warning: disturbing image...sheria mkononi?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
317031_224951500905838_100001729686150_600734_1079375650_n.jpg

hata kama ni mwivi sijui alikuwa konda huyu kwa nini tuchukue sheria mkononi?
 
Inasikitisha sana jamani haaaah, hebu fikiria kama huyu marehemu alikuwa na uhasama na mtu kisha akasingiziwa wizi hali iliyopelekea kutoa uhai wake!
...Hali ni mbaya sana Tanzania; watoto wadogo wanakua wanaona haya ni mambo ya kawaida tu. watajifunza wapi juu ya utawala wa sheria. Sad....
 
hapa sasa mkuu ndo umeharibu wikiend yangu sio siri. Mambo mengine yanatia huzuni sana, khaaaaa!
 
Hii inabainisha wananchi wamechoka, yote ni sababu ya vyombo vya usalama na sheria kutofanya kazi ipasavyo kukomesha wizi na ujambazi. kwa kifupi ni rushwa tu ndio kazi yao - kuwalinda watu wanaotii sheria sio kazi yao. Hao ndio wanastahili kupigwa mawe.
 
Oooh!! Waliotoa hukumu hii wajue ya kwao inawasubiri. Imeniuma sana. Mwenyezi Mungu amrehemu, Amina.
 
Maskini hata kama alikuwa mwizi wangeacha aadhibiwe na mahakama. Mungu amrehemu.

Ila watu nao hawajifunzi wataona mwenzao kafanyiwa hivyo bado wataenda kuiba tena.
 
Nimesikitika sana, How about his wife, children, wazazi? kweli dunia hii!
Mungu amlaze pema.
Ss nimeamini maneno ya Dr.Slaa kuwa Nchi hii haitatawalika tena!
 
Naamini kama angeambiwa achague Kuifo ama kukatwa mkono angechagua kukatwa mkono... Ni hayo tu
 
Juzi mgogoro wa ardhi watu 5 wameuwawa kwa kupigwa na "wananchi wenye hasira"

Inasikitisha kuwa sasa uhai wa mtu hauna thamani hata kidogo Tanzania hii. Polisi wanalipwa mshahara wa kazi gani?
 
when you loose faith you also loose hope,
when you loose hope you then loose what is mean to be a human being.
many Tanzanian today are becoming so!
nasikitika kusema hivi lakini baada ya Mwalimu kuondoka tukawa tunajiendea tu yaani "mwenye nguvu mpishe" na sasa imefikia sehemu "wasio na nguvu" wamekuwa wengi mno na wanajaribu kutumia theory hiyohoyo ya "mwenye nguvu..." na matokeo yake ni kama haya!!
Ukitaka kujua kuwa MATUMIZI YA AKILI Tanzania yamepungua angalia kwenye mikusanyiko ya kijamii. Mfano matumizi (upanadaji) wa daladala, kukuta vibao vya 'usikojoe hapa' katikati ya miji-kujisaidia ovyo, utunzaji wa miundombinu ya jamii kama mabomba ya maji, kutupa taka hovyo wakati kuna mapipa ya taka. Hayo yote ni 'variables' ambazo climax yake ni hii picha.
 
Wako wapi wanaotetea haki za binadam? Tuyakemee haya kwa nguvu zote? Tusiishie kutetea haki za wanawake na watoto tu.......!!!
 
Back
Top Bottom