warning: disturbing image...sheria mkononi?

Mjiulize mbona hayatokei katika nchi za wenzenu?? wananchi wanapofikia hapa ujue wamepoteza imani!! watu wanatafuta kwa jasho na wengine wanatumia jasho kidogo tu kuchukua kile kilichopatikana kwa jasho jingi..ukiomba dola ifanye kazi yake unakuta dola nayo inakutaka utoe tena jasho vinginevyo hakuna msaada..hapo ndipo inafikia watu kutumia njia ya mkato kama hizi za kurahishisha maamuzi tu (kuiba si kosa lenye kustahili adhabu ya kifo) lakini wananchi hawajui haya kutokana na mfumo wa maisha uliowekwa na wenye mamlaka..turekebishe haya kwa kuangalia yale yajayo mbele, hali itazidi kutisha..
 
Hivi CCM sijui hawajui kuwa Hungry people are angry people!!!!
 
Saint Ivuga usiwe na miono ya kurusha lawama zote kwa chama chochote mambo kama uhalifu,tabia mbaya au maadili mabovu inatokana na asili ya mtu mwenyewe,malezi na hata mazingira kwa machache.
 
Juzi mgogoro wa ardhi watu 5 wameuwawa kwa kupigwa na "wananchi wenye hasira"

Inasikitisha kuwa sasa uhai wa mtu hauna thamani hata kidogo Tanzania hii. Polisi wanalipwa mshahara wa kazi gani?
Wanalipwa mshahara wa kuzuia mikutano ya CHADEMA na kukamata wafuasi wa CHADEMA.

Nyie wengine fanyeni mnachotaka.............Polisi wapo busy kwenye Siasa, wanatekeleza Ilani ya CCM.

Unafikiri kama Raia wanaua na polisi hawachunguzi nini kimetokea, na baadae wakaanza kujipanga kulinda maeneo korofi kwa vibaka.......haya hayawezi kutokea.
 
Umeshawahi kuonja machungu ya kuadhibiwa wakati hujafanya kosa? Na adhabu yenyewe iwe kifo.

Uchubgu wa kuibiwa hautoi mamlaka ya kuua, Never ever?????
Mkuu umeshawahi kusikia kama gari yako imewashwa.......na ukaangalia dirishani ukaona ileeee inakata kona???!!!

umeshawahi kuwa unarudi home, una alfu tano tu na huna hela ingine, hata ya kula kesho, na ukapewa roba, watu wakachukua hiyo buku 5, then wakakutandika mabapa kwamba mwanaume mzima unatembea na buku tano tu??

Mkuu.......wezi/vibaka/majambazi/wanyang'anyi sio rafiki zangu.........akiniibia na kumuona yeye ndo ananiibia, haijalishi, nikimpatia timing nammwaga utumbo fasta.

Nikikuta mtu anapigwa na random people na hakuna jinsi ya kuhakiki kwamba ni kibaka, sitampiga wala kunyanyua mkono wangu.
 
kuua mtu ni mbaya. Ila kuna mazingira yanayopelekeaga watu wasiwe na huruma na wanaua binadamu kama mnyama...
 
Bila kufanya hivyo wizi hautaisha hiyo ndio dawa ya wezi,mkimpeleka polisi anahonga pesa kesho mnamkuta kitaani akiendelea na kazi yake ya wizi
 
angeiba kwa fisadi wala asingeuwawa
ila kwa mfuja jasho mchumia juani hakika mauti lazima yakukute!
 
Mkuu umeshawahi kusikia kama gari yako imewashwa.......na ukaangalia dirishani ukaona ileeee inakata kona???!!!

umeshawahi kuwa unarudi home, una alfu tano tu na huna hela ingine, hata ya kula kesho, na ukapewa roba, watu wakachukua hiyo buku 5, then wakakutandika mabapa kwamba mwanaume mzima unatembea na buku tano tu??

Mkuu.......wezi/vibaka/majambazi/wanyang'anyi sio rafiki zangu.........akiniibia na kumuona yeye ndo ananiibia, haijalishi, nikimpatia timing nammwaga utumbo fasta.

Nikikuta mtu anapigwa na random people na hakuna jinsi ya kuhakiki kwamba ni kibaka, sitampiga wala kunyanyua mkono wangu.

Are you serious????? I think you dont even listen to what you are talking, watu wameiba EPA, watu wameiba Dowans, watu wameiba hela za rada, watu wanaiba kujenga nyumba ya RC mtwara Good I.4 billion for 3 years, watu wameiba hela za mafunzo tume ya mawasiliano, watu wameiba meremeta, watu wameiba twiga, watu wanaiba dhahabu geita na kila mahali. Una maana hujawapata hao wote kama bado una usingizi wa PONO ndugu yangu. Anza kuwalia timming hao na utoe hayo matumbo, kwa sababu kwa njia moja au nyingine wamekuibia.

As to mob justice that part you are right, absolutely right, you just dont involve yourself before asking.
 
Tatizo linaanzia pale waarifu wanapopelekwa kwenye vyombo vya dora alafu jamaa anaachiwa kwa kutoa kitu kidogo na jamaa akirudi masikani anakuja kulipiza kisasi wakati yeye ni mharifu siungi mkono ila police wabadilike tutamalizana jamani!!
 
This is too much aisee hata kama kaiba nini thamani ya utu na vitu vitu vinaweza patikana lakini utu haupatikani tena.Si wote wanaiba wanapenda watu wana matatizo wandugu inawezekana hapo alikuwa na mgonjwa hospitali kwa hiyo alikuwa anatafuta hela ya kulipa.Anyway watanzania napenda washauri hata kama una matatizo kiasi gani jaribu kuomba kwa mtu yeyote wapo watu wenye moyo watakusaidia kwani kuiba unahatarisha maisha yako watu wamechoka aisee watakuua
 
unachoongea ni kweli lakini hawa jamaa washawahi kukuibukia wewe ukiwa an mkeo na mwanao wa kike? utapona?
 
Haya ni matokeo ya Mahakama kutenda haki lakini haionekani haki ikitendeka!
 
Back
Top Bottom