Tetesi: Wasanii wengi kumfuata Wema Sepetu, CHADEMA kuweni makini

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Hii taarifa imenaswa mahali kua kuna kundi kubwa la wasanii muda si mrefu wataungana na msaani mwenzao Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA, kundi hilo linadaiwa kua na wasanii maarufu nchini hasa wale wanachama wa CCM kujumuisha bongo moviez na Mziki. Ni wale ambao kwa kiasi kikubwa walishiriki kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2015.


Sababu kuu ya wao kufikia maamuzi hayo kutoridhishwa na jinsi ambao wenzao wanaadhibiwa kwa tuhuma za kujihudisha na Madawa ya kulevya bila ya kua na ushahidi tena kwa kuwadhalilisha hadharani bila kufuata taratibu za kisheria. Sababu nyingine wamedai kutelekezwa na chama chao mama ambacho walikipa nguvu kwa kiasi kikubwa wakati wa kampeni na hata wengine kutotimiziwa madeni yao hivyo hawaoni faida kuendelea kubaki mahali pasipo na shukrani.

KWAANINI CHADEMA WAWE MAKINI?

Inasemekana kua ndani ya kundi hilo kuna wale wasanii ambao walituhumiwa kulipwa tshs million 2 kila mmoja ili kunogesha ile press ya kijana mpambanaji wa Madawa ya kulevya, swali la kujiuliza kama kweli walilipwa mil 2 kila moja, je wameshavuta halafu wanasepa au kuna mchezo unachezwa ili kufumba hilo suala la mgao wa pesa hizo kuepuka kumtia mtu aibu juu ya uhalisia wake na nia yake ya kupambana na madawa?

Hivyo hilo suala CHADEMA katika kuwapokea wageni wawe makini sana, isijekua ni mafuriko ya msimu tu.
 
alie weka thamani sawa ya kura kwa watanzania alikosea sana.

haiwezekani bendera fata upepo, mtu asiye na uwezo wa kufikiria kura yake kuwa na thamani sawa na anayefikiria.

hao wasanii ni bendera fata upepo (kama ni kweli) maana hawajui nini kinawapeleka huko zaidi ya kumfata wema
 
alie weka thamani sawa ya kura kwa watanzania alikosea sana.

haiwezekani bendera fata upepo, mtu asiye na uwezo wa kufikiria kura yake kuwa na thamani sawa na anayefikiria.

hao wasanii ni bendera fata upepo (kama ni kweli) maana hawajui nini kinawapeleka huko zaidi ya kumfata wema
Ndio maana marekani kuna electoral college
 
miaka ya nyuma, wasomi kadhaa kujiunga CHADEMA.
Sababu ya kujiunga ina maana sana kuliko kujiunga kwenyewe
 
Haina haja ya kuwapa Alarm Chadema mana kama mtu kaja kwa njaa au lengo baya atarudi kwa staili ya mgongo mgongo kama mwenzao Wolper ila kadi zao watapokelewa kama wanazo
 
Suala la kupokea 2m liko wazi halina ubishi.
Daudi anachofanya ni kuuwa makundi mengine ya wauza unga ili kundi lake lipasue anga bila mpinzani.

GSM,
semaaa " Daresalaaam"

Connect Rinda.
 
Ngoja waweke kodi kwenye matamasha yao watarudi wenyewe waganga njaa hao wanaleta siasa za upepo wala hatuwataki upinzani
 
AKUFAAE KWA DHIKI NDO RAFIKI.MUONE JINSI ATAKAVYOSAIDIWA KESI YAKE NA LISSU MTABAKI MIDOMO WAZI.WEMA BORA UMETAMBUA MAPEMA KULEEEE HAKUNA WA KUKUFUTA MACHOZI
 
Hawajui kupokea pokea watu kuna maana ipi,endeleen kupokea pokeen sana mtapokea na wasiopokelewa
 
Mmh, me nashangaa sana mnavoshupalia swala la wema kuhama ccm, wamihama wangap waliokuwa mpaka na vyeo vyao ccm na ccm bado iko ngangar mpaka leo! Itakuwa wema ambae hajawah kuwa hata mjumbe wa nyumba kum? Kaamuulizen kingunge atawaambia
 
Tukifikiria chanzo cha yote haya ni ishu ya ngada.kwann asihame siku zote mpaka baada ya kuhusishwa na ishu hizo?nina wasiwasi na hili japo tunaendeleza ushabiki wa kisiasa hata kwenye mambo ya msingi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom