Warning: Wizi kwa njia ya M-Pesa

Darvon

Member
Apr 14, 2018
93
74
Salama wakuu?


Kwenye simu yangu leo hii mida ya saa tano amepiga simu mtu akiniuliza naitwa nani natokea wapi nina kiasi gani cha pesa, kwa kuwa si mara ya kwanza kupigiwa simu na matapeli wa aina hii nilidanganya kila kitu mpaka kiasi kilichomo kwenye mpesa nikasema nina 50000/-. Ili nione atafanyaje.

Ndipo aliponitumia sms ambayo inaonesha imetoka kwa namba binafsi na wala sio muamala wa Mpesa halafu akapiga simu kuwa eti nirudishe pesa! Nilichomjibu ndicho hapo chini.

Namba ya tapeli +255 757 695 978

Matapeli wamekuwa na tabia ya kutuma pesa kuzichanganya na zako katika account halisi ya mpesa, kwa kuwa sio mara ya kwanza kupigiwa na matapeli wa hivi nilidanganya nikijua Mpesa yangu haina salio.

Huo mchezo unafanywa siku hizi sana tuwe makini ndugu!

Mchana mwema.
CYMERA_20180420_111653.jpg
Screenshot_2018-04-20-11-33-54.jpg
 
Waliwahi kunipigia akaniuliza nina kiasi gani?

Nikamjibu wewe uko makao makuu, utakuwa unaona salio langu!
Alikata simu yake fasta
 
Walinipigia wakaniambia nimeshinda laki mbili niwape details...

Nikawapa zote za uongo

Akaniukiza kama nina salio nikamwambia nina elfu tano

Akaniukiza kama nina sim banking...nikamjibu natumia kibubu hata akaunti ya benki sina

Akadai atanitumia hiyo hela niliyoshinda nisubirie....nina mwezi wa tatu sasa nasubiri laki mbili....
 
Back
Top Bottom