Wasichana watekwa na Boko Haram

Wasichana watekwa na Boko Haram

Status
Not open for further replies.

Jerick06

Member
Joined
May 2, 2014
Posts
51
Reaction score
15
Huko Nigeria Wasichana 234 wametekwa , 46 wamefanikiwa kutoroka, lakini 188 mpaka sasa awajulikani walipo. Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau kupitia video amesema wasichana wawili wameshafariki kutokana na kugongwa na nyoka.

Madai ya Boko Haram ni kupingwa kwa elimu kwa mtoto wa kike, wakisema mtoto wa kike atakiwi kujua kusma wala kuandika bali ni kukaa nyumban kwaajili ya kujifunza malezi peke yake.

HASHTAG nyingi katika mitandao ya kijamii za kulitaka kundi ilo kurejesha watoto hao wa kike zikisema #BRINGBACKOURGIRLS
Sambaza neno ili kwaajili ya Wasichana hao na kupinga ukatili.
 
This is old news. Habari ya mujini kwa sasa ni mlipuko wa bomu kwa mara nyingine huko Abuja (kitongoji cha Nyanya) juzi usiku!
 
Lakini naona alipewi kipaumbele kama ilivyo habari za Malaysian Airway na habar za NBA katika vyombo vingi vikubwa vya habari, sasa sijui ni kuwadharau waafrika au kutowapa kipaumbele wanawake wa kiafrika. inauma sana.
 
Lakini naona alipewi kipaumbele kama ilivyo habari za Malaysian Airway na habar za NBA katika vyombo vingi vikubwa vya habari, sasa sijui ni kuwadharau waafrika au kutowapa kipaumbele wanawake wa kiafrika. inauma sana.
Tatizo hata wanaijeria wenyewe hawalipi suala hilo kipaumbele. Sasa wasitegemee jamaa wengine kufanya hivyo.
 
Ni wiki ya pili sasa tangu wanamgambo wa Boko haram wavamie shule na kutoweka na wanafunzi wa kike zaidi ya 223. Mpaka sasa haijulikani kama wanafunzi hao wako hai au laa. Sasa swala kujiuliza: Ile ndege ya malaysia ilipotoweka ikiwa na abiria zaidi ya 200 tuliona dunia nzima ime react, ikijitolea kwa hali na mali,na sasa wamehamua kuitafuta kwa mwaka mmoja http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/05/140502_malaysia_ndege_mwaka.shtml. Lakini kwa hili tukio la Nigeria hatuoni hata kama tukio limetiliwa umuhimu katika vyombo vya habari. Humu duniani inaonekana kuna double standard. Mimi nilitegemea vyombo vya kipelelezi na majeshi kadhaa wangeisha kwenda Nigeria ili kuweka nguvu katika kuokoa hao watoto. Huko waliko haijulikana kama kweli wanapewa chakula maana ni wengi kuwalisha katika maficho, au wameuawa na kuzikwa kwenye kaburi la pamoja, haijulikana. Very sad
 
hao wanafunzi ni wazungu hadi watafutwe na madege makubwa?
 
Sidhani kama Nigeria wameomba kusaidiwa kwa mambo yao ya ndani.
 
wafia dini hutawaona kwny uzi huu.

al sisi ua nyonga wote magaidi.

al asad ua wote magaidi wanaojifanya waasi.

boko haram ni symbol ya uislam wa ukweli. pumb.f sana.
 
Rai yangu kwa Jonathani kuomba Msaada kwa Mashirika ya Usalama nje ya Nigeria ili kutokomeza hiki kikundi.
 
Waafrika wengine mkisaidiwa mnasema mnaingiliwa mambo yenu ya ndani, mkiachiwa mfanye mambo yenu wenyewe mnalalamika dunia haiwajali.

Huwezi kulinganisha tukio la kupotea ndege lililotokea kwa kupitia anga na bahari za kimataifa na kubeba watu wa mataifa tofauti na kitendo cha watoto wa Nigeria waliotekwa Nigeria.
 
Umeanzisha maswali; Lakini kwa ujumla kuna mambo mengi ya msingi yanayohitaji kufanyiwa kazi ili dunia nzima pawe ni mahali salama pa kuishi. Jiulize hizo silaha na mabomu ya Boko haramu yanatoka wapi na kwa faida ya nani? "Miafrika ndivyo tulivyo".
 
Ni wiki ya pili sasa tangu wanamgambo wa Boko haram wavamie shule na kutoweka na wanafunzi wa kike zaidi ya 223. Mpaka sasa haijulikani kama wanafunzi hao wako hai au laa. Sasa swala kujiuliza: Ile ndege ya malaysia ilipotoweka ikiwa na abiria zaidi ya 200 tuliona dunia nzima ime react, ikijitolea kwa hali na mali,na sasa wamehamua kuitafuta kwa mwaka mmoja Mwaka 1 kuitafuta ndege ya Malaysia - BBC Swahili - Habari. Lakini kwa hili tukio la Nigeria hatuoni hata kama tukio limetiliwa umuhimu katika vyombo vya habari. Humu duniani inaonekana kuna double standard. Mimi nilitegemea vyombo vya kipelelezi na majeshi kadhaa wangeisha kwenda Nigeria ili kuweka nguvu katika kuokoa hao watoto. Huko waliko haijulikana kama kweli wanapewa chakula maana ni wengi kuwalisha katika maficho, au wameuawa na kuzikwa kwenye kaburi la pamoja, haijulikana. Very sad

CIA ndio boko haram na kamwe hutasikia mission zao zikikwama mpaka mafuta yaishe! Wanaifanya serikali kuwa bussy kupambana na hicho kikundi halafu wao wanachota mafuta. Ndio maana huko nigeria wamebatizwa jina la boko CIA haram. Wanafanya watakavyo jiulize nguvu na siraha wanazipata wapi
 
Waafrika wengine mkisaidiwa mnasema mnaingiliwa mambo yenu ya ndani, mkiachiwa mfanye mambo yenu wenyewe mnalalamika dunia haiwajali.

Huwezi kulinganisha tukio la kupotea ndege lililotokea kwa kupitia anga na bahari za kimataifa na kubeba watu wa mataifa tofauti na kitendo cha watoto wa Nigeria waliotekwa Nigeria.

Evidence? inategemea ni msaada wa mambo yapi
 
Binafsi nadhani hizi fujo za Nigeria zimekaa kisiasa zaidi kuliko kidini. Yaani wanafunzi zaidi ya 200 wachukiliwe na kuvushwa mpaka hadi huko walipo, na serikali imekaa kimyaa! Halafu nchi yenyewe sio a failed state. Tunaongelea Nigeria, a country with the largest military machine in West Africa. Yaani haingii akili ni Hata kidogo. Hao Boko Haramu wana nguvu gani Hata kuweza kushambulia maeneo nyeti watakavyo?
 
Evidence? inategemea ni msaada wa mambo yapi

Evidence soma post ya mtoa mada halafu linganisha na falsafa nzima ya Boko Haram.

Boko Haram hawataki Nigeria waingiliwe na utamaduni wa magharibi.

Maana yake watu wengine, hususan wa magharibi kuingia hapo ni ku complicate issue, kwa sababu watachochea sentiments za kwamba Nigeria inaendeshwa kwa remote control.

Halafu bado kuna Waafrika wanalialia kwamba dunia haiwajali.

Dunia haiwajali wakati Nigeria ni nchi influential hapo West Africa imechangia wanajeshi kuliko nchi yoyote ECOMOG mpaka vita Liberia vimeisha. Ina influence kubwa sana ECCOMOG/ ECOWAS.

Tatizo hapa si dunia kutojali, tatizo ni uongozi wa Nigeria kutojali.

Tangu wanafunzi watekwe hata huyo rais Jonathan hajatoa statement.

What does that say about his commitment and political will to pursue these animals?

Waafrika imefikia wakati sasa tuweze kutatua matatizo matatizo yetu wenyewe na kuacha kulialia kuhusu kusaidiwa na dunia.
 
Umenikumbusha stori za genocide ya rwanda. UN ilijikakamua kupeleka majeshi na kuwithdraw. Ukiangalia movie ya hotel rwanda inasikitisha jinsi ambavyo order ya kuondoka ilivyopokelewa.

but who said the world is fair. Sillyiddiotic africans abusing and killing their fellow africans for stupidiest excuses!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom