Wasanii wa Bongo movie, wasikilizeni wateja

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Amelisema hilo Assumption Nalitolela wa gazeti la Mwananchi Jumapili, Jan 31, 2016. Anaongeza kwamba "Uwezo wa kuigiza iwe vichekesho, filamu na tamthilia ndiyo unaofanya mtu anunue kazi ya msanii'.

Anabainisha kwamba:
1) Maidhui ya hii fani ya usanii haifanyiwi utafiti wa kina wa nini watazamaji walengwa (km watanzania) wanataka kukiona na siyo wanachokitaka watayarishaji.
2) Kazi za hawa waandaaji haziwawezeshi wasanii kufanywa kazi zao kufuata matakwa ya watazamaji/wasikilizaji wao bali ya waandaaji.
3) Hadithi/maudhui ya hizo filamu ni za kawaida mno zilizo jaa uzungu, badala ya visa hasilia vyenye mikakati ya msisimko.
4) Viwango vya waigizaji ni vya chini ya kiwango cha kawaida cha kubeba uhalisia wa mtu anayeigizwa.
5) Maneno ya kiingereza yanayowekwa kama tafsiri fupi ni ya kiingereza kibovu na hovyo.

Waandaaji na wasanii wa bongo " muvi"
CHAMBUA CHUNGUZA AMUA CHUKUA HATUA
 
Back
Top Bottom