Wasichana wa JF ambao hamjaolewa

Duh! I thread kuna watu imewagusa sana!!!

Ukiolewa au kuoa mara ya pili - things will never be the same!!! Kubali au kataa ukweli ndiyo huo...

Watafiti wa mambo ya mahusiano wanaandika hivi "...Kama mwanaume au mwanamke aliyeacha/aliyachwa angepewa nafasi ya kumrudia mwezi wake baada ya muda, asilimia 95% wangefanya hivyo..."

Walio wengi huwa wanapata kuishi kwa taabu katika mahusiano ya pili - it is more or less of "sogea tuishi"!

tatizo hapa inakuwa ni fear of the unknown!binadamu ni wagumu kukubali na kukabiliana na mabadiliko!!alieachika bado anaweza kuonyesha upendo mkubwa tu atakapoweza kupata second chance!!!!
 
mmh shostito apo kuna mawili mama
1.kuna aliyeachana na mkewe kwa sababu za msingi kabisa
2.kuna walioachana na wake zao kwa ugume gume wao....
cha msing siyo kukupuruka ....mkae vkao na umdadis kwakina ndo utajua nin kilimsibu kinyume na hapo imekula kwako
km vile kuna wanawake mashetani...i do blv umesoma boardng skul hasa za wasichana tupu yan kuna bnadamu wengne wana tabia ngumu sana huwez ishi nae ,awez ishi na mtu she z so dfcult so hard ni mbish kwa kila kona yeye yupo kivyake tu na idea zake iki ni kisu lakin anaweza sema i ni sufuria...kuna tabia mbalimbali mpk mnasema mmh uyu atakaye kuwa mume wake atakuwa na tabu....alikadhalika na wanaume the same...ni mbishi tu mwanzo mwsho iz ol abt him thats ol....so km ikitokea umemuoa uyo na badaye ukashndwa nae apo mi ntaelewa....kuna bnadamu wengne si wakuish nao.

Asi-generalise kiasi hicho. Yapasa aangalie waliachana ktk mazingira gani, ushauri huo wa Dena Amsi ni upotoshaji mkubwa.
 
Habari zenu wote.

Katika pita pita zangu nimekutana na mambo mengi ambayo yamekuwa yakinishangaza sana. Katika wanaume 25 walioachana na wake zao (niliowafanyia uchunguzi) hawawi na mapenzi tena. Kama kuna msichana humu akikutana na mwanaume kama huyu namshauri akae mbali nae kabisa na uweze kujiuliza maswali yafuatayo:
1. Kwanini aliachana na huyo mkewe??
2. Wewe unakipi kipya hasa ambacho utamfanya asikuache kama huyo mwingine??
3. Kakufuata wewe kwa sababu gani??? (Pesa, uzuri, nk)
4. Alikuwa anatafuta pa kupumzika then ale kona lakini ukambana akashindwa kuchomoka
5. Endeleza na sababu zako nyingine nyingiiiiiiiiiii

NB: Usikubali kuolewa na mwanaume alieacha mkewe wa ndoa kamwe!!!!!!!!!!!!!!!11

Usipotoshe watu ndugu yangu. mimi nimeacha mke na nikaoa miaka miwili sasa, tuna mtoto na tunaishi kwa raha mstarehe japo ilikuwa ndoa ya kikatoliki. Mzee malecela ameoa mke aliyeachika, mbona wanaishi vizuri tu. Mke wangu mimi ilikuwa mkikwaruzana tu anajifungia ndani. uwe ulikuwa nje huingii tena ndani hadi uite majirani au ndugu zake. kama mpo ndani atakimbia kufunga milango na yeye kujifungia chumbani. nje huwezi kutoka na chumbani huingii. Wanawake aina hiyo hata kumi nitawaacha
 
Labda tu nikupe kisa hiki kisha nikuulize swali ndugu mtoa mada,
Kuna jamaa alitoka kazini amechelewa kutokana na wingi wa kazi zake,na akaamua jioni hiyo ampe lifti sekretari wake kisha naye arejee nyumbani,kumbe mke wake sababu ya wivu alikuwa amechukua gari nyingine na kumfuata mumewe ili ajue nyendo zake,na akashuhudia mume wake akiingia kwenye gari na sekretari wake,kwa hasira na wivu yule mke akaingia kwenye gari akarudi nyumbani.Haukupita muda mrefu yule jamaa naye akaingia ndani akiwa amechoka,kajaribu kumsalimia mkewe kanyamaziwa,kaomba ugali akajibiwa kale hukohuko kwa hao unaowapa lifti.Jamaa hakutaka maneno wala majibizano kwa kuwa alikuwa haelewi mkewe anamaanisha nini.Akamuagiza msichana wa kazi amletee ugali,basi kabla hata msichana hajaufikisha ule ugali mke akauchukua na kumpiga nao(ugali) kwa hasira mumewe.Mume naye hasira zikamshika na hapohapo akaandika talaka.

SWALI:Sasa kwa kesi kama hii na nyingine zinazofanana bado utamhukumu mwanaume huyo kwa sheria zako kwamba kwa kuwa ameachana na mkewe basi asioe tena?

Dena hujanijibu bado hilo swali hapo juu........
 
Usipotoshe watu ndugu yangu. mimi nimeacha mke na nikaoa miaka miwili sasa, tuna mtoto na tunaishi kwa raha mstarehe japo ilikuwa ndoa ya kikatoliki. Mzee malecela ameoa mke aliyeachika, mbona wanaishi vizuri tu. Mke wangu mimi ilikuwa mkikwaruzana tu anajifungia ndani. uwe ulikuwa nje huingii tena ndani hadi uite majirani au ndugu zake. kama mpo ndani atakimbia kufunga milango na yeye kujifungia chumbani. nje huwezi kutoka na chumbani huingii. Wanawake aina hiyo hata kumi nitawaacha
Halafu nimegundua wanawake wanapenda wanaume waliooa na kuacha
 
Usipotoshe watu ndugu yangu. mimi nimeacha mke na nikaoa miaka miwili sasa, tuna mtoto na tunaishi kwa raha mstarehe japo ilikuwa ndoa ya kikatoliki. Mzee malecela ameoa mke aliyeachika, mbona wanaishi vizuri tu. Mke wangu mimi ilikuwa mkikwaruzana tu anajifungia ndani. uwe ulikuwa nje huingii tena ndani hadi uite majirani au ndugu zake. kama mpo ndani atakimbia kufunga milango na yeye kujifungia chumbani. nje huwezi kutoka na chumbani huingii. Wanawake aina hiyo hata kumi nitawaacha

Sijampoteza mtu utakaloambiwa changanya na zako hujui hilo?? Kwani wewe uko kama upepo kila unachoambiwa unafata bila kupima je ufanye au usifanye???
 
PM Hapa si kwamba mwanaume kamuacha mwanamke ni mwanamke ndo amesababisha na anajua sababu kumbuka kule mwanzo nilieleza kwanini alimuacha?? unakumbuka lakini???

Hivi DA, ukiambiwa uchague uwe mpango wa nje wa mtu au uolewe na mwanaume aliemwacha mkewe wa kwanza, JE WEWE UTACHAGUA NINI?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom