wasaliti UDSM

KWETU PAZURI

Senior Member
Oct 14, 2011
161
26
wanafunzi wa UDSM wamewasaliti wenzao waliofukuzwa kwa kuendelea na masomo huku haki za wenzao zikikandamizwa, hii ni tofauti kabisa UDSM inayojulikana kwa kutetea haki za kila mwanafunzi.
Nawakilisha.
 
Hamna wapambanaji tena hapa,vijana mnaweka mbele usharobaro na usister duu tu na wakati mnanuka shida!!oi, ngoja sisi tumalize zetu tuwaachie chuo chenu na wakna mkandala wenu waendelee kuwaonea ...maana kitendo cha makamanda wenzetu kufukuzwa thn sisi tunaendelea kuingia class ni dhambi moja kubwa sana kwa maisha ya hapa udsm.
 
...wanisamehe kama nitawaudhi, ila bado ni watoto wadogo kiumri na kiakili pia.
Nahisi wakati flani watachapwa hata bakora darasani.
 
wanafunzi wa UDSM wamewasaliti wenzao waliofukuzwa kwa kuendelea na masomo huku haki za wenzao zikikandamizwa, hii ni tofauti kabisa UDSM inayojulikana kwa kutetea haki za kila mwanafunzi.
Nawakilisha.

siamini kama hili laweza tokea UDSM!! kama ni kweli hawa vijana wanatia aibu!! isingewezekana hii enzi za FOE!!!
 
Wamepewa boom wamewasahau wenzao kweli hela mwanaharamu,mwanzoni walijifanya wanapigania haki ya wale waliosimamishwa kumbe ilikuwa gelesha boom ndyo ilikuwa lengo haswa,dah!poleni mliofukuzwa
 
Uliwahi ona wapi sharobaro au sister du anafanya maamuzi magumu?wamenikera sana usharobaro gani wakati mmejaa shida mwili mzima?
 
someni vijana ndio kilichowapelekeni hapo msifuate mkumbo walioenda wameenda kazeni buti.
 
inauma sana ndugu zangu, laiti kama igekua wewe ni mzazi au mwanafunzi mmojawapo kati yao, ndio ungeona nchi hii inavyoendeshwa kidkteta, wamejaza usalama wa taifa na FFU kibao huku chuo kiasi ambacho hata kuongelea hilo jambo inakua ngumu. Ila naamini kama ALSHABAAB alivyosema "KAMA IPO, IPO TUU" kuna haja ya kutafuta namna nyingine ya kuwasaidia wenzetu ikiwezekana wakishtaki chuo kwa maana kupata elimu ni haki ya msingi ya kila mtanzania, iweje leo wakatazwe kujiunga na chuo chochote cha umma Tanzania?
 
Umoja wa UDSM ulikuwepo kille kipindi cha kina Mtatiro hata mmoja akifukuzwa kunji mpaka chuo kinafungwa ila sasa masikini ndiyo wamekuwa waoga na hatima yao wanapomaliza chuo ni kufanya kazi za mshahara wa laki tatu hata watakapodhulumiwa hawatahoji huko ndiko tunakokwenda na usishangae wale waliofukuzwa ni kutoka familia bora kesho na keshokutwa watakuwa mabosi kwenye hizi ofisi za serikali sasa utakapokwenda na cheti cha mlimani sijui jamaa atakuchukuliaje ebu fikiria hapo unamkuta bosi uliyemuasi utaficha wapi huo uso.Tuna mifano ya watu waliofukuzwa hapo mlimani miaka flani sasa ni kati ya mabosi katika serikali hii kwa hiyo mnapofanya mambo muangalie impact yake huko mbele.Masomo mema wale mliofukuzwa mlango mmoja ukifungwa mwingine unafunguka msikate tamaa ya maisha it is very complex inawezekana mmeandikiwa kutosoma hapo mlimani jitahidini kutafuta other altenative Mungu yupo pamoja nanyi.
 
kila jambo na wakati wake, UDSM ya 1990's na early 2000's haiwezi fanana na hii ya sasa! ingekuwa enzi zetu, Buhenyenge aka 'Bush', mr owawa, mtatiro n.k wangekuwa washatengeneza modality ya kunji mpaka kieleweke...
 
Back
Top Bottom