Nilufer
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 9,863
- 14,349
jamani wanajamvi mimi natatizwa sana na wasanii wengi kutoa nyimbo za maombelezi muda mfupi tu baada ya vifo. hivi huwa wanakuwa wameshatunga halafu wanasubiri wakisikia kifo 2 wanaingiza jina au. hivi inakuwaje kwa kifo cha ghafla kama cha ngwea tayari kuna nyimbo tatu mpya? hizi nyimbo nimezikia leo clauds fm katika kipindi ch leo tena, yaani hata masaaa 24 yalikuwa hayajatimia tayari watu wameshatunga nyimbo, kurekodi studio na kupeleka redioni. sasa nimejiuliza ni kwamba wameguswa na msiba? au ni fursa ya kutoka kimuziki. Nawasilisha.