Wasanii wa bongofleva mmeishiwa pumzi?

GadoTz

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
370
636
Nina muda mrefu sana sijasikia wimbo ukanisisimua toka kwenu wasanii wa bongofleva.

Nyimbo karibu zote za sasa naishia kuzipenda baada ya kuzizoea zikishapigwa mara nyingi lakini haziingii mpaka damuni.

Kimewakuta nini wasanii wa bongofleva? Mmeishiwa tungo? Au ndio muziki wa biashara kama wenyewe mnavyouita!?

Naskiza wimbo wa Young D BBM naskia chorus tupu. Eti ndio swag .

Namskiza hasara roho ya Darasa naskia part two ya Muziki .

Uko Wcb naona kama wameamua wote kuimbia kwenye beat moja na melody moja.

Kiba na remix ya aje isiyo na kigeni.

THT ndio ata sielewi wanafanya nini siku hizi.

Izzo business na yule demu wake wamejaribu kuwa Navy Kenzo lakini muziki wao unaumiza masikio .

Navykenzo wao wameamua kutuletea album kabisa ya autotunes.

Jide ata sijui album yake anauzia wimbo upi.

Uko kwa wana hiphop ndio balaa weusi hawana jipya, young kilaa ndio dah mpaka ukiniuliza kama bongo bado kuna hiphop sijui cha kujibu. Ukiona msanii kama Nay anatrend kwenye hiphop ujue hiphop inakufa sio inabaniwa maana sijaona wimbo mkali wa hiphop ukabaniwa.

Yani muziki kiufupi umepoteza dira sio hiphop sio waimbaji. Leo tunasikilizishwa kina Hamorapa sababu hakuna tena ubunifu kwenye muziki.

Uko kwenye mastudio kunani? Tafuteni ata waandishi basi.

Hivi wasanii mnalalamika hakuna show kwa nyimbo zipi za kujaza watu ukumbin?

Mbona Darasa alikuwa bize na shows pamoja na usawa huu huu wa Magu!

Nani kawadanganya raia bado wanashangaa video za drone na magari ya kuazima.

Watu wanataka muziki mzuri. Bring back bongofleva yetu.
 
Uchambuzi mzuri sana mkuu, yaani album/ diwani ya Navykenzo dah wimbo baada ya wimbo ni autotunes tu na mfanano wa melodies, inabidi wa jipange tu
 
uone wabongo wanavyojua kuwaponza wasanii wao,apa watakuambia toa zako tuzisikie
ilihali mwana akitoa boko hiyo mijineno yao sasa
inamfanya msanii mpaka anaenda zimua akili na ngada
 
Hivi wakuu izzo business na yule dem ni mtu na mtu wake au ni kakundi ka biashara .??
 
Nina muda mrefu sana sijasikia wimbo ukanisisimua toka kwenu wasanii wa bongofleva.

Nyimbo karibu zote za sasa naishia kuzipenda baada ya kuzizoea zikishapigwa mara nyingi lakini haziingii mpaka damuni.

Kimewakuta nini wasanii wa bongofleva? Mmeishiwa tungo? Au ndio muziki wa biashara kama wenyewe mnavyouita!?

Naskiza wimbo wa Young D BBM naskia chorus tupu. Eti ndio swag .

Namskiza hasara roho ya Darasa naskia part two ya Muziki .

Uko Wcb naona kama wameamua wote kuimbia kwenye beat moja na melody moja.

Kiba na remix ya aje isiyo na kigeni.

THT ndio ata sielewi wanafanya nini siku hizi.

Izzo business na yule demu wake wamejaribu kuwa Navy Kenzo lakini muziki wao unaumiza masikio .

Navykenzo wao wameamua kutuletea album kabisa ya autotunes.

Jide ata sijui album yake anauzia wimbo upi.

Uko kwa wana hiphop ndio balaa weusi hawana jipya, young kilaa ndio dah mpaka ukiniuliza kama bongo bado kuna hiphop sijui cha kujibu. Ukiona msanii kama Nay anatrend kwenye hiphop ujue hiphop inakufa sio inabaniwa maana sijaona wimbo mkali wa hiphop ukabaniwa.

Yani muziki kiufupi umepoteza dira sio hiphop sio waimbaji. Leo tunasikilizishwa kina Hamorapa sababu hakuna tena ubunifu kwenye muziki.

Uko kwenye mastudio kunani? Tafuteni ata waandishi basi.

Hivi wasanii mnalalamika hakuna show kwa nyimbo zipi za kujaza watu ukumbin?

Mbona Darasa alikuwa bize na shows pamoja na usawa huu huu wa Magu!

Nani kawadanganya raia bado wanashangaa video za drone na magari ya kuazima.

Watu wanataka muziki mzuri. Bring back bongofleva yetu.
Turudi kwa za kale, vijana jazz band, Marquis etc!
 
Skuhiz,kuna mzk au n mnanda tu wanaimba

Bora hata ukamskilize khadja kopa akupashe jins ya kuish
Na mkeo wa kizaramo

Presha ya kuusogeza muziki kwenye uso wa kimataifa unawafanya wasanii wakose ubunifu wanakomaa na budget kubwa ya video lakini hawana muda wa kuandika kabisa kitu kinachoeleweka na mashabiki pia tumechangia kuuporomosha muziki kwenye uandishi na sauti kwa kua tumewapandisha wasanii wetu kwenye idadi ya viewers kwenye digital platform hakuna anaejalia kuhusu audio tena.
Ingawa wapo ambao wamebaki kwenye misingi ya utunzi na sauti ambao hawapati nafasi ya kupenya kwenye soko,siku hizi ninapakua ngoma mpya leo baada ya siku 3 naifuta baada ya kugundua siwezi kuisikiliza au kuangalia tena bado namiliki joints za miaka ileeeeeee kwenye device zangu.
 
POINT

Mfano mzuri ni Diamond.

Sikiliza na angalia utofauti wa wimbo wa Nitarejea, Moyo wangu au Kamwambie zilikuwa na mafunzo na ladha nzuri, leo anahangaika na hizi za kimataifa kama Kokoro ndio zinamharibia.

Ukitaka kujua hilo...pitia comments za viewers wake wa East Africa nzima wanavyolalamika.
 
Mziki biashara mkuu sasa kama kokoro ndo zina mpa show ughaibuni unategemea nn ???? Zama za nitarejea nenda kamwambie zimeshapita ....
 
Ila kiukweli nyimbo za sasa zinawahi kukinai sijui ata kwanini!
Nahreel hata kama na yeye ni producer kwanini ile album hao baadhi ya nyimbo zingepita kwa maproducer wengine?
Angalau kupata radha tofauti.....
 
Back
Top Bottom