Wageni hawazuiliwi kuwepo nchini kikazi, lakini kwa kazi za namna hii sheria za nchi zinazingatiwa kweli??? Wana vibali vya kazi ?? Usalama wa nchi ni kazi ya kila mwananchi, unaweza ajiri mmalawi mshamba tu kumbe wewe ndio mshamba maana anaweza akawa secret agentHusika na kichwa hapo juu.
Kama mjuavyo kazi za ndani imekuwa ni ajira kwa baadhi ya wasichana.
Tena imefika mbali zaidi kumekuwa na makampuni ambayo yanawafundisha vizuri namna kufanya kazi kwa ufanisi na kuwapatia ajira.
Tena wanakuwa wanalipwa mishahara ambayo inaweza kuwasaidia.
Sasa hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasichana wa kazi za ndani wa Kimalawi hapa Tanzania.
Ukienda kwa watu wanaotafutia kazi wasichana wa ndani utakuta wadada wa kazi wa Kimalawi wameenea.
Ukija kwenye salon nyingi utakuta wadada wa salon ni wa kimalawi.
Hata baa mtaani naona wamejaa hawa mabinti wa kimalawi.
Ukikaa na kina mama kwenye vikoba na jumuiya wanawasifia sana wadada wa kazi wa Kimalawi.
Sasa nauliza nini sababu ya wasichana wa kitanzania kupoteza sifa za kazi?
Je, hawa mabinti wa Malawi wana nini cha ziada?
Tuwajibike sote kulinda nchi yetu