Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,163
- 5,766
Bado kuna tatizo kubwa la ujinga Tanzania. Mojawapo ni hili la kutotambua nini maana ya demokrasia na mfumo wa vyama vingi. Unapohoji eti kwa nini wasanii wanashabikia CCM wakati unatambua wazi kuwa nchi hii kila mtu yupo huru kushabikia chama akipendacho unathibitisha dalili ya ujinga uliotukuka kichwani mwako. Kila mtu ana mtazamo na maono tofauti katika maisha yake, wewe kama unaiona CCM ni mbaya, wapo wanaiona CCM ni nzuri kama vile imeazishwa jana. Wewe unapoiona Chadema ni nzuri jua kuwa wapo wanaoina ni mbaya kuliko hata ukimwi. Ni vile namna kila mtu anavyoishi na maisha yake. Maisha hayana kanuni kwamba kila mtu lazima afuate. Vivyo hivyo hata kwenye siasa hamuwezi wote kuwa na mawazo sawa na mitazamo inayofanana.