Was Mkapa Wrong on This? Really?

Back to Ben stuff. Kuna jamaa mmoja wa PSRC nilikuwa namuuliza kuhusu kama kweli kulikuwa na haja ya kuuza makampuni, alisema wazi kabisa kuwa kila mahali kulikoingia foreign element, kimsingi kulionesha mabadiliko na mafanikio makubwa, japokuwa local elements (siasa za ubinafsi) ziliendelea kukwamisha baadhi ya mambo. Lakini nimekumbuka mengi sana niliyokuwa naongea na Mr Kavishe wa PSRC na kuangalia jinsi tulivyoichezea ATCL, Tazara etc naona kuwa Ben hakukosea sana. (Japokuwa kuna maswali mengi huko TRC).

.

PSRC ndio wa kulaumiwa including huyu uliyemtaja hapo juu, ambaye alikuwa Director mkubwa tuu. Hawa watu kipindi kile wakibinafsisha walikuwa wakidhihaki wale wote wenye mawazo tofauti. Hawa watu (PSRC), waliamini ya kuwa wao ni watu wenye uwezo mkubwa sana wa kufikiri, na wana exposure ya hali juu na kuwabeza wananchi wengine. Kuna kipindi waliwahi kusema kuwa wananchi taka wasitake haya mashirika yatabinafsishwa tuu!

Hawakufanya Research yoyote kuona wether makampuni yale yalikuwa profitable or not albeit, the fact that, they were being paid alot of money by the taxpayers. The sad thing is, Tanzaninans are on the loosing end on this issue after being betrayed by their fellows compatriot (PSRC). Wale wote waliokuwa wakurugenzi wa PSRC wanaishi kama wafalme sasa hivi (classic example Rubambe), to make a long story short, we don't want to hear their advice now because they didn't listen to us when it matters.
 
. May be I would have done the same if I was wearing Bens shoes in 1996. I know this may make me sound like an idiot to some, but am not, I think am not.

.

Moja ya sifa ya ungozi ni kujua tabia na saikojia ya unaowaongoza.Ben (mwandishi wa habari na mpenda kusoma) alitujua na mpaka leo anatujua tabia yetu.

Ugonjwa wa tanzania ni kama mtu mwenye jipu, ukitaka ulisogelee kukamua anakufukuza.Hatutaki kuambiwa ukweli na tunataka kuonyosha vidole kwa wengine.

Nashangaa mnasema watanzania wengi wako nje, believe me si kama mataifa mengine ya Afrika, Kenyan, western afrika, wako nje kama kwao vile.Lengo la kusema hivi ni kuwa sisi ni waoga, tumedumazwa, elimu yetu siyo ya Objectively ila subecjtively.

Confidence ndogo, uvivu jadi yetu, kuishi kwa kushindana na kujua nani kafanya nini is part of our culture(kamuulize Shigongo).

The only way that can add value in human life is WORK, thats all, siyo ubosi kama elimu yetu ya vyuoni inavyotufanya tuamini. As a result tuna watu wengi wenye uwezo wa kukaa ofisini, they are not creative! these are very same people that catch any 'opportunity' in their workstations

Nyerere alijitetea na kusema alichukua nchi ina wahandisi wawili, leo hii tunao maelfu, where are they?I know the best genius students(Ilboru, Mzumbe, Kibaha) in this country ndio wengi wamesoma uhandisi wa umeme! yet tunajitetea siasa inawaingilia, wanasiasa hawa wametoka wapi?

We have problems, we are the part of it.

Nikatoa hoja siku moja kuwa Kama Mkapa kafanya hivyo where is the problem, Mkapa au system yetu? na solution ni kulilia system ibadilike au kumsema Mkapa, nani ambaye anaweza kuthibitisha kama angekuwa Ikulu asingeiba? katika sisi wanadamu? wengine watasema Nyerere,WELL Nyerere hakuwa system, hakuwa nchi, hakuwa sheria, hakuwa katiba na hatakuwa katiba, alifail kwa kuweka System mbaya kwa sababu yeye ni 'mtakatifu' basi woote wako hivyo hivyo! as a result wezi wakubwa wote wa nchi hii ni 'watoto wa Nyerere'

Mamlaka ya rahisi inabidi yapunguzwe, katiba ibadilishwe, serikali iwe ya umoja wa vyama vyote MMEISHWAHI KUSIKIA VYAMA VYA UPINZANI WANAANDAMANA NA KUTOKA DAMU KWA SABABU YA KULILIA HAYA MAMBO?? hii si dalili tosha ya kuwa tuna ulemavu wa ubongo, kama vyama vya upinzani havijui wajibu wao, kesho wanaenda kwenye uchaguzi wakijua wanshindwa, HUKO MAOFISINI NA MAKAZINI je!! si same-like story

Who said Mkapa was wrong anyway??

Sipati picha kama Mkapa angekuwa madarakani mpaka leo!!!!!!
 
It is one thing kubinafsisha mashirika na viwanda vya umma.

Quite another kuuza at throwaway prices zinazosuggest sleaze, kwa watu wasio na uzoefu, majority yao wakiwa wageni.

And the game hits the stratosphere when Mkapa cut a piece of the pie for himself with Kiwira .

I mean how can you defend such a man, Mkapa came across as a common uneducated thief on the scale of the Abachas, Mobutus and Marcoses of this world, at least in principle if not exactly in scale.

PSRC wanatakiwa kulaumiwa kwa kukosa principles certainly, lakini PSRC ilikuwa inaendeshwa kutoka Ikulu na kupewa agenda na Ikulu, kwa waliojali kibarua zaidi ya principle hawakuwa na jinsi.

In any case, Mkapa kama rais alichukua responsibility ya kila kitu na ndiye mtu aliyekuwa na uwezo wa kubadilisha mambo kuliko mwingine yeyote Tanzania.Hakutumia uwezo wake wa kushawishi au nguvu za ofisi ya rais kuhakikisha process nzima inaenda vizuri.
 
Well, mkuu ni kweli kabisa it is only a tiny part of Tanzanians who are abroad, sidhani kama wamefika milioni moja. Na kati ya hao kuna wachache sana wale ambao watanzania tunaweza kuwa proud nao, wengi wako hapa JF (at least wanatoa mchango wa vidole na bongo zao), wengine wamekuwa wezi na matapeli na kuchafua jina la Tanzania, so it is only a tiny part and very few of them ndio wanatoa msaada wa kiakili tunaouhitaji zaidi kuliko hela.

"The only way that can add value in human life is WORK, thats all,"

Mkuu nimelazimika ni quote hiyo ni sentenisi nzito sana, tumejenga utamaduni fulani wa kupenda kuletewa kichwa kilichokatwa mezani, tukidhani kuwa huyo serikali ndio atafanya kazi hiyo. Hata wengine huko juu wanajenga utamaduni wa ajabu sana na kumfanya kila mtu anayeingia amadarakani atamani kuwa mwizi na sio kuiendeleza Tanzania.

In deed we are part of the problem, while we are trying to throw everthing at mafisadi, ni lazima tujiangalie sisi wenyewe. Wenzetu ambao leo wanaishi maisha ya raha wanafanya kazi zaidi kuliko sisi tunaoishi kwenye maisha ya taabu.

Masanja & others

Umenena. Ila binafsi naomba kujua jinsi gani tunaweza kumwajibisha JK na timu yake na tukafanikiwa? Kwa ufupi hali inasikitisha sana.
 
It is one thing kubinafsisha mashirika na viwanda vya umma.

Quite another kuuza at throwaway prices zinazosuggest sleaze, kwa watu wasio na uzoefu, majority yao wakiwa wageni.

And the game hits the stratosphere when Mkapa cut a piece of the pie for himself with Kiwira .

I mean how can you defend such a man, Mkapa came across as a common uneducated thief on the scale of the Abachas, Mobutus and Marcoses of this world, at least in principle if not exactly in scale.

PSRC wanatakiwa kulaumiwa kwa kukosa principles certainly, lakini PSRC ilikuwa inaendeshwa kutoka Ikulu na kupewa agenda na Ikulu, kwa waliojali kibarua zaidi ya principle hawakuwa na jinsi.

In any case, Mkapa kama rais alichukua responsibility ya kila kitu na ndiye mtu aliyekuwa na uwezo wa kubadilisha mambo kuliko mwingine yeyote Tanzania.Hakutumia uwezo wake wa kushawishi au nguvu za ofisi ya rais kuhakikisha process nzima inaenda vizuri.

Salute mkuu. Ben alikuja na idea nzuri, yaani kuuza makampuni yaliyokuwa yana underperfom, tulitegemea kuwa yakiuzwa yataperfom na yatawanufaisha zaidi watanzania kuliko ilivyokuwa mwanzo. That is what we were told and that was what we were expecting, not what has come out to be ujanjaujanja, we did not know that someone was trying to buy a mine for himself( labda alikuwa namuwezesha mzawa-yeye mwenyewe)

PSRC si wapo? why don't we bring them before the public and let them tell us why did they lie to us? Hii ndio weakness yetu watanzania. Kwanini na sisi tusiwe na Chilcot inquiry yetu? au ndio waafrika wepesi wa kusahau?
 
.

Nikatoa hoja siku moja kuwa Kama Mkapa kafanya hivyo where is the problem, Mkapa au system yetu? na solution ni kulilia system ibadilike au kumsema Mkapa, nani ambaye anaweza kuthibitisha kama angekuwa Ikulu asingeiba?

Mzee hayo maneno niliyabold yanachefua na yamesummarize kila kitu kuhusu wewe na value zako. Inaonyesha ya kuwa tofauti yako na Mkapa ni kwamba wewe hujapata nafasi tuu aliyopata Mkapa na laiti ukipata utafanya the same.
 
Salute mkuu. Ben alikuja na idea nzuri, yaani kuuza makampuni yaliyokuwa yana underperfom, tulitegemea kuwa yakiuzwa yataperfom na yatawanufaisha zaidi watanzania kuliko ilivyokuwa mwanzo. That is what we were told and that was what we were expecting, not what has come out to be ujanjaujanja, we did not know that someone was trying to buy a mine for himself( labda alikuwa namuwezesha mzawa-yeye mwenyewe)

PSRC si wapo? why don't we bring them before the public and let them tell us why did they lie to us? Hii ndio weakness yetu watanzania. Kwanini na sisi tusiwe na Chilcot inquiry yetu? au ndio waafrika wepesi wa kusahau?

Certainly PSRC wanahitaji kuwajibishwa.

Lakini zaidi ya PSRC anayehitaji kuwajibishwa ni Ben Mkapa aliyetoa order kwa PSRC mkataba wa TICS uongezwe muda kinyume na taratibu wakati anakaribia kutoka katika urais, huo ni mfano mmoja tu.

Kama unataka kuwawajibisha PSRC utawawajibisha kwa kukubali upuuzi, lakini usisahau kulikuwa na orders kutoka Ikulu kufanya haya mambo. Mkapa alikuwa mbabe mpaka aka expose hubris ya kijinga.

Kabla ya kumu appoint Rubambe PSRC Mkapa alimuweka under surveillance kwa zaidi ya mwaka, including phone-tapping him. Alikuwa anatafuta nini kama siyo blackmailing info ili Rubambe asiwe na objectivity?
 
The only way that can add value in human life is WORK, thats all, siyo ubosi kama elimu yetu ya vyuoni inavyotufanya tuamini. As a result tuna watu wengi wenye uwezo wa kukaa ofisini, they are not creative! these are very same people that catch any 'opportunity' in their workstations

Nyerere alijitetea na kusema alichukua nchi ina wahandisi wawili, leo hii tunao maelfu, where are they?I know the best genius students(Ilboru, Mzumbe, Kibaha) in this country ndio wengi wamesoma uhandisi wa umeme! yet tunajitetea siasa inawaingilia, wanasiasa hawa wametoka wapi?

We have problems, we are the part of it.

Nikatoa hoja siku moja kuwa Kama Mkapa kafanya hivyo where is the problem, Mkapa au system yetu? na solution ni kulilia system ibadilike au kumsema Mkapa, nani ambaye anaweza kuthibitisha kama angekuwa Ikulu asingeiba? katika sisi wanadamu? wengine watasema Nyerere,WELL Nyerere hakuwa system, hakuwa nchi, hakuwa sheria, hakuwa katiba na hatakuwa katiba, alifail kwa kuweka System mbaya kwa sababu yeye ni 'mtakatifu' basi woote wako hivyo hivyo! as a result wezi wakubwa wote wa nchi hii ni 'watoto wa Nyerere'

Mamlaka ya rahisi inabidi yapunguzwe, katiba ibadilishwe, serikali iwe ya umoja wa vyama vyote MMEISHWAHI KUSIKIA VYAMA VYA UPINZANI WANAANDAMANA NA KUTOKA DAMU KWA SABABU YA KULILIA HAYA MAMBO?? hii si dalili tosha ya kuwa tuna ulemavu wa ubongo, kama vyama vya upinzani havijui wajibu wao, kesho wanaenda kwenye uchaguzi wakijua wanshindwa, HUKO MAOFISINI NA MAKAZINI je!! si same-like story

Who said Mkapa was wrong anyway??

Mkulu nadhani hiki kipengele ndo kimebeba uzito wa thread nzima. Ubarikiwe sana mkuu.

I have to be honest, mimi ndipo nadiffer na akina Mwanakijiji (people I admire) wanapotaka kutuaminisha kwamba Nyerere ndo alikuwa kiongozi mwadilifu sana. Maybe, maybe not. I dont blame him. After all mda wa kulaumiana haupo tena. Lakini tuwe wawazi. Nyerere might have been a good leader..lakini mzee huyu alishindwa kututengenezea misingi/structures za nchi. Kiukweli katika misingi ya utawala bora..huyo Mzee-I am afraid-ana score zero.
Katiba tuliyonayo leo..ni takataka aliyotuachia na..CCM hawawezi kuibadilisha kwa sababu ndo inawafanya wabaki madarakani..... he might have been mtakatifu..lakini na kusoma kote wanafilosophia..hakujua ni jinsi gani..absolute power inavyo-corrupt?

To me, kiongozi madhubuti ni yule anayeangalia miaka kumi, ishirini itakuwaje. Nyerere..inawezekana alikuwa na mapenzi mema na nchi yake..lakini ukweli..kama huyu mzee angetuwekea misingi ya katiba inayoeleweka..I am sure we would be doing much much better.

Naomba nisieleweke kwamba nalaumu tuu..hapana..lakini najaribu kuonyesha kwamba bila misingi madhubuti ya kuwachukulia hatua/accountability viongozi..hatuwezi kutegemea mabadiliko yoyote. And we simply dont have those means. Leo watu wanaiba na impunity...hivi kweli katika mazingira kama hayo..bila kuwa responsible citizenship..twaweza songa mbele?

Wapinzani nao wamejichokea tuu..hawajui ni agenda gani ya muhimu katika maisha ya wale wanao wapigania..pathetic..
 
Mzee hayo maneno niliyabold yanachefua na yamesummarize kila kitu kuhusu wewe na value zako. Inaonyesha ya kuwa tofauti yako na Mkapa ni kwamba wewe hujapata nafasi tuu aliyopata Mkapa na laiti ukipata utafanya the same.

Hayachefui labda kama hutaki kukubali kuwa binadamu anaongozwa na sheria, system na taratibu walizojiwekea, leo tunalia Mkapa hatuwezi kumshtaki kwa nini? Binadamu tuna hulka ya umimi,kutaka vingi na security, kama mtu anaona ana uwezo wa kuchukua kitu fulani na hataulizwa huoni ni hatari kwa tabia ya binadamu.Huoni maneno yangu yanathibitishwa na wingi wa jela kila kona dunia hii.Kama wewe unasema ungepata cheo cha Mkapa usingeiba ni wewe ila wengi ni wezi ndugu yangu.Tunazuia wezi kwa sheria kali.

Hao mawaziri Mafisadi na viongozi wengine si ni binadamu? unataka niape kuwa mimi ningekuwa clean!! hata kama mimi nitakuwa clean je ajaye? we have to have a clear and undisputed system za kuzia huu wizi na sio kuishi kwa assumptions! kuwa Rufiji mzee wa kanisa mpe wizara ya fedha! agha! makanisani nako ndio hivyo!

Leo hii JK yuko ikulu naye akifanya ya Mkapa solution ni kumsema tu!! you missed my main point! sorry
 
Very Very True!

Mr Bongolander, are u real a Tanzanian? or may be you a relative to that Man, I can't believe you came up with this article!

Well, i am real Tanzanian, am a relative of that man in a sense that he is my fellow country man, but not my sibling or close relative, not at all. The thing is a tried to look at a thing itself not a man himself.

Actually if you look at it from different angles you will be suprised where did Ben got all the guts he had in selling his idea. It is sad that we are the ones who gave him the guts. And we gave him all excuses to do what he did. Ni sisi tulivurunda mashirika yetu na akatumia excuse hiyo hata kuuza ambayo hayakuvurundwa.
 
Japo umejaribu kujitakasa hayo maneno niliyoweka kwenye red nayarudia tena kwa herufi kubwa kuonyesha msisitizo, YOU ARE AN IDIOT. Kwani nasema hivyo nakunukuu hapo chini

Unataka kusema ATC ilikuwa afadhali wakati wa makaburu japo wametuongezea deni tunalowalipa for not only doing nothing but also stealing from us? What about Net Group Problems? Kaa kimya ufurahie matunda ya ujambazi kuliko kututukana waziwazi.

Hapa jisemee mwenyewe, angalia vitendo vyako ambavyo vinajidhihirisha kutokana na utetezi wako. Kuleta TX mgodini anayefundishwa kazi na wazalendo aliowakuta pale halafu analipwa mara kumi yao ni jambo la kujisifia. Kisha akipata hela zake je akaunti yake iko NMB? Usituchefue hapa. Eboo! Narudia tena you are an idiot.

ATC ilihujumiwa enzi za Mkapa, kwa baraka za Mkapa kupitia PSRC na Mwandosya. Wataalam walijaribu kuwatahadharisha hatari na hasara za kuingia ubia na South African Airways lakini Mkapa alikuwa anapewa shinikizo na kina Ami Mpungwe, ambaye alikuwa kibaraka wa wa-afrika kusini wote waliokuwa wanajidai wanataka kuwekeza hapa kuitoa ATC kwa bei ya nyanya na kwa masharti ya kijinga mno!
 
Mkulu nadhani hiki kipengele ndo kimebeba uzito wa thread nzima. Ubarikiwe sana mkuu.

I have to be honest, mimi ndipo nadiffer na akina Mwanakijiji (people I admire) wanapotaka kutuaminisha kwamba Nyerere ndo alikuwa kiongozi mwadilifu sana. Maybe, maybe not. I dont blame him. After all mda wa kulaumiana haupo tena. Lakini tuwe wawazi. Nyerere might have been a good leader..lakini mzee huyu alishindwa kututengenezea misingi/structures za nchi. Kiukweli katika misingi ya utawala bora..huyo Mzee-I am afraid-ana score zero.
Katiba tuliyonayo leo..ni takataka aliyotuachia na..CCM hawawezi kuibadilisha kwa sababu ndo inawafanya wabaki madarakani..... he might have been mtakatifu..lakini na kusoma kote wanafilosophia..hakujua ni jinsi gani..absolute power inavyo-corrupt?

To me, kiongozi madhubuti ni yule anayeangalia miaka kumi, ishirini itakuwaje. Nyerere..inawezekana alikuwa na mapenzi mema na nchi yake..lakini ukweli..kama huyu mzee angetuwekea misingi ya katiba inayoeleweka..I am sure we would be doing much much better.

Naomba nisieleweke kwamba nalaumu tuu..hapana..lakini najaribu kuonyesha kwamba bila misingi madhubuti ya kuwachukulia hatua/accountability viongozi..hatuwezi kutegemea mabadiliko yoyote. And we simply dont have those means. Leo watu wanaiba na impunity...hivi kweli katika mazingira kama hayo..bila kuwa responsible citizenship..twaweza songa mbele?

Wapinzani nao wamejichokea tuu..hawajui ni agenda gani ya muhimu katika maisha ya wale wanao wapigania..pathetic..

You are right, NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO!

Misingi ya chi ikiwa mibaya kila kitu baadaye kinakuwa vibaya, Tunachomiss ni kupata viongozi wanaijua misngi na na tatizo letu, watufanyie underpinning([ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Underpinning[/ame]).

Tuna matatizo mengi ambayo msingi wake ni siasa ya ujamaa, tunaviongozi wabovu na wasiotusikia kwani walilewa fikra za mwenyekiti ndio sahihi.

Tusipoangalia msingi ya nchi hii,na kujua ugonjwa wetu uko wapi, tutawasema akina mkapa wee, kesho JK, na fulani na fulani maisha yanaendelea na nchi bado inakuwa kwenye top 10 ya nchi 'bora maskini' duniani yet people try to defend Nyerere!

Mkapa alishtua kidogo sehemu moja ya umwinyi tuliokuwa nao, hata kama leo bado watu sio wachapa kazi, lakini Mkapa alifungua macho kuwa UTAKULA KWA JASHO , sio njia za kijanja janja za akina Mwinyi!

Concept ya ujamaa kuwa wewe masanja ufanye kazi tule wote 'kwa sababu vyote ni mali ya wote'' mmh! I doubt imetuleta hapa!
 
Moja ya sifa ya ungozi ni kujua tabia na saikojia ya unaowaongoza.Ben (mwandishi wa habari na mpenda kusoma) alitujua na mpaka leo anatujua tabia yetu.

Ugonjwa wa tanzania ni kama mtu mwenye jipu, ukitaka ulisogelee kukamua anakufukuza.Hatutaki kuambiwa ukweli na tunataka kuonyosha vidole kwa wengine.

Nashangaa mnasema watanzania wengi wako nje, believe me si kama mataifa mengine ya Afrika, Kenyan, western afrika, wako nje kama kwao vile.Lengo la kusema hivi ni kuwa sisi ni waoga, tumedumazwa, elimu yetu siyo ya Objectively ila subecjtively.

Confidence ndogo, uvivu jadi yetu, kuishi kwa kushindana na kujua nani kafanya nini is part of our culture(kamuulize Shigongo).

The only way that can add value in human life is WORK, thats all, siyo ubosi kama elimu yetu ya vyuoni inavyotufanya tuamini. As a result tuna watu wengi wenye uwezo wa kukaa ofisini, they are not creative! these are very same people that catch any 'opportunity' in their workstations

Nyerere alijitetea na kusema alichukua nchi ina wahandisi wawili, leo hii tunao maelfu, where are they?I know the best genius students(Ilboru, Mzumbe, Kibaha) in this country ndio wengi wamesoma uhandisi wa umeme! yet tunajitetea siasa inawaingilia, wanasiasa hawa wametoka wapi?

We have problems, we are the part of it.

Nikatoa hoja siku moja kuwa Kama Mkapa kafanya hivyo where is the problem, Mkapa au system yetu? na solution ni kulilia system ibadilike au kumsema Mkapa, nani ambaye anaweza kuthibitisha kama angekuwa Ikulu asingeiba? katika sisi wanadamu? wengine watasema Nyerere,WELL Nyerere hakuwa system, hakuwa nchi, hakuwa sheria, hakuwa katiba na hatakuwa katiba, alifail kwa kuweka System mbaya kwa sababu yeye ni 'mtakatifu' basi woote wako hivyo hivyo! as a result wezi wakubwa wote wa nchi hii ni 'watoto wa Nyerere'

Mamlaka ya rahisi inabidi yapunguzwe, katiba ibadilishwe, serikali iwe ya umoja wa vyama vyote MMEISHWAHI KUSIKIA VYAMA VYA UPINZANI WANAANDAMANA NA KUTOKA DAMU KWA SABABU YA KULILIA HAYA MAMBO?? hii si dalili tosha ya kuwa tuna ulemavu wa ubongo, kama vyama vya upinzani havijui wajibu wao, kesho wanaenda kwenye uchaguzi wakijua wanshindwa, HUKO MAOFISINI NA MAKAZINI je!! si same-like story

Who said Mkapa was wrong anyway??

Sipati picha kama Mkapa angekuwa madarakani mpaka leo!!!!!!

Webby....kula tano babake
 
Hayachefui labda kama hutaki kukubali kuwa binadamu anaongozwa na sheria, system na taratibu walizojiwekea, leo tunalia Mkapa hatuwezi kumshtaki kwa nini? Binadamu tuna hulka ya umimi,kutaka vingi na security, kama mtu anaona ana uwezo wa kuchukua kitu fulani na hataulizwa huoni ni hatari kwa tabia ya binadamu.Huoni maneno yangu yanathibitishwa na wingi wa jela kila kona dunia hii.Kama wewe unasema ungepata cheo cha Mkapa usingeiba ni wewe ila wengi ni wezi ndugu yangu.Tunazuia wezi kwa sheria kali.

Mimi napinga kitendo chako cha kutaka kujustify maovu ya mkapa simply kwa sababu hatuna sheria kali zinazowabana viongozi wetu. Kitendo cha kusema hata wewe ungekuwa Ikulu you would have done the same, ni cha kinyama na kizandiki to say the least !

Waberoya , mimi naamini ya kuwa mwanadamu lazima uwe na value ambazo zitakuongoza katika maisha yako ya kila siku . Moja ya sababu inayowafanya watu waogope kuua , sio adhabu ya kifo peke yake ; bali ni maadili yao na unyama wa hicho kitendo. Hata kama tutakuwa tuna sheria kali, kama atutakuwa misingi binafsi imara tutakuwa tunapoteza muda. Vile vile lazima ujue ya kuwa ,two wrongs don't make a right kutokuwa na sheria hakualalishi mtu kuiba! Vipi kama watu kama kina Nyerere wangekuwa na mawazo kama hayo ?

Kusema ukweli kauli yako sio tuu imenikwaza bali imenialibia siku yangu. Zaidi, ni kauli kama hizi ndio zinastawisha tabia chafu za ubinafsi.
 
Kaka nakubaliana na wewe! una roho nzuri na utu,

Ila what about Mkapa? Mkapa asingeiba tungekuwa tunajadili haya leo? Ok Mkapa aliongozwa na hizo value kujichukulia Kiwira?, mbona kama tunaongea lugha moja kwa style tofauti? hizo value ndio zinawafanya wazee tunaowaheshimu kubaka watoto wadogo!

Yaani kwa sababu ya value tusiwe na sheria wala system? kwa binadamu hawa tunaowaamini na wana tu turn down everyday? kwa concept ya value hizo hizo watu ndio wanaiba na huwezi kuamini,

Kitu usichojua wa kwetu ni kuwa hakuna standard value, kitu ambacho wewe unakiita wizi mwenzako anaita deal, kitu ambacho wewe unaita uzinzi mwenzako anaita kujirusha, kuna wenzako wanaona kuua si kosa, wakati wewe Rufiji unaona kuchinja kuku dhambi, where are those standard value that we human are based on? why we are not equal? why Mkapa then is not thinkin like you? I am not such bad ,but human has proved failure to value 'value' thats why I insist laws and systematic system should put in place! hapa mimi mbaya?

is those Value value??

Kiongozi gani wa CCM unayemwamini anayeongozwa na hizo value? I am not such bad, mkuu nikiongea kichungaji mimi mchungaji, linapokuja swala la kitaifa na kuheshimu sheria ondoa kabisa ubinadamu mkuu! The world is dangerous simply because we have failed to practise those value mkuu!

Hautaki kukubali kuwa kutokuwa na sheria au kuzitekeleza ndio matatizo?

Simply Mkapa ameiba, tutazuia tatizo kwa value?

Rufiji jiamini mwenyewe value ni wewe tu, na wengine nao watajiaminisha kivyao, ila usimwamini binadamu kuwa ataongozwa na value, hiyo notion imeshafail, sana sana nawafundisha watu makanisani, ila kitaifa, sahau, otherwise tusingekuwa na watu magerezani

Nyerere alifail, aliona kila mtu mtakatifu kama yeye, watu walikuwa wakiharibu au kufilisi mashirika ya umma ana wahamisha, kimsingi point yako ya value inaondoa kabisa sense of responsibility, na value unaijua kwa sababu mtoto wa watu una dini sijui mwislamu au Mkristo, wengine hawamjui huyo Yesu wala Muhammad, thats why I made statement.lazima kuzuia ili tatizo kuwe na sheria ya kumbana rais, maana kama tutawaamini watu basi yeyote anaweza kuiba! sijajua ubaya wangu uko wapi

In the beginning ...Genesis 1:1......Genesis 3; Utaona mwanadamu alivyopoteza value, utaona Musa baadae anayoanza kuweka sheria na waamuzi, utaona Sodoma na Gomora ushoga ulivyokuwepo, I am telling you in those days...huu ni mwaka 2008 For God sake, watu wamefanya dhambi mpaka wanaanza kuzi-recycle tena. Simwamini mtu yeytote kuingia Ikulu kwa sense ya value nataka mtu aingie ajue akitoka tu kama amekosea JELA.

I repeat kwa wanadamu hawa, aingie ikulu unamwambia fanya lolote utakavyo, hata Kilimanjaro chukua, chukua fedha zozote utakazo, ukimaliza kipindi chako u are free! I said these attracts ufisadi, nikiiangalia historia ya binadamu napata wasiwasi kuwa hawa marais wetu kila atakayetoka itakuwa kama Mkapa, and this may happen to many others, Unless hao watu sio wa dunia hii!

I doubt standard ya value ya Mkapa ni kujichukulia Kiwira! LOL

.Kumsema Mkapa huku hakutusaidii sisi , tuangalie solution, tumeshasema mwaka wa nne, naamini akina JK wenye value wangekuwa wameshamevaluate huyu jamaa na kumweka ndani segerea akajifunze value.

with all due respect, na samahani kwa kukuharibia siku mpendwa
 
Salute mkuu. Ben alikuja na idea nzuri, yaani kuuza makampuni yaliyokuwa yana underperfom, tulitegemea kuwa yakiuzwa yataperfom na yatawanufaisha zaidi watanzania kuliko ilivyokuwa mwanzo. That is what we were told and that was what we were expecting, not what has come out to be ujanjaujanja, we did not know that someone was trying to buy a mine for himself( labda alikuwa namuwezesha mzawa-yeye mwenyewe)

Hivi Bongolander una hakika kwamba idea ya kuuza mashirika ya umma ililetwa na Mkapa? Tafuta hotuba ya Nyerere ya Mei Mosi 1995 alipokuwa akilaani kuuza mashirika yanayotengeneza faida kama TCC na TBL halafu utaelewa idea ya kuuza mashirika ya umma ilianza lini. Na kwa taarifa yako idea ya kuuza mashirika ya umma ilianza kwa akina Reagan na Thatcher huku kwetu ikaletwa na taasisi kama World Bank na IMF kipindi cha uchumi huria hasa kuanzia mwishoni mwa miaka ya themanini. Lengo lilikuwa kuzifanya serikali ziache kujishughulisha na biashara je ni kiasi gani imefanikiwa kwa kweli tafiti nyingi hasa kwenye nchi zinazoendelea zimeonyesha mafanikio kidogo.
 
Ninavyokumbuka na kufahamu ni kuwa, policy ya kubinafsisha mashirika ya umma ilianza awamu ya pili ya uongozi wa nchi. Shinikizo lilitoka nje kama ambavyo Mkodoleaji alivyoainisha kwa ufupi hapo juu.

Ukweli unabaki kuwa, mashirika mengi yalikuwa katika hali mbaya sana. Uongozi mbovu wa serikali na mashirika yenyewe ndiyo iliyokuwa chanzo cha kufa kwa mashirika hayo. Mashirika na viwanda vililipia kila kitu kilichofanywa na serikali. Kuanzia mbio za mwenge, sherehe za kitaifa na kichama, vikao vya kisiasa hadi safari za viongozi.

Kwa wale waliokuwa wakifuatilia, watakumbuka kuwa viwanda vyote vya nguo, kusindika nyama, mahoteli (Kilimanjaro Hotel, Hotel 77, na nyingine nyingi), viwanda vya vipuri kama Kilimanjaro Machine tools na vingine (hata Kioo Limited) vilikuwa aidha vimekufa au vilielekea kufa (vimesimamisha uzalishaji).

Niliwahi kufanya ka-research kadogo wizara ya viwanda mwaka 1994, nikakutana na Mkurugenzi mmoja wa viwanda wakati ule. Akaniambia sababu kubwa za kufa kwa viwanda hivyo ni kama zifuatazo;

1. Ukosefu wa mitaji, pamoja na uwekezaji mdogo wa serikali kwa viwanda vyake
2. Uongozi mbovu: Kitaaluma, pamoja na zoefu wa kuendesha viwanda kibiashara
3. Utunzaji mbovu wa mali, ikiwa ni pamoja na periodic maintenance za vifaa vya viwandani na mitambo
4. Uzalishaji wa bidhaa duni unaotokana na uchakavu wa mitambo (kutokana na mitambo mingi kuwa ya zamani sana)
5. Ufujaji wa makusudi unaofanywa na viongozi wa kisiasa kwa manufaa binafsi, ya serikali na ya chama.
6. Mengine mengi: Ikiwa ni pamoja na ushindani wa kibiashara kutokana na bidhaa za bei rahisi zilikuwa zikiingia kwenye soko n.k.

Wakuu, hata kama viwanda hivyo vingepewa wananchi (ambao wengi wao walikuwa na uwezo mdogo wa kuviendesha kiuchumi) hakuna la manufaa ambalo leo tungekuwa tunaliongelea. Sababu ni kwamba, viwanda hivyo vilihitaji uboreshaji mkubwa sana, ambao kwa namna nyingine ni kama kuvianzisha upya.

Watanzania wangapi ambao wangeweza (kwa tathmini yetu, na ni akina nani) kujiingiza na kuendeleza viwanda hivyo, wakapata faida na kuleta manufaa kwa Taifa kwa hali ambayo tunategemea, na hasa kwa kuzingatia jinsi viwanda na mashirika hayo yalivyokuwa? Nina uhakika wengi wangeendelea kutunza magofu ambayo wangeyanunua kutoka kwa serikali. Na hii ndio sababu kubwa ya walioyanunua waliamua kubadilisha biashara na kufanya zile ambazo waliweza kuwekeza kwa haraka ili waweze kupata faida badala ya kujitafutia hasara ambazo wangeweza kuzikwepa.

Wakuu, mkifanya tathmini ya viwanda na mashirika hayo kwa wakati/kipindi hiki, bila kujali hali tuliyokuwa nayo wakati ule, mtaona dhahiri kuwa makosa makubwa yalifanyika kuvibinafsisha (sina maana kuwa kila kitu kilikuwa sahihi). Sababu ni kuwa, hali yetu ya sasa ni tofauti kwa kila namna. Ni tofauti kwa kuwa watu wengi zaidi wanaupeo mkubwa, na uwezo mkubwa zaidi kiuchumi kuliko wakati wa ubinafsishaji huo.

Vyovyote iwavyo, na mifano iko mingi ya jinsi ambavyo hata biashara za watu binafsi zinavyoumizwa na wanasiasa wa TZ. Mwakani, tutashuhudia michango mingi kutoka kwenye private sekta (ambayo sio yote ni ya hiari sana). Nini kinachotufanya tudhani kuwa, mashirika na viwanda hivyo vingekuwa bora zaidi kama vingepewa wananchi, bila kubadilisha utaratibu na utamaduni wetu? Wanasiasa wale wale waliosababisha vife ndio wangeviuza kwa wenzao na wangeendelea kudai wapewe pesa za kampeni na kujiendeleza kibinafsi. Hilo pia ni dhahiri.

Mkapa anaweza kuwa alifanya makosa sana kubiafsisha viwanda, mashirika na vitega uchumi kama alivyofanya. Lakini je, nini ingekuwa njia mbadala ya kukuza uchumi katika hali ambayo vitega uchumi hivyo vilivyokuwa? Labda tukipata jibu ya swali hili, tutatoa hukumu sahihi.
 
Niliwahi kufanya ka-research kadogo wizara ya viwanda mwaka 1994, nikakutana na Mkurugenzi mmoja wa viwanda wakati ule. Akaniambia sababu kubwa za kufa kwa viwanda hivyo ni kama zifuatazo;

1. Ukosefu wa mitaji, pamoja na uwekezaji mdogo wa serikali kwa viwanda vyake
2. Uongozi mbovu: Kitaaluma, pamoja na zoefu wa kuendesha viwanda kibiashara
3. Utunzaji mbovu wa mali, ikiwa ni pamoja na periodic maintenance za vifaa vya viwandani na mitambo
4. Uzalishaji wa bidhaa duni unaotokana na uchakavu wa mitambo (kutokana na mitambo mingi kuwa ya zamani sana)
5. Ufujaji wa makusudi unaofanywa na viongozi wa kisiasa kwa manufaa binafsi, ya serikali na ya chama.
6. Mengine mengi: Ikiwa ni pamoja na ushindani wa kibiashara kutokana na bidhaa za bei rahisi zilikuwa zikiingia kwenye soko n.k.

Wakuu, hata kama viwanda hivyo vingepewa wananchi (ambao wengi wao walikuwa na uwezo mdogo wa kuviendesha kiuchumi) hakuna la manufaa ambalo leo tungekuwa tunaliongelea. Sababu ni kwamba, viwanda hivyo vilihitaji uboreshaji mkubwa sana, ambao kwa namna nyingine ni kama kuvianzisha upya.

Mkapa anaweza kuwa alifanya makosa sana kubiafsisha viwanda, mashirika na vitega uchumi kama alivyofanya. Lakini je, nini ingekuwa njia mbadala ya kukuza uchumi katika hali ambayo vitega uchumi hivyo vilivyokuwa? Labda tukipata jibu ya swali hili, tutatoa hukumu sahihi.

Mkuu we are on the same page. Kwa mazingira ya sasa ambayo hata Ikulu yenyewe tunashindwa kui-manage, Benki kuu tunaiibia na tunashindwa hata kuwaadhibu wezi ambao tunawafahamu wazi kabisa, sioni kama tunaweza kuendesha hata kiwanda cha chumvi au cha kahawa. Pamoja na kuwa mimi sio supporter wa sera ya ubinafsishaji, lakini siwezi kuipinga kwa kuwa hata viwanda hivyo tukirudishiwa leo, ninahakika vitaishia kufa tu. Research uliyofanya ilikuonyesha sehemu tu ya hali halisi.

Hata investors nao wanalalamika kuwa wafanyakazi ni wezi, wanapenda sana ishahara mikubwa lakini efficiency inaenda chini.

Wakati wa Nyerer kulikuwa na viwanda vingi lakini angalia vilivyokufa. Ndio maana kwenye post yangu nimesema, wait a minute.. can we really blame Ben on privatization? ni vizuri tukijiangalia kwanza sisi wenyewe then tukaangalia ni vipi tumefika tulipo.
 
Back
Top Bottom