Wasanii wasusia Kampeni ya Uzalendo kwanza

Nihan

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
16,682
2,000
Viongozi wa taasisi ya Uzalendo Kwanza wameamua kujiweka pembeni kwa kile walichodai kwamba hawamuelewi mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.


Chanzo makini kililieleza kuwa viongozi wote akiwemo aliyekuwa makamu mwenyekiti, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wengine kama Halima Yahya ‘Davina’, Salom Urassa ‘Thea’, Sabrina Rupia ‘Cathy’ waliamua kujiweka pembeni kwa kile wanachodai kuwa Steve Nyerere anajinufaisha mwenyewe kwani anafanya mambo kibao bila kuwashirikisha.

Viongozi hao ambao walikiri kujiweka pembeni kwa sababu hawamwelewi Steve na kudai kuwa ili wasije kugombana wameamua kujiengua mapema wafanye mambo yao mengine ingawa haki zao zipo palepale kwani ndiyo waanzilishi. Kwa upande wa Steve alipoulizwa kuhusiana na hilo alijibu kwa ufupi ‘hakuna kitu kama hicho’.
 

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,446
2,000
Nikimuona Steve huwa nacheka tuu.
Nikikumbuka ile saga yake na mama wema na namna alivyokuja kuomba msamaha mbele ya waandishi wa habari, mpk kulia machozi naona bongo hamna msanii na mzee wa kuchungulia fursa km Steve Mengere, huyu jamaa ni njaa hatari.
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,075
2,000
Haka kajamaa na ufupi wake nashangaa kwanini mara zote ndiko kanakuwa kanawaongoza wenzake
 

kasulamkombe

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
2,234
2,000
kafupi kama mav na kichwani kumejaa maji nashangaa sijui wanakubalije kuongozwa na haka kapilitoni
 

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,797
2,000
Mi napata shida sana Kumtofautisha na Polepole, hawajulikani ni Wazee ama Vijana
Halafu ngozi yake amekarithisha wanawe..alipost selfie na mwanae nikajua mbabu gani..mtoto mdogo ana sura nzito kama uji Wa magimbi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom