambapo aliifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977. Mwaka 1977 akateuliwa kuwa Waziri wa Elimu wa Zanzibar na akatumika katika nafasi hiyo hadi mwaka 1980.

Mwezi Februari 1984 akateuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar (Cheo sawa na cha Waziri Mkuu wa Tanzania, kimajukumu). Maalim Seif amekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Mwinyi kama Rais wa Zanzibar, na mwaka 1985 alipochaguliwa Rais Idris Abdul Wakil kuongoza Zanzibar, bado Maalim Seif aliteuliwa kuwa Waziri Kiongozi na alishikilia wadhifa huo hadi Januari 1988 alipoondolewa katika baraza la mawaziri na baadaye kufukuzwa ndani ya CCM. Kwa hivyo, Maalim Seif amekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuanzia mwaka 1977-1988.

Tokea Maalim Seif aondolewe katika utumishi wa uongozi wa juu wa Zanzibar (akiwa mwanachama wa CCM), imemchukua miaka zaidi ya 22 ndipo tena amerejea kileleni, sasa akiwa ni Makamu wa Kwanza Rais wa Zainzibar, lakini akitokea Chama Cha Wananchi CUF.

Kisiasa, Maalim Seif amepitia katika nafasi nyingi sana. Mwaka 1977 – 1988 alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM lakini pia mwaka 1977 – 1987 alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM huku mwaka 1982 – 1987 akiteuliwa kuongoza Idara ya Uchumi na Mipango ya Chama cha Mapinduzi (kitaifa).

Maalim Seif na wenzake kadhaa walifukuzwa kutoka Chama Cha Mapinduzi mwaka 1988 baada ya kushindana kimsimamo na CCM na alikuwa mmoja wa waanzilishi wa vuguvugu la “Kamahuru” la Zanzibar lililoungana na CCW (Chama Cha Wananchi) ya Tanzania Bara na kuunda Chama Cha Wananchi CUF ambapo yeye (Maalim Seif) alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa CUF akihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 1999 alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CUF hadi hivi sasa.

Kimataifa, Maalim amewahi kushikilia wadhifa mkubwa sana kimataifa kati ya mwaka 1997 - 2001, alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa “The Unrepresented Nations and Peoples Organization (UNPO)” (Nchi zisizowakilishwa na Mashirika ya Watu) - Tafsiri yangu. Hii ni taasisi ambayo makao makuu yake yapo jijini The Hague nchini Uholanzi na inahusisha mataifa zaidi ya 50 duniani na watu ambao siyo wajumbe wa Umoja wa Mataifa, yaani ambao wakienda Umoja wa Mataifa wanakuwa na hadhi ya waangalizi tu (au wageni). Baadhi ya nchi mwanachama wa umoja huu ni pamoja na Taiwan, Tibet na Zanzibar. Lakini pia amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Vyama vya Kiliberali Duniani kati ya mwaka 2002 – 2003.

Maalim Seif amemuoa Aweina Sinani Masoud tangu mwaka 1977 na wana watoto watatu.

Mbio za ubunge

Maalim Seif si mgeni katika masuala ya uwakilishi na Ubunge. Yeye ni mmoja kati ya Watanzania wachache waliobahatika kupitia nafasi zote za kuwawakilisha wananchi kwa pande zote mbili za muungano.

Mwaka 1977 – 1982 amekuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini pia kati ya mwaka 1977- 1980 na 1984 – 1988 amekuwa ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kwa muktadha huu anafahamu vizuri shughuli za kibunge na kiuwakilishi na amepata kuzishiriki vilivyo.

Mbio za urais

Maalim Seif, “Rais wa Mioyo ya Wazanzibari” ameshiriki katika mbio za urais za Zanzibar mara nne bila mafanikio, lakini zikiwa chaguzi ambazo hata waangalizi wa kimataifa wamekuwa bila kupepesa macho wakisisitiza kuwa zina walakini mkubwa.

Uchaguzi Mkuu wa Kwanza alioshiriki ni ule wa mwaka 1995 akigombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF. Maalim Seif alikosa kuingia ikulu kwa sababu “ilitangazwa” kuwa amepata asilimia 49.76 ya kura zote dhidi ya Rais Salmin Amour “Komandoo” aliyekuwa na asilimia 50.24. Pamoja na CUF kupinga matokeo hayo, pia Waangalizi wa kimataifa walisisitiza kuwa uchaguzi ule ulikuwa “uchafu”.

Mwaka 2000 tena Maalim Seif alitaka kuingia Ikulu lakini haikutokea. Ilitangazwa kuwa amepata asilimia 32.96 ya kura zote dhidi ya asilimia 67.04 za Amani Karume wa CCM. Huu ni uchaguzi ambao pia hata waangalizi wa kimataifa waliutaja kama moja ya chaguzi zisizofuata kabisa misingi ya kidemokrasia huku ukandamizaji wa vyama vya upinzani hususani CUF ukiwa wazi. Kwa mfano, waangalizi wa Jumuiya ya Madola waliutaja uchaguzi huu kama “Shambels” (Msambaratiko) – Tafsiri yangu.

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, Maalim Seif aliangushwa kwa mara nyingine na Rais Amani Karume wa CCM, Safari hii Maalim akitangaziwa kupata asilimia 46.07 dhidi ya 53.18 za Karume. CUF ilikataa matokeo haya na ikatangaza kutomtambua Karume kama Rais wa Zanzibar. Waangalizi wa kimataifa kama Jumuiya ya Madola na Taasisi ya Demokrasia ya Marekani ziliweka wazi kuwa uchaguzi ule haukuwa huru na wa haki, baadhi ya maandiko yanasisitiza kuwa huwenda hii ndiyo sababu iliyofanya Marekani (kama nchi) isitume hata balozi wake au mwakilishi kushuhudia sherehe za kumwapisha Karume (mara ya pili).

Maalim Seif alitupa karata ya nne ya kusaka urais wa Zanzibar mwaka 2010 mara hii akipambana na Dk Ali Mohamed Shein ambapo pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ilitangaza kuwa Dk Shein amemzidi Maalim Seif kwa kura 4471. Ndiyo kusema kuwa Maalim Seif alipata asilimia 49.1 dhidi ya asilimia 50.1 za Shein. Uchaguzi wa mwaka huo pia ulionekana kuwa na kasoro nyingi sana.

Kwa mwaka huu 2015 tayari Maalim Seif Sharif Hamad amekishachukua fomu na kupitishwa na CUF kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi wa mwaka huu n CUF upande wa Zanzibar inaonekana imejipanga sana kushiriki kwenye uchaguzi mwaka huu, huwenda kuliko wakati wowote ule kama alivyowahi kuandika Ismail Jussa, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, kwenye ukurasa wake wa “Facebook”.

Nguvu yake

Kwanza, Maalim Seif ndiye kiongozi mwenye uzoefu mkubwa sana wa kisiasa kati ya viongozi wa upinzani, akianza utumishi wa juu kabisa serikalini alipokuwa kijana mdogo tu na ameendelea hadi kufikia nyadhifa za juu kabisa. Uzoefu wake ni silaha tosha kuwa ukimpa uongozi wa nchi wala hawezi kwenda kuanza kujifunza, tayari anajua wapi aanzie na kwa nini.

Lakini nguvu kubwa na sifa maalum ya Maalim Seif ni kuwa Msimamo thabiti na usioyumba. Kiongozi huyu ana misimamo yake juu ya baadhi ya masuala na ikifika hapo hawezi kuyumba. Mathalani, hivi karibuni amekuwa na msimamo wa dhati wa kudai mamlaka kamili ya Zanzibar, msimamo huu umekuwa ajenda kubwa sana katika siasa za Zanzibar na ni moja ya masuala ambayo. Lakini pia watu waliowahi kufanya naye kazi

Katika siasa ukiwahi kupitia kifungo cha kisiasa, kunyanyaswa moja kwa moja na kuteswa kwa sababu ya msimamo wako kidemokrasia, jambo hili hugeuka na kuwa ushujaa. Maalim Seif alipofukuzwa CCM mwaka 1988 alikaa muda mfupi tu kabla ya kuanza kuwa mfungwa. Alikamatwa mwezi Mei 1989 na kufikishwa mahakamani akishitakiwa kwa kukutwa na nyaraka za siri za serikali (mashtaka ya kupikwa). Alikaa gerezani kwa miaka mitatu (hadi mwaka 1991). Wananchi na marafiki wan chi yetu kimataifa walipoomba sana Maalim Seif na wenzake watolewe gerezani, Rais wa Zanzibar wakati huo, Salmin Amour “Komando”, aliwakebehi hadharani kuwa “wanapaswa kukaa huko huko, hawataoza kwa sababu wao siyo mapapai!”

Lakini pia mwaka 2000 alikamatwa tea na kupewa mashtaka ya kumshambulia askari polisi na kumyang’anya bunduki (kosa la kubambikizia pia). Shitaka hili lilitupwa na mahakama mwaka 2003. Maalim Seif ni mmoja wa viongozi wakubwa sana wa kisiasa hapa Tanzania ambaye amewahi kukaa gerezani muda mrefu sana. Jambo hili ni umadhubutu muhimu kwa mtu anayetaka kuongoza nchi. Kama ameweza kukaa gerezani kwa ajili ya demokrasia na akatoka akaendelea kuipigania, inamjenga katika sifa ya uvumilivu na kutokata tamaa.

Udhaifu wake

Kwanza, Maalim Seif amekuwa na uungwana uliopita kiasi katika mazingira ambayo Zanzibar inahitaji kufanya maamuzi magumu. Uungwana huu kisiasa unaweza kuwa na shida siku za mbele. Hivi karibuni, Mzee anayeheshimika sana Zanzibar na mtu wa karibu na Maalim Seif alitangaza hadharani kuwa mwaka 2010 “yeye Mzee Moyo ndiye alitumwa kwenda kumuomba Maalim Seif ayakubali matokeo ya uchaguzi”. Ndiyo kusema kuwa matokeo yale yalikuwa yamechakachuliwa na ilimpasa Maalim Seif ayakubali ili kuiepusha Zanzibar kuingia kwenye shari. Pamoja na mzee Moyo kurudia kauli hii mara kadhaa, Si Maalim Seif au CUF vimewahi kukanusha.

Kama hiyo hali ni ya kweli basi, tutegemee tena mwaka huu CCM itakuja na mpango huo huo wa kupora ushindi Zanzibar na kutegemea uungwana na huruma ya Maalim Seif. Hakika ifikie wakati Maalim Seif awaachie Wazanzibari wenyewe waamue hatma yao ikiwa wataendelea kufanyiwa ujanja kwenye masanduku ya kura. Uungwana wa namna hii unazika haki za kidemokrasia za wapiga kura na si jambo linalopaswa kujirudia tena na tena kwa kiongozi mkubwa.

Tulipokuwa katika Bunge Maalum la Katiba na nadhani waliokuwa wakifuatilia matangazo ya bunge hilo kupitia kwenye luninga walikuwa wakisikia kwa uwazi kabisa wajumbe wa BMK ambao ni viongozi wakubwa wa CCM kutoka Zanzibar wakitamka waziwazi kuwa hawawezi kuuachia Urais wa Zanzibar kwenye masanduku ya kura. Hii ina maana kuwa CCM itaendelea kupora ushindi wa kidemokrasia wa Wazanzibari kwa kutumia uungwana na busara za Maalim Seif. Jambo hili likiendelea litahesabiwa tena kama udhaifu mkubwa sana.

Nini kimefanya apitishwe

Jambo la kwanza lililofanya CUF impitishe kugombea urais ni kwa sababu yeye ni Mhimili wa siasa za Zanzibar kitaifa na kimataifa. Huwezi kutaja mustakabali wa Zanzibar na Wazanzibari bila kumtaja kiongozi huyu, amehusika katika sehemu kubwa za mabadiliko kadhaa tangu alipokuwa ndani ya CCM na hata alipohamia upinzani. Hali hii nadhani imeivutia CUF na kuona kuna haja ya kuendelea kumpa nafasi.

Lakini sababu ya pili nadhani ni kwa sababu amegombea Urais mara nne zilizopita huku ndiye pekee akionekana bado ana mvuto na ukubalikaji mkubwa zaidi kuliko mwanachama mwingine wa CUF. Hadi sasa CUF haina mgombea mwenye sifa, uwezo, uzoefu na umaarufu au umashuhuri kama wa Maalim Seif. Nadhani chama hicho kimempitisha kikitegemea kwamba yeye peke yake kwa sasa ndiye anaweza kuaminiwa sana na wananchi kiasi cha kuweza kupigiwa kura na kupata ushindi.

Nini kingeweza kumwangusha

Jambo moja ambalo lingemkwamisha Maalim Seif kuwa mgombea urais wa CUF upande wa Zanzibar ni ikiwa yeye mwenyewe angeamua kupumzika au kutogombea. Kwa hali ya kisiasa ya Zanzibar ilivyo “chanya” kwake, sikutegemea kuwa angeliweza kutopitishwa, na labda sana angetokea mwanachama mwingine wa CUF mwenye sifa, uwezo na vigezo kwa upande wa Zanzibar, ambaye hadi sasa sijamuona.

Mpango B kama asingepita

Mipango kama mitatu hivi inaweza kufuatwa na Maalim Seif ikiwa asingepitishwa kugombea urais;

Mpango wa kwanza ni Kuendelea na wadhifa wake wa kiserikali aliona sasa hivi pamoja na kuendelea na uongozi wa CUF ambao unapaswa kukamilika mwaka 2019. CUF bado inamhitaji kiongozi huyu na nadhani bado serikali ya Zanzibar inamhitaji zaidi kiutumishi.

Lakini jambo la pili ni uimarishaji wa maridhiano na utangamano wa Wazanzibari. Ikumbukwe kuwa Maalim Seif ni mmoja wa waasisi wawili wa Maridhiano ya sasa yanayoifanya Zanzibar iwe kwenye utulivu na amani ya sasa. Naamini kuwa angekuwa na jukumu la kujipanga kuanza kusimamia masuala ya utangamano wa Wazanzibari kwa vitendo, ikiwemo kuanzisha taasisi maalumu ambazo zingeendelea kufanya naye kazi kwa lengo la kuimarisha mustakabali wa Zanzibar.

Lakini lingine ambalo nadhani ni ajenda yake ya kudumu ni kupigania Zanzibar yenye mamlaka kamili. Ajenda hii naamini ingeendelea kuwa mikononi mwa Maalim Seif na wanachama wake kwa sababu imekuwa na “mashiko makubwa” na kwa wazanzibari wanaweza kuona kuwa inahitaji kuendelezwa na walioianzisha akiwemo yeye mwenyewe. Namuona akiipigania ajenda hii hata ikiwa atachaguliwa kuingia Ikulu.

Hitimisho

Vijana ambao hawakuwahi kufanya kazi na Maalim Seif wamekosa kujifunza uongozi thabiti kutoka kwa mtu ambaye anajua uongozi unafanywaje. Maalim Seif ni Mwalimu wa Siasa na Uongozi na anajua muda gani afanye nini ili kuendelea kuweka utulivu mahali anapoongoza.

Nakumbuka wakati anatangaza kumtambua tena Rais Karume, vikao vya chama vilitoa baraka za jambo hilo lakini vikiwa na hofu kubwa ya nini kitakachotokea. Maalim Seif aliihimili hali ile, akamtambua Karume, akatengeneza maridhiano na Wazanzibari wakamuelewa. Ni nadra sana kwa dunia ya sasa kupata viongozi wanaokubalika, kuheshimika na kuaminiwa na wafuasi wao, kama ilivyo kwa Maalim Seif.

Maalim Seif si mtu wa mambo makuu sana, mara nyingi utamkuta yumo mitaani kabisa akiwatembelea wagonjwa huku na kule, wazee na watu wasiojiweza. Staili yake ya uongozi ni ya kuamini kuwa watu wa chini wanahitaji msaada na faraja kubwa ya uongozi. Namna anavyosimamia ajenda muhimu ndani ya Zanzibar huku misimamo yake ikiwa wazi ni karata muhimu kwake kuzidi kuaminiwa na huwenda kukabidhiwa dola.

Mimi namtakia kila le heri kiongozi huyu, katika safari yake ya kurejesha hadhi ya Zanzibar na Wazanzibari wote kwa ujumla.

Chanzo: Mwananchi


Mwalimu wa skuli na mtaalamu huyu wa sayansi ya siasa ni mmoja wa wanasiasa waandamizi wa zama za baada ya Mapinduzi ya 1964 anayewania urais wa Zanzibar kwa mara ya tano sasa.

Mwenyekiti na mgombea urais wa chama cha CUF, Seif Shariff Hamad
Hamad, ambaye anajulikana zaidi Visiwani na Bara kama Maalim Seif amekuwa akisiisitiza siku zote kwamba alishinda chaguzi zote tatu ziliopita, lakini Tume ya Uchaguzi Zanzibar ilikataa kuheshimu uamuzi wa wananchi na kuamua kuyaghushi matokeo ili kuwapa ushindi wapinzani wake.
Maaalim aliweka wazi kuwa ijapokuwa zilikuwepo dosari katika uchaguzi wa Jumapili alikubali matokeo na kumpongeza Dk. Shein kw ushindi kwa maslahi ya Zanzibar na watu wake ili kuepusha mfarakano.

Maalim Seif ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimia miaka 67 katika mkutano wa kampeni na kulishwa keki na mke wake, Bi Awena Sinani, wiki mbili ziliopita, anaangaliwa na watu wengi kama ni mtu ambaye ni muwazi sana na kwa ujasiri anasisitiza umuhimu wa kutambuliwa kama nchi na kutaka iwachiwe kutumia rasilmali zake inavyoona ni kwa maslahi ya Wazanzibari bila ya kuingiliwa na Bara ambayo iliungana nayo mwaka 1964 kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msimamo wake usiotetereka wa kutaka pawepo na uwazi kuonyesha mambo mambo gani ya Muungano na masuala gani ni yale ambayo Zanzibar ina mamlaka kamili ya kujiamualia yamempatia marafiki na maadui.

Baadhi ya watu waliopo Bara wana wasi wasi kwamba Maalim Seif ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha CCM mwaka 1987 na moja kwa moja kupoteza wadhifa wake wa Waziri Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar anataka kuudhoofisha Muungano. Lakini kwa Wazanzibari wengi na hasa katika kisiwa cha Pemba ambako anatoka anaonekana ni mzalendo mwenye uchungu na Zanzibar.

Alizaliwa kutokana na familia ya wakulima wa kijiji cha Mtambwe, nje kidogo ya mji wa Wete, Pemba, katika mwaka 1943, Maalim Seif alivuka bahari ya mkondo wa Pemba kuja Zanzibar kuendelea na masomo ya sekondari kutoka 1958 hadi 1963.

Hakuweza kuendelea na masomo ya chuo kikuu pale alipotakiwa aende kusomesha katika shule za sekondari ili kujaza mapengo yaliowachwa na walimu wengi wa Kiingereza na wachache wa kizalendo baada ya Mapinduzi ya 1964. Wakati ule siasa kali za utawala wa mkono wa chuma ulishuhudia serikali ikitaifisha vikataa vidogo vya mashamba na nyumba za makazi za watu walioonekana maadui wa Mapinduzi ziliipelekea Zanzibar kuelezwa na nchi za Magharibi kama Cuba ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, alifanikiwa kuchukua shahada ya kwanza ya Elimu, Sayansi ya Kisiasa na Uhusiano wa Kimataifa´kutoka mwaka 1972 hadi 1975 na aliporudi Zanzibar alichaguliwa msaidizi maalum wa Rais wa Zanzibar mpaka mwaka 1977 alipochaguliwa Waziri wa Elimu.
Katika medani ya siasa Maalim Seif alichaguliwa mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo aliitumikia kwa miaka 11. Katika mwaka 1984 kufuatia kile kilichojulikana kama kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Visiwani kulikoshuhudia kulazimishwa kustaafu kwa aliyekuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe, Maalim Seif alichaguliwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lakini kauli zake za uwazi za mara kwa mara za kuonyesha hafurahishwi na mwenendo mzima wa Muungano na kueleza Zanzibar haitendewi haki kwa baadhi ya mambo ndani ya Mungano kuliepelea kutimuliwa katika chama na pia kupoteza wadhifa wa Waziri Kiongozi kufuatia hatuahio ya chama.
Tokea wakati huo aliandamwa kwa kuonekana tishio la kisiasa na mwaka 1989 alifunguliwa mashitaka bandia ya kupatikana na nyaraka za siri za serikali. Alikaa miaka miwili gerezani, baadhi ya wakati katika chumba akiwa peke yake kwa muda unaoweza kufikia wiki mbili mpaka alipoachiwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa kuwa hakuwa na kesi ya kujibu.

Tanzania ilipofungua milango yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Maalim Seif na baadhi ya wenzake aliofukuzwa nao Halmashauri Kuu ya CCM walikuwa miongoni ma walioanzisha Chama chaWananchi (CUF) na kuwa Makamo Mwenyekiti wake wa kwanza na sasa Katibu Mkuu.

Aligombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, mwaka 2000 na 2005. Alishindwa kwa kura chache, lakini mwenyewe amekuwa akiamini alishinda chaguzi zote hizo na aliporwa ushindi kwa sababu Tanzania na hasa Zanzibar haijakuwa tayari kupokea mfumo wa demokrasia kwa moyo safi.

Mandhari iliopo baada ya uchaguzi wa Jumapili ni tofauti na iliokuwepo katika chaguzi tatu ziliopita ambapo mshindi alichukua kila kitu.
Katika uchaguzi wa safari hii mshindi anatakiwa aunde serikali ya umoja wa kitaifa. Nini kitatokea baada ya Dk Shein kutangazwa mshindi kitatoa mwanga kama Zanzibar itaendelea na hali ya kisiasa ya watu wake kuelewana na kuvumiliana au itarudi katika zama za siasa za chuki na uhasama ambazo zilionekana kuigawa Zanzibar katika mapande mawili, moja linalokiunga mkono chama tawala cha CCM na jengine chama cha upinzani cha CUF.

Mwandishi: Salim Said Salim
 
CV yake ni kiboko wa CCM na mfalisayo Lipumba ukimbipu anakupigia..ana master ya kuwatandika CCM kila uchaguzi ila mwenyekiti wa tume anaweka mpira kwapani
 
..kama ulikua hujui....Maalim Seif jina lake liko kwenye kuta za udsm...akiwa kati ya waliopata GPA za juu kabisa mwaka wake pale udsm...nenda udsm library uliza utaambiwa....kama issue ni elimu yake...hayo mengine ya cv yake wala yanajibiwa na status yake kisiasa tangu ulivyoanza kumjua...
 
Majorty ya wasomi wa kiafrica hawajaelimika. Hivi mtu mwenye cv kubwa kama hii anawezaje kufanya mambo ya kujidhalilisha namna ile kana kwamba hawezi fanya maisha popote zaidi ya uenyekiti?
Anatoa somo gani kwa watu waliokuwa wanamtazama kama role model?
Angetakiwa awe na chuo chake cha kufundisha uchumi East Africa.Kwa nini hawamtumii kufundisha.Something is wrong somewhere.Sio bure hata Havard au Cambridge wasimuite kweli.
 
..kama ulikua hujui....Maalim Seif jina lake liko kwenye kuta za udsm...akiwa kati ya waliopata GPA za juu kabisa mwaka wake pale udsm...nenda udsm library uliza utaambiwa....kama issue ni elimu yake...hayo mengine ya cv yake wala yanajibiwa na status yake kisiasa tangu ulivyoanza kumjua...
Kweli alipita UDSM mwaka 1973, walikuwa drafted group ya watu watano kwenye intake yao walisomeshwa na SMZ chini ya Rais Jumbe , Komandòo akiwa katibu wa Fedha ndio aliekuwa akiidhiinisha malipo ya ada zao.
Maalim Seif, Dr. Ramadhan Mapuri, Juma Duni Haji na wengine wawili majina yamenitoka nikiyakumbuka ntayaleta.
 
duuuh prof ana GPA ya 5 first degree mbona kidizani fulani kama kadata hivi kama vile mpiga jani (mmea)
 
CV yake ni kiboko wa CCM na mfalisayo Lipumba ukimbipu anakupigia..ana master ya kuwatandika CCM kila uchaguzi ila mwenyekiti wa tume anaweka mpira kwapani

Kwa namna hio basi atakuwa na phd ya hekima na busara na wala sio ile phd ya JPM ya hasira!
 
Menu

Skip to content

Maalim Seif Sharif Hamad’s Profile

hakinaumma / November 9, 2008

Mr. Seif Sharif Hamad, popular known as Maalim Seif, was the Presidential candidate in the October 2005 Zanzibar elections and Secretary General of the Civic United Front (CUF) which is the principal opposition party in Zanzibar and Tanzania, and was born at Nyali, Mtambwe in Wete, Pemba (Zanzibar’s sister island) on October 22, 1943. After completing his primary education in 1957 in Pemba he joined King George VI MemorialSecondary School where he attained his Ordinary and Advanced Level Secondary Education in 1961 and 1963 respectively.

Following the January 1964 Revolution, which saw many foreigners and other civil servants leaving the islands, Mr. Hamad was asked by the new government to join the teaching profession to fill the gaps. He taught for eight years at Lumumba Collegeand Fidel Castro Secondary Schoollocated in Unguja and Pemba islands respectively.

In 1972 he was part of the first group of Zanzibari students to be sponsored by the Revolutionary Government of Zanzibar to join the University of Dar es Salaam. He graduated in 1975 with a first class Bachelor of Arts degree (Honors) in Political Science, Public Administration and International Relations.

Mr. Hamad served briefly as a Personal Assistant to the President of Zanzibar, then Mr. Aboud Jumbe (1975 – 1977) before he was appointed Minister of Education, a position he served for three years (1977 – 1980).From 1977 – 1987, he was a member of the National Executive Committee and the Central Committee of the ruling party, Chama Cha Mapinduzi . He became the head of the ruling party’s Economic and Planning Department for five years (1982 – 1987). CCM was then the only political party allowed in Tanzania.

In February 1984, Mr. Hamad was appointed the Chief Minister ofZanzibar by Mr. Ali Hassan Mwinyi who was installed as the new president following Jumbe’s resignation. He retained the same position during the first half of Mr. Idris Abdul Wakil’s presidency before he was dropped in a cabinet reshuffle in January 1988.

Mr. Hamad was finally expelled from the ruling CCM, together with six other colleagues, in May 1988 on allegations that they were rebels within the party.He was imprisoned for 30 months (May 1989 – November 1991) on trumped up charges of organizing an unlawful assembly, which were later changed to that of being found with government classified documents. The case was finally dismissed by the Tanzanian Court of Appeal in January 1993 due to lack of sufficient evidence.

In 1992, when Tanzania amended its constitution to allow multi-party system, Mr. Hamad, together with colleagues, formed a new party, the Civic United Front (CUF) and was elected its first National Vice Chairman. 1n 1999, the CUF National Congress meeting in Dar es Salaam, elected him as the Secretary General of the party, a position he still retains.

In both 1995 and 2000 general elections, Mr. Hamad represented CUF as its presidential candidate forZanzibar. He was robbed of his clear victory during the 1995 presidential elections through manipulation of results by the ruling CCM and the state organs in full collaboration with the Zanzibar Electoral Commission (ZEC).The fiasco repeated itself in 2000 elections that were termed as a shambles by the international observers including the Commonwealth Observer Group, as well as local observers. He then led CUF into dialogue with CCM which culminated with the signing of the popular Accord, the Muafaka, onOctober 10, 2001.

In international arena, from 1997 to 2001 Mr. Seif Sharif Hamad served as the Chairman of the General Assembly of the Unrepresented Nations and Peoples Organization (UNPO) based inThe Hague. UNPO is an organization that comprises of over 50 nations and peoples who are not members of the United Nations Organization including Taiwan, Tibet and Zanzibar. It is has observer status in the United Nations.

Maalim Seif’s Curriculum Vitae

Secretary General, The Civic United Front (CUF) party since 1999
The Civic United Front (CUF), Party Headquarters, Mtendeni Street, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania


Bachelors of Arts (BA Honors) in Political Science, Public Administration and International Relations, University of Dar es Salaam


Born October 22, 1943 Pemba, Tanzania


Residence Zanzibar


Married to Ms. Aweina Sinani Masoud since 1977 with three children

EXPERIENCE AND ACTIVITIES:

Teacher, Lumumba College, Zanzibar and Fidel Castro Secondary School, Pemba 1964-1972Personal Assistant to the President of Zanzibar 1975-1977Member of the National Executive Committee of Chama Cha Mapinduzi (CCM) 1977-1988
Member of the Central Committee of Chama Cha Mapinduzi 1977-1987Director of Economy and Planning of Chama Cha Mapinduzi 1982-1987Member of the Revolutionary Council of Zanzibar 1977-1980 and 1984-1988Member of Parliament of the United Republic of Tanzania 1977-1982Chief Minister of Zanzibar February 1984 – January 1988 and Minister of Education, Zanzibar 1977 – 1980Member of the House of Representatives, Zanzibar 1977 – 1980 and 1984 – 1988

Vice Chairman of The Civic United Front (CUF) party 1992-1999Member of the Defence and Security Committee of The Civic United Front (CUF) since 1999Zanzibar Presidential Candidate on CUF ticket 1995, 2000 and 2005Co-Chairman, CCM/CUF Joint Secretaries General Committee for Resolving Zanzibar Political Crisis 2001-2005Chairman of the General Assembly of Unrepresented Nations and Peoples Organisation (UNPO) 1997-2002Vice Chairman of Liberal International (LI) 2002-2003

Countries Visited: Kenya, Mozambique, Senegal, South Africa, Sultanate of Oman, United Arab Emirates, United Kingdom, France, Germany, The Netherlands, Sweden, Denmark, Finland, Norway, Belgium, Italy, Canada, United States of America

Language proficiency: Swahili, English

Interests: Museums, literature, opera and ballet

Contact Information:maalimseif@hotmail.com
 
Katika siasa (kwani wote ni wanasiasa) Maalim Seif yuko mbali maili nyingi kitaaluma na kiutendaji,wakati Lipumba amesomea uchumi,maalim amesomea na kufaulu kwa kiwango cha juu mno (GPA 4.9) Siasa na Utawala,wakati Lipumba anafundisha uchumi UDSM mwenzake Maalim alikuwa anaitumikia taaluma take ya Siasa na Utawala kuanzia Waziri wa Elimu,MNEC ccm,Waziri Kiongozi na baadae Makamu wa Rais,Wakati Lipumba si mwanzilishi wa mageuzi Bali mkaribishwa,Maalim ni mwanzilishi wa mageuzi,wakati Lipumba akijisifia kulala selo kwa akili ya CUF,mwenzake Maalim alikaa mahabusu kwa miezi 30,Ni kweli kuwa Prof Lipumba ana CV nzuri kwenye uchumi lakini katika siasa Maalim ni habari nyingine
 
Maalim Seif na ndoto yake ya Urais 2020 itatimia akiwa na Chadema?

Baraza la Wazee la Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema limebainisha mipango ya kumshawishi Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)

na Makamu wa kwanza wa zamani wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (2010-2015), Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa mgombea wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 visiwani Zanzibar.

Tamko la Wazee wa Chadema lililotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashimu Issa Juma, limekuja katika kipindi ambacho chama cha CUF kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu mwaka 2015.

Hii ni baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa wake kuelekea uchaguzi mkuu kisha mwaka 2017 kurejea kwenye cheo hicho kinyemela licha ya kueleza kuwa baadhi ya wanachama wamemuomba arudi madarakani.

Kurudi kwa Lipumba ndani ya Cuf kumetengeneza makundi mawili. Kundi la wanaomuunga mkono Profesa huyo na jingine likiwa upande wa Maalim Seif.

Mvutano unaosababishwa na makundi hayo unaonekana kuwa mkubwa. Kuna dalili kkwamba huenda ulichangia baadhi ya viongozi akiwemo Julius Mtatiro akikihama chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalumu waliomuunga mkono Maalim Seif kupoteza ubunge wao.

Nia ya baraza la wazee wa Chadema imetafsiriwa kuwa mbinu ya kuongeza ushawishi wao katika siasa za Visiwani Zanzibar kwa kuwa chama hicho hakina nguvu za kutosha wala kuwa na mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa visiwani humo.

Maalim Seif mwenye miaka 74 alizaliwa Oktoba 22, 1943 kisiwani Pemba na jina lake halisi ni Seif Sharif Hamad. Maisha na shughuli zake ndizo zilichangia aitwe Maalim Seif kwa kuwa alikuwa miongoni mwa watu wanaojihusisha na jamii moja kwa moja.

Swali moja linalotakiwa kujibiwa, Maalim Seif amefika tamati au ni mwanzo wa kutikisa tena siasa za Zanzibar?

Maalim Seif ni miongoni mwa wanasiasa ambao wanasifika kwa misimamo pamoja na mikakati ya kisiasa.

Ni miongoni mwa wanasiasa wanaopendwa visiwani Zanzibar. Tangu akiwa mwanachama wa CCM alikuwa mmoja wa makada wenye ushawishi ndani ya chama visiwani Zanzibar.

Akiwa CCM amewahi kuwa Mjumbe Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Waziri wa Elimu wa visiwa hivyo kati ya mwaka 1977-1980.

Maalim Seif alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kati ya mwaka 1980-1989, pia Mbunge wa Jamhuri ya Tanzania mwaka 1977.

Aidha, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kati ya mwaka 1977 hadi 1987 pamoja na kuwa Mkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango wa CCM kati ya mwaka 1982 hadi 1978. Baadaye alikuwa waziri kiongozi wa Zanzibar kuanzia Februari 6, 1984 hadi Januari 22, 1988.

Hata hivyo mwaka 1988 ulikuwa wa mwisho kwake CCM, baada ya kufukuzwa kutokana na mgogoro wake na maofisa wa chama hicho.

Miongoni mwa rekodi ya kukumbukwa ni kwamba jina la Maalim Seif linaleta sura nyingine ya mgongano mkubwa wa maslahi ndani ya CCM Zanzibar, kati yake na aliyekuwa Rais wa visiwa hivyo Aboud Jumbe.

Taarifa mbalimbali zinamtaja kuwa Maalim Seif ndiye mwanasiasa aliyemdokezea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuhusu azima ya Rais Jumbe kuhoji muundo wa muungano wa Tanzania.

Rais Jumbe pia alichukua uamuzi wa kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Damiani Lubuva na badala yake akataka kumwajiri mwanasheria kutoka Ghana.

Pamoja na kufukuzwa na CCM, bado Maalim Seif alionekana kubaki na nguvu zake za kisiasa hali ambayo iliwasumbua makada wengi wa chama tawala huko Zanzibar.

Haikutegemewa kuwa Seif angepaa kisiasa licha ya kutangazwa si mwanachama wa CCM.

Ikumbukwe wakati akifukuzwa kulikuwa na mfumo wa chama kimoja.

Hivyo basi baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Maalim Seif alikuwa miongoni mwa wanachama walioanzisha chama cha wananchi (CUF) mnamo Mei 28, 1992 na kupata usajili wa kudumu Januari 12, 1993.

Unaweza kutaja majina matano ya wanasiasa wenye nguvu ndani ya Chama cha CUF, ambapo Maalim Seif anakuwa miongoni mwao wakifuatiwa na mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba, Ismail Jussa Ladhu, aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2015, Juma Duni Haji (alitokea Cuf).

Seif ndiye katibu mkuu wa muda mrefu zaidi wa chama cha siasa nchini Tanzania. Tangu kuanzishwa chama hicho kimekuwa chini ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

CUF ilipata usajili wa kudumu mwaka 1993 ikiwa na maana hakijawahi kupata katibu mkuu mwingine hadi hivi pale kilipokumbwa na mgogoro, ambapo upande wa Profesa Lipumba kipo chini ya ukatibu Mkuu wa Mbunge wa Kaliua mkoani Tabora, Magdalena Sakaya.

Seif ameweka rekodi ya aina yake ambayo haijafikiwa na mwanasiasa yeyote nchini. Lakini nini sababu hasa ya Seif kubaki kuwa katibu mkuu wa muda mrefu kiasi hicho? Jawabu la swali hilo ndiyo kuibuka kwa dhana kwamba CUF ni Seif na Seif ni CUF.

Kwamba CUF licha ya kutambulika kama chama cha siasa kinaonekana kuwa mikononi mwa Maalim Seif kuliko mwanasiasa mwingine yeyote Visiwani Zanzibar. Amepitia makatibu wasaidizi kadhaa wakiwemo Julius Mtatiro (Bara), Magdalena Sayaka (Bara), Nasoro Mazrui (Zanzibar) na wengineo.

Je wanachama wa Cuf hawana imani na wanasiasa wengine wenye uwezo wa kuwa katibu mkuu? Kwamba Maalim Seif ndiye mwanasiasa pekee ambaye anaweza kuimudu nafasi hiyo na kukifanya CUF kuwa chama bora? Jibu ni kwamba kutokana na kuongoza kwa muda mrefu katika chama hicho amejikuta akitengeneza athari - chanya au hasi- ambayo hutoa sura ya Cuf ni Maalim Seif au Maalim Seif ni Cuf.

Rekodi ya kugombea urais
Rekodi nyingine iliyowekwa na Maalim Seif ni kuwa mwanasiasa aliyegombea urais mara nyingi zaidi kuliko mwanasiasa mwingine yeyote katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hadi sasa amegombea urais wa Zanzibar mara 5, na iwapo mwaka 2020 atapitishwa itakuwa ni mara ya sita kuwania urais.

Seif alianza kuisaka tiketi ya kuingia Ikulu katika uchaguzi wa mwaka 1995 kupitia chama cha Cuf ambapo alipambana na mgombea wa CCM, Salmin Amour.

Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) matokeo ya urais mwaka 1995, Salmin Amour alishinda kwa asilimia 50.24 dhidi ya 49.76 alizopata Maalim Seif. Hata hivyo Cuf ilitangaza kutoutambua ushindi huo.

Mwaka 2000 Seif aliingia tena ulingoni, na safari hiyo alipambana na Amani Karume mtoto wa rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume.

Kwa mara nyingine matokeo ya ZEC yalionyesha Seif aliangushwa baada ya kujikusanyia asilimia 32.96 ya kura dhidi ya asilimia 67.04 alizopata Amani Karume.

Katika uchaguzi wa mwaka 2000 ulionyesha anguko kubwa sana la Maalim Seif kutokana na kupata asilimia chache (32.96%) tofauti na uchaguzi wa mwaka 1995.

Tofauti hii pekee inaweza kutusaidia kutuzindua mwelekeo wa Maalim Seif kama ni mwanzo wa mtikisiko au mwisho wake kisiasa visiwani Zanzibar na Jamhuri ya Muungano kwa ujumla. Hata hivyo kulikuwa na malalamiko katika uchaguzi huo ambapo baadhi ya waangalizi walisema haukukidhi vigezo vya kidemokrasia kutokana na wagombea kutoka vyama vya upinzani kutishwa na vyombo vya dola.

Aidha, waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola walisema uchaguzi huo ulitawaliwa kwa kile walichokiita 'uchafu mwingi'.

Vidonda vya uchaguzi wa mwaka 2000 vilijitokeza zaidi mwaka 2001 ambapo baadhi ya wafuasi wa Cuf walipoteza maisha baada ya kushambuliwa na vyombo vya dola.

Vurugu zilizotokea Januari 27, 2001 zilichangia kusainiwa makubaliano ya pili ya amani baina ya pande mbili za Cuf na CCM ili kuleta utulivu visiwani Zanzibar.

Uchaguzi wa mwaka 2005 ulivihusisha pia vyama vyote kinzani CCM na CUF. Kwa upande wa CUF walimsimamisha Maalim Seif na Amani Karume akateuliwa na CCM kutetea kiti chake. Mambo yaliyokubaliwa kwenye muafaka wa mwaka 2001 yalifanyiwa marekebisho kwenye uchaguzi wa mwaka 2005.

Uchaguzi huo ulipokamilika, ZEC ilimtangaza Amani Abeid Karume kuwa mshindi baada kujikusanyia asilimia 53.18, huku Seif Hamad akijipatia asilimia 46.07. uchaguzi huo ulionyesha Maalim Seif alipanda kidogo kutoka asilimia 32.96 za mwaka 2000 hadi 46.07% za mwaka 2005.

Hata hivyo waangalizi wa kimataifa kwa mara nyingine walisema kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki.

Wangalizi wa Jumuiya ya Madola walisema palikuwa na kasoro nyingi na uhaba wa uhuru miongoni mwa wapigakura na wagombea. Cuf ilipinga matokeo hayo.

Maalim Seif alirudi tena kwenye mbio za urais mwaka 2010 akiwakilisha chama cha CUF dhidi ya Dk. Ali Mohammed Shein wa CCM. Baada ya uchaguzi wa Oktoba 31, 2010 ZEC ilimtangaza Dk. Shein kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar. Palikuwa na tofauti ndogo ya alama, ambapo Dk. Shein alipata asilimia 50.1 na 49.1 za Seif.

Kutokana na makubaliano ya vyama hivyo kumaliza mgogoro wa muda mrefu visiwani humo, Maalim Seif alitakiwa kuwa sehemu ya serikali ambapo aliteuliwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, huku Balozi Seif Ali Iddi akiwa makamu wa pili wa Rais. Mgawanyo huo wa madaraka ulikuwa na lengo la kuimarisha umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ilifuta uchaguzi mkuu wa Oktoba 30, 2015 na Mwenyekiti wake Jecha Salum Jecha. ZEC ilitangaza pia uchaguzi wa marudio utafanywa Machi 20, mwaka uliofuata.

Licha ya kufutwa uchaguzi huo, Maalim Seif aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mnamo Oktoba, 2015 na kusema yeye ndiye mshindi wa kiti cha urais Zanzibar.

Oktoba 26, mwaka huo Maalim aliviambia vyombo vya habari, "Baada ya kukusanya matokeo yote, nimepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein."

Mosi, mara baada ya uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015 Maalim Seif alifanya mazungumzo na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini Davies Mwamunyange.

Pili, Seif alifanya mazungumzo na rais mstaafu Jakaya Kikwete kabla hajaondoka madarakani. Tatu, Seif alifanya mazungumzo na Dk. Shein. Nne, Seif alifanya mazungumzo na Rais John Magufuli. Mazungumzo yote hayo yalikuwa na lengo la kuleta utulivu visiwani Zanzibar.

Raia hawakuwawahi kuambiwa hadharani mazungumzo hayo yalikuwa na makubaliano ya gani hadi leo zaidi ya 'hisia za wananchi' zilizotamalaki ingawa ajenda kuu ilikuwa ni kuhusu ni 'hali ya Zanzibar'.

Jambo la tano ni uamuzi wa CUF kukataa kushiriki uchaguzi wa marudio na kufuta ndoto zake za kuchukua madaraka ya urais.

Naam, sasa limeibuka suala la kuombwa kujiunga na Chadema, ikiwa na maana kuwa wafuasi wa Chadema na Cuf wanaweza kuungana na kutengeneza nguvu kubwa ya kisiasa visiwani humo na kuwa na mshikamano madhubuti.

Akawania tena, kuna uwezekano wake kushinda?

Atajenga umaarufu wa Chadema visiwani?
Juhudi za Malim Seif katika siasa za Zanzibar si za kubeza hata kidogo. Ni mwanasiasa ambaye ana wafuasi wengi kila kona ya Zanzibar. Hili linafahamika vyema mbele ya wazee, viongozi na wanachama wa Chadema.

Pia Chadema bila shaka wanatamani tena kupata uhondo wa nguvu waliopata kwenye uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 pale Juma Duni Haji alipohamia chama hicho na kuwa mgombea mwenza wa Edward Lowassa.

Ile nguvu ya wafausi wa Cuf inahitajika mno Chadema, hivyo suluhisho ni kumsajili Maalim Seif. Hii ina maana kuwa iwapo Maalim Seif atakihama Cuf, wimbi la wanachama na wafuasi wake watamiminika Chadema.

Ngome ya Maalim Seif huko Kisiwani Pemba itahamia Chadema. Hata hivyo wasiwasi unakuja kutokana na misimamo thabiti ya wafuasi wengi wa Cuf haifahamiki kama wote wataunga mkono mpango wa kwenda Chadema.

Aidha, ukitazama kwa makini mpango wa kuhamia Chadema unaweza kutumika kama mbinu nyingine ya kumjenga Maalim Seif na kupima kuhitajika kwake ndani ya Cuf na siasa za Tanzania kwa ujumla wake.

Pamoja na mambo yote, Maalim Seif bado ni lulu katika ulingo wa kisiasa Zanzibar na Jamhuri ya Tanzania kwa ujumla. Nguvu, umahiri na ushawishi wake vyote vinahitajika kuwa chachu ya kuwaelimisha vijana juu ya siasa za upinzani pamoja na uongozi wa taasisi na nchi.

Muda utaongea.
 
Back
Top Bottom