Mkuu mi nadhani ni Elimu na uwezo wao wa kufikiri, lakini na mara nyingi ni hawa wanaoimba nyimbo za kulialia na mapenzi. Ila kwa wale wa hip hop ya ukweli na iliyosimama huwakuti wakifanya hivyo kwa sababu wanaupeo mkubwa wa kufikiri, mfano Fid Q, Mwana FA, n.k.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa Bongo fleva na Bongo Movie kushabikia CCM,tumeona wengi tena wale maarufu wakijitokeza waziwazi kwenye shughuli za CCM.Jambo la kujiuliza hivi ni kweli hawa wasanii wana mapenzi ya dhati na chama hiki au ni ubinafsi wao,au kwa kuwa wengi wao wana elimu ndogo hivyo kushindwa kuelewa matatizo makubwa yaliyosababishwa na CCM?
Weweeee chama tawala kinalipa vizuri hakina longo longo...ukiingia kwenye system usafiri wa uhakika kwenda kuburudisha na unatumia muda mfupi...sasa wewe upandishwe kwenye gari kwenda kwenye shoo kigoma......wapi na wapi
sasa mbona ume comment?Ngoja nisicomment chochote juu ya hawa wanaojiita wasanii lakini kwa akili ya kawaida ni kwamba wameamua kuwajoin Wasanii wenzao