kiatu kipya
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 3,269
- 1,979
Asante kwa mchango huuTwaha Generali Ulimwengu amezaliwa Tanzania na amesoma Tabora boys na ameshika nyadhifa kadhaa kwenye CCM pamoja na ubunge. Wazazi wake walitokea Rwanda.
Aliandika habari za mke wa Kitine kupelekwa India kutibiwa mafua. Kumbuka Kitine aliwahi kuwa mkurugenzi wa Usalama waTaifa. Kitine alituma vijana wake wakaiba faili la Ulimwengu pale wizara ya mambo ya ndani. Baada ya hapo Ulimwengu akatiwa kashkash. Baadaye Ulimwengu alianza kuishi kwa vibali na kisha kupewa uraia.
PRESS RELEASE
The Ministry of Home Affairs has officially granted Jenerali Twaha Ulimwengu citizenship by naturalisation.
According to the public notice issued by Director of Immigration Services Mr. K.W.B. Kihomano and published March 11, 2004 on Thursday edition of the Daily News, Ulimwengu plus 32 others were given citizenship as empowered upon him under section 9 (1) and 1 (11) of Tanzania Citizenship Act No 6, 1995.
Ni kweli, jamaa sio mtanzania halisi...ila kwakuwa ni kada basi ndo hivyo.Kuna kipindi nilisikia huyu jamaa ni mrundi ila bado sina uhakika maana ccm nawajua kwa fix
Hili la maofisini limenigusa kabisa.....daaa sisi ngozi nyeusi sisi.......Mungu anatuonaWatz tunachukiana sana, umaskini umedhoofisha kufikiri kwetu. Hata maofisini hizi roho mbaya zipo. Mtu amesoma lakini kuona kwake ni mufilisi kabisa
Nimekuelewa mkuuTwaha Ulimwenge ni bidha adimu,na itachukua kalne mmoja kupata mtu sampuli hii.Hataki quick fix,ila anataka binadamu ajitambue kabla ya kufungua mdomo auganishe ubongo wake kwaza,mimi siyo Mark Antony ila ujumbe umefika.
Nimekuuliza wewe... kwanini nisome humu humu wakati nafahamu kila mmoja atakuwa na jibu lake?Ukisoma vizuri humu humu utapata majibu ya swali lako. Soma kwa ufasaha usiruke na kudharau post ya Member yoyote na utapata majibu.
Mtanzania halisi ana sifa zipi?!Ni kweli, jamaa sio mtanzania halisi...ila kwakuwa ni kada basi ndo hivyo.
Uzalendo ni nini bandugu? Au inategemea umelalia upande gani?Siyo Mzalendo yule. Ni mnafiki kama Zitto. Ana hasira na visasi sababu nchi yake ya asili karibu raia wake wote ni watu wa visasi vya kudumu tena wengine wanarithishwa.
Kweli mkuu,au hawajui historia ya wabantu,sema nimesahau tu but wenyeji wa asili kabisa wa hapa tz ni kabila moja au mawili tu,wengine wote wakuja.Mkuu na wewe umeamua kuongopa? Jenerali alinyang'anywa uraia lakini baadaye akaomba na kupewa.
Sababu za kunyang'anywa nina imani unazijua. Jenerali ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
Mtu yeyote ambaye wakati Tanganyika inapata uhuru alikuwa ndani ya Jamhuri, ni raia.
Jenerali amezaliwa Tanganyika. Kama suala ni kuwa ana asili ya Nchi jirani, basi mamilioni ya Watanzania si raia.
Twaha Ulimwengu anayo haki kuwa RAIA wa Tanzania kwa kuzaliwa ( right to citizenship by birth) haki ambayo mi na we tunayo. Ingawa ilidaiwa kuwa wazazi wake hawakuwa na asili ya Tanzania, bado hilo haliwezi kumnyima haki ya uraia wa Tanzania. Hata hivyo taarifa ilikuja kubainika kuwa Ulimwengu alikuwa anahold uraia wa nchi nyingine kama sikosei ni Rwnda au Burundi ambako ndiko ilikuwa asili ya wazazi wake. Jambo hilo kwa sheria za Tanzania lilimnyima haki ya kuendelea kuwa RAIA wa Tanzania, pamoja na kwamba alikuwa na haki hiyo kwa kuzaliwa(right by birth). Jambo hill lilimhitaji Ulimwengu kuukana uraia wa nchi nyingine na kuomba upya uraia wa Tanzania. Kutokana na misimamo yake ya kuikosoa serikali hapo ndipo wabaya wake serikalini wakashikilia kwa kumzungusha kupata haki ya kuwa RAIA wa Tanzania, hata kutaka aondolewe nchini. Ilibidi kukata vibali vya muda na baada ya wadau kuukosoa sana msimamo wa serikali ndipo baadae maombi yake yalipokubaliwa. So he is legally a citizen of Tanzania right now as we speakMkuu acha kutoa mapovu. Mimi sijasema kuhusu ushiriki wake ama mabaya yake ila nasema kwa kinywa kipana kwamba si Mtanzania. Naweza kuwa nina reservations lakini sijasema. Kitu ninachoweza kusema ni kwamba wakati wa mauaji ya 1994 kule Rwanda, Wanyarwanda wengi waliokuwa Tanzania walishiriki kwa njia moja ama nyingine.
Ila nafahamu kwamba Kabila aliponyakua madaraka kule Zaïre akishirikiana ana akina Bizima Karaha (Banyamulenge), Generali na Prof. Wamba dia Wamba walikuwa watu wa kwanza kwanza kufika kule.
Ni mrundi sio mtanzaniaNingependa kujua cv ya Jenerali Ulimwengu kwani nimefurahia uzalendo aliouonyesha kuwa pale mahakamani katika kesi ya katiba.
Kitaaluma nilikuwa namtambua Jenerali kama mwandishi sio mwanasheria. nasikia pia alishakuwa mwakilishi wa Tanzania makao makuu ya umoja wa vijana huko Algeria, pia ni mmoja wa vijana waliolelewa na umoja wa vijana wa Tanu na ni muumini mkubwa wa sera za mwalimu nyerere ya siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Kalne=Karne.Twaha Ulimwenge ni bidha adimu,na itachukua kalne mmoja kupata mtu sampuli hii.Hataki quick fix,ila anataka binadamu ajitambue kabla ya kufungua mdomo auganishe ubongo wake kwaza,mimi siyo Mark Antony ila ujumbe umefika.
Kwa ufupi Jenerali Ulimwengu ni mmoja ya watu makini kupata kutokea nchi hii kama sio dunia hii. Nina heshma kubwa kwa nguli huyu. Na mpaka sasa hajawahi kuniangusha.Ni Mnyarwanda na alinyang'anywa uraia wa Tanzania yeye na akina Balozi Bandora, Castico, nk. Nadhani hakurudishiwa na kwa sasa anafanya kazi kama mgeni.
Ni mwandishi wa Habari na pia miaka kama mitatu nyuma alitunukiwa u advocate. Amewahi kuwa TYL na akawa mwakilishi wa Tanzania kule Algiers. Amewahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati ule wa kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa. Wakati vyama vingi vinaanzishwa kulikuwa na sheria kwamba ukitaka kufanya maandamano ama mikutano unaomba kibali kwa mkuu wa wilaya. Basi huyu bwana alikuwa hana hiyana ya kutoa vibali kwa vyama. Akahamishwa kupelekwa Singida kama mkuu wa Wilaya. Kama sijasahu hakwenda Singida badala yake akajiuzulu ukuu wa Wilaya.
Huyo ndiye Generali Twaha Ulimwengu.
Kama nyie zilivyo fupi kama njia ya chooni unavyoona hii nchi isingekuwa na upinzani ingekuwaje? Jiulize ndio uandike humu.Chadema akili zenu fupi sana yaani mtu hata akiwa zuzu mtamwagia sifa zote ilimradi akija upande wenu,tatizo hata hamjiulizi kwa nini kaja kwetu mlivyo mazuzu
Je, una uhakika gani kama aliyeandika hii comment ni chadema? Generali ulimwengu hawezi kufahamika kwa kizazi cha sasa cha mwendo kasi. Watu tuliokuwa vijana wa TYL miaka ya sitini na sabini tunamjua saana. Muulize mzee Kikwete, waulize wana Tanu wote na jinsi vijana kama Ulimwengu walivyoiletea sifa nchi hii? Mtu zuzu asingeteuliwa kuwa Mwakilishi wa nchi nje hasa enzi hizo ambazo hazikuangalia umetoka familia gani na una nini. Tufanye research sisi tuliokuwa vijana wa TYL from sixtees na nyinyi mnajifanya wana CCM sasa nani ana uchungu wa nchi?Chadema akili zenu fupi sana yaani mtu hata akiwa zuzu mtamwagia sifa zote ilimradi akija upande wenu,tatizo hata hamjiulizi kwa nini kaja kwetu mlivyo mazuzu
Tunaomba utoe background ya vizazi vyako vitano vilipotokea hapa mtandaoni na kabila lako ndo tukujue wewe mtanzania. Yawezekana wewe ni indigenous lakini huna faida kwa mtu yeyote lakini mtu ambaye babu zake walitokea mbali lakini wakafaidisha taifa. Jamal, Waziri wa kwanza wa Afya walikuwa wenye asili ya wapi na Je, Mwalimu unajua vizazi vyake asili yake? Think before you jot.Mrundi , mrundi rundi
Wape elimu hawa makaburu uchwaraUmeacha mambo ya msingi sana kuhusu Jenerali; ama kwa makusudi au kwa kutofahamu historia yake vizuri!!!
Kwamba, pamoja na Unyarwanda wa Jenerali/Twaha Ulimwengu (Twaha Ulimwengu or Jenerali Uimwengu) ambao ulioneshwa na serikali ya Mkapa lakini Mzee Khalfani Ulimwengu; Baba mzazi wa Jenerali/Twaha Khalfani Ulimwengu alikuwa ni mmoja wa watu walioheshimika sana miaka ya 1940's huko Mkoa wa Ziwa Magharibi; nchini Tanganyika!!!!!
Likewise, huyu Jenerali/Twaha Khalfani Ulimwengu, nae alizaliwa Tanganyika hii hii huko Ngara na kusoma Tanganyika hii hii ambapo, eilimu yake ya awali aliipatia Kamachumu na middle school Katoke tangu miaka hiyoooo... hata kabla ya uhuru!!!
Hata elimu ya sekondari, aliipatia Tanzania hii hii huko Nyakato na Tabora Boys kabla hajaenda JKT na hatimae UDSM!!
Lakini pamoja na yote hayo, miaka 54 baadae ndipo serikali ya Mkapa ikamuona eti sio Mtanzania!!!!!
Bado nina kumbukumbu ya Makala ya mwisho kabla Ulimwengu hajapigwa ban!!! Heading ya makala ile ilisomeka: Akina Jefferson na Magazeti!!
Kwamba, hapo kabla Rais Jefferson wa Marekani alijifanya ni mpenzi kweli kweli wa magazeti kwa sababu tu walikuwa wanamwandika vizuri! Lakini magazeti yale yale yalipoanza kuandika mabaya ya serikali ya Jefferson, Rais Jefferson akageuka kuwa mbogo na mkali kweli kweli dhidi ya magazeti!!!
Hivi ndivyo Mkapa alikuwa!! Mwanzoni alijifanya ni rafiki wa media jambo ambalo watu halikuwashangaza kwa sababu nae alipata kupitia huko hapo kabla! Lakini media zilipoanza kuandika maovu ya serikali ya Mkapa; Ben akageuka kuwa mbogo.... AKINA JEFFERSON NA MAGAZETI!!
Tuambie basi visasi na chuki zake angalau kdg.Siyo Mzalendo yule. Ni mnafiki kama Zitto. Ana hasira na visasi sababu nchi yake ya asili karibu raia wake wote ni watu wa visasi vya kudumu tena wengine wanarithishwa.
Duh! Nadhani hata mimi sio mzaledo,maana hao unawaita wanafiki mimi kwangu ndio wazalendo wa kweli.Siyo Mzalendo yule. Ni mnafiki kama Zitto. Ana hasira na visasi sababu nchi yake ya asili karibu raia wake wote ni watu wa visasi vya kudumu tena wengine wanarithishwa.
Mtanzania halisi ni nani? Ukitaka ujue kama ni Mtz au sio tofautiana na wakubwa utaona. Sheria za nchi zinasema mtu yeyote aliyezaliwa Tanganyika kabla ya Uhuru na alikuwepo nchini Tanganyika siku ya Uhuru ni Mtz. Mr. Mo yule kwao ni India, hata rangi inasema, kwa nini hakujavuliwa uraia, Wenje, nadhani mnafahamu alipogombea, alivuliwa uraia. Watz tunachukiana kwa sababu za kisiasa. Not good at all, tubadilikeNi kweli, jamaa sio mtanzania halisi...ila kwakuwa ni kada basi ndo hivyo.