Wasanii wa Tanzania ongezeni ubunifu

Wasanii wa Tanzania ongezeni ubunifu

NUMBER 10

Senior Member
Joined
Aug 4, 2021
Posts
103
Reaction score
170
Habari wakuu.

Nimetoka youtube kusikiliza mziki kwa wasanii tofauti wa kitanzania. Kusema la ukweli kuna kichefuchefu cha kutosha huko kwa aina ya muziki unaozalishwa na wasanii wetu.

Takribani wasanii 70% kwa sasa wanaiga mapigo ya miziki wa nje hususan Afrika Kusini. Kwa sasa Afrika Kusini kuna Amapiano. Huu mziki ni mwepesi mnnoo na hauna ladha hasa ua miziki basi tuu ni vufurgu na kuruka ruka.

Haipendezi kwa wasanii na waandaji wa mapigo ya muziki kuwaiga wa Afrika kusini ilhali tuna chetu tena kizuri kupindukia. Wimbo kama ule wa marioo ME AMOUR ukisikiliza unapata ladha na raha masikioni kwa mchanganyiko wa ala zinazopigwa, nampongeza sana mzalishaji wa muziki ule, heko yake.

Ila huyu Mario ana kigeugeu ingawa ni muandishi mzuri na anabuni maudhui mazuri sana. Ispokuwa saa zenfine ni hana utwuzi mzuri wa mirindimo mpaka kifika kuiga vitu vibovu. Nimetoka kusikiliza wimbo wake mwengine wa DEAR X. Huu wimbo siupendi kweli shida tupu ni mingurumo tuuu na mirindimo ya wasouth ndio unasikia.

Niseme kweli kuna kinanda kimepigwa mule kina ladha safi ila zile souti za amapiano zimenichafua vibaya vya kutosha. Hivi kweli mzalishaji ameahindwa kuleta ubunifi wa aina nzuri ya mapigo ya muziki hadi akalazimika kuweka ushuzi ule.

Wasanii hawajiulizi kwa nini wasanii wa nchi jirani inakuwa ngumu kuiga aina ya mziki wetu hata kama wanataka, ni vile kwasababu mziki wetu una ufundi mwingi mnooo si rahisi kwa watu wepesi kuiga ladha zetu inataka mtu mkomavu ndio aweze kupiga ala kama zile za katika Mi Amour.


Naomba wasanii tumieni chetu hadi tuweke alama yetu duniani kuwa hiki ni cha TZ na sio Nigeria ama kenya.

Lala unono
Ala mziki.
 
Back
Top Bottom