Wasaidieni wagonjwa kwa hili

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Kama kuna mgonjwa wa ngoma unamfahamu, iwe ni ndugu rafiki au jirani, Kama binaadamu yeyote yule msaidieni kwa kumtengenezea supu ya mbigili. (mmea wa mbigili una miba midogomidogo ya kijani kabla ya kukauka) Wazee wa zamani walitumia kama mboga na tiba kwa ajili ya maradhi mbalimbali ikiwamo maralia. Hivyo basi ikiwa mgonjwa hajiwezi kabisa apewe supu hiyo, isitiwe chumvi ama kiungo chochote anyweshwe na kama ana nguvu zake basi akorogewe uji wa ulezi na achanganyiwe asali kidogo na itiwe supu ya mbigili aidha itumike supu hiyo kukoroga huo uji.

Usaidizi mwingine ni kwa watu walioko middle east: Majani ya Tini yanasaidia pia kupunguza makali.

Naomba ieleweke vema, hiyo si tiba kamili bali ni usaidizi wa mgonjwa kupata nafuu na kupandisha kiwango cha kinga, kitokea mtu amepona basi na amshukuru na kumhimidi mola wake.
 
Asante kwa kutujuza na wasisahau kupima kipimo cha APLICOR HIV 1 MONITOR TEST baada na kabla ya kunywa supu ya MBIGILI ili kujua maendeleo yao
 
Maelezo zaidi:
Mbigili ni aina ya mmea jamii ya nyasi ambayo hutumiwa kama mboga hususani na wakazi wa mkoa wa Pwani na kwengineko barani Afrika. Una miba midogo midogo. wakati wa kiangazi hukauka na miba ile watembea peku wanaijua habari yake. (miiba yake ni kama umbile la nyota - vile wanavyonasibisha wachoraji)
 
Kama kuna mgonjwa wa ngoma unamfahamu, iwe ni ndugu rafiki au jirani, Kama binaadamu yeyote yule msaidieni kwa kumtengenezea supu ya mbigili. (mmea wa mbigili una miba midogomidogo ya kijani kabla ya kukauka) Wazee wa zamani walitumia kama mboga na tiba kwa ajili ya maradhi mbalimbali ikiwamo maralia. Hivyo basi ikiwa mgonjwa hajiwezi kabisa apewe supu hiyo, isitiwe chumvi ama kiungo chochote anyweshwe na kama ana nguvu zake basi akorogewe uji wa ulezi na achanganyiwe asali kidogo na itiwe supu ya mbigili aidha itumike supu hiyo kukoroga huo uji.

Usaidizi mwingine ni kwa watu walioko middle east: Majani ya Tini yanasaidia pia kupunguza makali.

Naomba ieleweke vema, hiyo si tiba kamili bali ni usaidizi wa mgonjwa kupata nafuu na kupandisha kiwango cha kinga, kitokea mtu amepona basi na amshukuru na kumhimidi mola wake.

kinachotengezwa supu ni majani, mizizi au matunda na mmea huu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom