MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Hii taarifa imenaswa mahali kua kuna kundi kubwa la wasanii muda si mrefu wataungana na msaani mwenzao Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA, kundi hilo linadaiwa kua na wasanii maarufu nchini hasa wale wanachama wa CCM kujumuisha bongo moviez na Mziki. Ni wale ambao kwa kiasi kikubwa walishiriki kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2015.
Sababu kuu ya wao kufikia maamuzi hayo kutoridhishwa na jinsi ambao wenzao wanaadhibiwa kwa tuhuma za kujihudisha na Madawa ya kulevya bila ya kua na ushahidi tena kwa kuwadhalilisha hadharani bila kufuata taratibu za kisheria. Sababu nyingine wamedai kutelekezwa na chama chao mama ambacho walikipa nguvu kwa kiasi kikubwa wakati wa kampeni na hata wengine kutotimiziwa madeni yao hivyo hawaoni faida kuendelea kubaki mahali pasipo na shukrani.
KWAANINI CHADEMA WAWE MAKINI?
Inasemekana kua ndani ya kundi hilo kuna wale wasanii ambao walituhumiwa kulipwa tshs million 2 kila mmoja ili kunogesha ile press ya kijana mpambanaji wa Madawa ya kulevya, swali la kujiuliza kama kweli walilipwa mil 2 kila moja, je wameshavuta halafu wanasepa au kuna mchezo unachezwa ili kufumba hilo suala la mgao wa pesa hizo kuepuka kumtia mtu aibu juu ya uhalisia wake na nia yake ya kupambana na madawa?
Hivyo hilo suala CHADEMA katika kuwapokea wageni wawe makini sana, isijekua ni mafuriko ya msimu tu.