.wasanii na kampeni arumeru,chungeni yasiwakute kama ze-comedy

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Ni mara nyingi tumeshuhudia wasanii mbalimbali nchini,wakitumika kwenye uhamasishaji
majukwaani kama njia mojawapo ya kuwavutia wapiga kura katika mikutano ya kampeni, hii imekuwa ni mtindo wa vyama karibu vyote vya siasa nchini.
Lakini niseme wazi kuwa mtindo huu umeasisiwa na CCM,hapo awali wakiwatumia zaidi TOT chini ya kiongozi wao mahiri John komba..na baadae iolisambaa na kuwa kwa wasanii wengi zaidi kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Tumekuwa mara kadhaa tukiwaona wasanii kadhaa (ukiliacha kundi la TOT ambao hupewa ruzuku na ccm) wengi wao husahaulika na chama husika mara tu baada ya uchaguzi kuisha bila shukurani zozote ,za kuuenzi mchango wanaokuwa wameutoa katika majukwaa kuusaka ushindi wa chama husika.
Lakini pia hata malipo yao huishia kudhulumiwa na kuwaacha wakisota bila kujua pa kuanzia kwani huwa wametumia muda wao mwingi wakizunguka huku na kule katika kampeni hizo.kama hiyo haitoshi.pia mara zingine wasanii hujikuta wamekimbiwa na washabiki kwa kiasi kikubwa endapo inatokea kwamba walitumika kumnadi mgombea au chama ambacho jamii haina mahusiano mema nacho,au kimechafuka mbele ya jamii kwa tuhuma mbalimbali.na hivyo kupoteza imani na mvuto mbele ya jamii.

Kwa msanii makini yeyote ambaye mungu amekujalia baraka na kipaji,na uko juu kisanii kwa sasa.nina kushauri kwamba endapo umepewa mwaliko wa kushiriki kampeni kwa sasa.kabla hujaukubali ni vema ukatafakari kwamba nini kitaendelea kwako baada ya uchaguzi huo .na usifurahie tu ule mkusanyiko utakaokutana nao kwa kipindi hicho.
Ni vema ukaelewa wewe kama msanii,una washabiki wengi ambao hawafungamani na itikadi moja kisiasa.kwa hiyo unaweza kuwafurahisha wengi na pia kuwaudhi wengi pia.uelewe jambo hilo lina gharama zake kwako..

Tunawaona ze-comedy jinsi wanavyohangaikia kupewa mkataba mpya pale TBC,jambo ambalo bila shaka limewaacha njia panda kimaisha yao kisanii.mbali na hao kuna wengi pia wamepotea kwenye ramani ya sanaa baada ya kutumika kisiasa.
Kama mnakuja Arumeru kufaidi fweza za mafisadi basi nawashauri muwaombe wawape na kiinua mgongo kabisa,kwani huenda ikawa ndio safari yenu ya kuelekea kustaafu sanaa ikawa imeanzia hapo!
Naomba kuwakilisha humu JF.
.
 
Back
Top Bottom