Wasanii hawa wamepewa onyo kutoka Bungeni

Jamal naeem

Member
Jan 10, 2014
72
20
Naibu waziri Juma Nkamia amewapa onyo wasanii hawa
Ney wa Mitego
Shilole
Wema Sepetu
Aunt Ezekiel

Kwa sababu hawana maadili mazuri ndani ya Jamii kwa kazi zao kwa hiyo wametakiwa kujirekebisha tabia zao.

Alisema hayo bungeni asubuhi ya leo.
 
Afanye kwa vitendo sio kuwatishia. Ila kuna wasanii wanaharibu kabisa watoto wa Ki tanzania msanii kama Wema sio kioo cha jamii kabisa
 
wamepewa onyo la nin? mbona hwakumpa onyo yule mzito aliyebaka na kumuambukiza ngoma kale kabinti..?
 
ivi kweli anaenda kumpa onyo msanii bungeni??

BAKITA wanafanya nini? na je ilo ndo la kupotezea muda na hela za mlipa kodi?

aanzishe tume ya kuwafunda
 
Siku zote alikuwa wapi? Kwa nini awaonye hadharani na asiwaite na kuwapa hilo onyo personally? Hivi ni kazi ya Waziri kuonya Wasanii? Kama kazi zao hazina maadili (yepi?) BASATA na vyombo vingine vya kudhibiti kazi zao wako wapi?
 
Ni uendawazimu wa Hali ya juu kutegemea msanii au mtu mwingine kuwa kioo cha watoto wako! It's ur responsibility period, watu wasio na maadili sio Wema na hao wengine waliotajwa na m.j.i.nga wapo wengi sana! Hawawezi kuisha by the way kila mtu Ana uamuzi wa kuendesha maisha yake anavyotaka as long as they don't break the law.
 
Hata uwe na malezi mazuri kiasi gani ukweli utabaki sanaa na wasanii wana influence kubwa kwa vijana...watu kutwa wako IG wanafuatilia maisha ya hawa watu....

Huko kwa wenzetu kuna watoto mpaka wanaua kwa sababu ya kufuatilia fictions za mitandaoni...

Nakubali kuwa ni ngumu ku controll; ila nasikitika kuwa watoto wa digitally hawawezi kuwa controlled na malezi ya wazazi peke yake....Hapa ukute kuna mabinti ma elfu wanataka wakikuwa wafuate nyayo za Wema (sina hakika kama ni nzuri au mbaya maana si mfuatiliaji; si wa umri wangu) sasa kama si role modal mzuri wameingia chaka...

Na kwa kuwa wanatumia TV na other mass media Waziri hajakosea; kuwataja Bungeni nadhani ni ili na wengine wa mfano huo wasikie...

Nakumbuka HG wangu alikuwa ananambia ambitions zake na anavyotaka kuwa kama hawa wsanii...nikamwambia hao wako fake; usidhani usanii unalipa hivyo Bongo wana vyanzo vingine vya mapato...akanambia bora dada umenielimisha; yani nilikuwa nawa admire sana...

Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi kidogo sana, Kama kuna watoto wenye access ya mtandao basi nakuhakikishia wajapan wanaongoza ila huwezi kukuta watoto wana tabia za hovyo Kama kwetu, wazazi wengi wanaiachia jamii kwenye kujenga maadili ya mtoto baba yupo busy na kazi na ulevi. Watoto wanatakiwa kuwa monitored kwa ukaribu sana.
 
Back
Top Bottom