Washauri wa Rais wote waliokuwa kwenye press comference, kongamano, bungeni na kwengineko waliokuwa wanatoa kauli mbali mbali kuhusiana na kikokotoleo kipya wanapaswa kujiuzulu mara moja. sababu
Kiungwana na kwa roho safi wajiuzulu nafasi zao za ushauri kwa Mh. Rais badala yake wafanye kazi zingine za kuijenga nchi.
Call Me Jay.
- Hawakumshirikisha ipasavyo Rais kuhusu kikokotoleo ndio maana leo kabatilisha maamuzi yao
- Hawakuwa wakweli kwa Rais ndio maana imemlazimu Rais kuwaita shirikisho la wafanyakazi kuwasikiliza na kisha kufanya maamumuzi aliyoyafanya
- Katika hali ya kawaida maamuzi ya RAIS yanapingana na msimamo wao waliokuwa nao hivyo kupaswa kumeza matapishi yao, hivyo ni muda muafaka kuwapa wengine nafasi wamsaidie Rais
- Wameonyesha kupwaya kwenye nafasi zao hadi Rais kufanya mjia mmbadala ambayo wao wangekuwa wamefanya kabla (kukutana na shirikisho la vyama vya wafanyakazi) wangekuwa wamepata suluhisho kabla ya Rais kuingilia.
Kiungwana na kwa roho safi wajiuzulu nafasi zao za ushauri kwa Mh. Rais badala yake wafanye kazi zingine za kuijenga nchi.
Call Me Jay.