Wasichana wa siku hizi..na kutafuta elimu.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasichana wa siku hizi..na kutafuta elimu..........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Feb 7, 2012.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Zamani saana nilikuwa natazama sana filam za kihindi.....
  filam hizi zilikuwa na mambo meengi mno yanayofanana na maisha yetu ya kitanzania
  na mafunzo tele....

  sasa kuna filam moja naikumbuka kila siku......
  askari mmoja akiwa katika katika pita pita zake mitaani
  alisikia kelele za mwizi mwizii...akageuka akaona kijana anakimbia mbio...

  akaanza kumkimbiza huku akimwambia yule kijana kusimama...kijana hakusimama...
  akampiga risasi bahati mbaya ikamua yule kijana pale pale...
  askari alikwenda kuona ni nini yule kijana alichoiba akakuta kijana kumbe ameiba chapati....

  akajisikia vibaya mno na hasira saana...,mwisho akajua kuwa yule kijana ana mama yake mzee
  ambae ndo alikuwa anamtegemea yule kijana...akazidi kujisikia vibaya mno...

  mwisho akanunua kama chapati kumi akaenda kumpelekea yule mama wa yule kijana
  na kumuomba msamaha kwa kumuua kijana wake kwa wizi wa chapati.....

  yule mama aliongea kitu ambacho sijasahu ile filam mpaka leo...
  akasema akimwambia yule askari...usijisikie vibaya...kwa yaliyotokea....wewe umefanya kazi yako
  yeye angekuwa ananipenda na kunisikiliza mama yake asingekwenda kuiba...
  wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo wala mkubwa.....wote tunapaswa kuwa raia wema........
  wewe huna ulilokosea.....yeye alikuwa mwizi na yaliyomkuta ni sahihi kwa mwizi yeyote..
  angenipenda kweli mama yake angekwenda kutafuta kazi akapata kipato cha jasho lake..
  na sio kuiba......sijaisahau hiyo filam mpaka leo....

  sasa siku hizi kwa watanzania weengi kumezuka mbio za kutafuta elimu by any means neccessary..
  kwa wasichana wako tayari kujiuza eti ili wapate elimu...
  kutembea na walimu au wakuu wa vyuo imekuwa kawaida mradi tu wapate hiyo elimu...
  sasa swali ni hili hiyo elimu ina faida kweli kama umeipata kwa njia chafu?????

  nini maana ya elimu kama haiwezi kukuonesha ubaya wa unachokifanya?????????
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Faida ipo. . . ikiwa atajifunza kitu kweli maana hamna atakapoandikwa aliipata vipi useme waajiri wakiona CV yake watamnyima kazi.

  Tatizo ni kama atajiskia amani au la, kama ataweza kuendelea huko mbele kwa juhudi binafsi au kila mara atataka urahisi.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  nadhani tatizo linaanzia nyumbani
  wazazi tunawarithisha nini watoto wetu?

  Values tunazowafundisha
  ndizo zitakazowasimamia wakiwa wanafanya maamuzi yao
  popote waendako
   
 4. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Wanatafuta vyeti tu hao na sio ELIMU
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  umekuwa jimama now?
  faida zipi?
  ni sawa na kusema ujambazi una faida
  is it?
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Hiyo movie inaitwaje? Kasam Paida Karne Wake Ki?

  Nikirudi kwenye mada, huenda wapo ambao watakataa ila ni kweli wapo wadada wa elimu ya juu wanaojiuza ili wapate elimu. Sasa sijui wanajiuza ili wapate hela za ada au sijui wengine wanajiuza kwa walimu wa kiume ili wapate kufaulishwa mitihani....wao wadada wahusika ndiyo wanajua sababu za wao kufanya hivyo.

  Binafsi nimeshashuhudia kabisa wadada wa UDSM wakijiuza kwenye mabaa ya Sinza na Savei/ Mlalakuwa. Kwa kweli wanasikitisha na kutia huruma. Lakini kwa vile wanafanya hivyo kwa utashi wao basi sidhani kama wanastahili hata kuhurumiwa.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  hii mentality ya the end justify the means imeingia majumbani naona...
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Heheheeee umekuwa Jimama tena?
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  naomba kuuliza
  hivi ni kitu gani chenye thamani kwa mwanadamu
  kuliko mwili wake mwenyewe?

  Kama utatumia mwili wako
  kwa ajili ya kupata kipato
  unadhani ni kitu gani utakachoshindwa kutumia kupata utakacho

  mfano, kama uliuza mwili kako for monea
  nategemea waweza uza hata roho za wengine kwa pesa?

   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwani we mshahara wako una faida gani?Unakulipia kodi, unakulisha na unakuvisha. Wa jambazi nao una uwezo wakufanya mambo hayo hayo . .
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehehehe. . . you like?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Una mambo wewe!!!
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  nimeisahau jina
  lakini Amitabh Bachan ndo alikuwa stariing
  na alikuwa jambazi...huyo askari ni mdogo wake ambae alikuja kumuua mwisho kaka yake...
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lol... Una vituko wewe!
   
 15. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Nilishawahi kuwatembelea marafiki zangu katika chuo 'X' , niliyoyakuta ilikua ni karaha ,
  badala ya kuwaza wasome vipi ili wafauli pepa yao , wao wako busy na mipango kabambe ya kucheat ,
  to be honest , matokeo mengi ya vyuoni ya sasa ya ulakini mkubwa :A S embarassed:
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ofu kozi

  unajua kuna vitu vingine unajifunza kwenu bila hata kujua unajifunza kitu
  mfano, baba ni womanizer
  hata watoto hii dhambi watairithi bila wao kujua ndani ya nafsi zao

  au baba anauza roho za wengine kupata mafanikio
  ina a way mtoto anarithi
  maisha yakim-push hard
  anauza roho ya mwingine
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  huwezi ita faida..
  kazi sio mshahara tu...
  kazi ina faida nyingi ikiwemo heshima mbele ya jamii

  so huwezi sema kazi faida yake ni mshahara....
   
 18. m

  mitishamba JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila ulichonacho umekipata kwa njia halali?
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Thamani ya mwili wa mtu ni relative as well as subjective. Kuna namna ambayo wewe unaona ukiutumia mwili wako utakua umeushushia thamani, na mtu mwingine akaona kitu hicho hicho hakipunguzi chochote.

  Swala la watu kutoa ngono ili apewe sijui majibu na nini sifagilii. . ila kumpangia mtu asiyenihusu chakufanya na mwili wake pia sifagilii vile vile kwasababu sielewi akili yake inavyofanya kazi ama kinachomsukuma kufanya hivyo. . na hapa wale dada poa wanahusu sana.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hiyo heshima unayoitaka sio kila mtu anaihitaji kwahiyo usitegemee kila anaefanya kazi anafanya kwa sababu kama zako wewe. Hivyo hivyo hizo faida nyingine. . . kwasababu tu ni muhimu kwako haina maana ni muhimu kwangu pia. Unatakiwa uelewe kwamba binadamu tunatofautiana kwanzia sura mpaka malengo na hisia. . .
   
Loading...